Fred Lowassa: Baba hakuwahi kumsaliti rafiki yake

Fred Lowassa akihojiwa na Millard baada msiba wa Lowassa ameongea mambo kadhaa kuhusu baba yake. Moja ya swali aliloulizwa ni kipi hawezi kusahau kutoka kwa baba yake.

Fred amesema kitu kikubwa alichokuwa nacho mzee wake ni 'Loyalty' akiita kama 'kufa na mtu wako' kwani katika historia yake ya uongozi yote hajawahi kumsaliti rafiki hata mmoja na ndio kilichomjengea heshima mzee Lowassa na amewafia rafiki zake wote kwenye siasa.

======

Swali(Mwandishi Paschal): Kipi ambacho hutasahau kutoka kwa Baba?

Fred Lowassa: Niseme Loyalty, yaani ni mtu ambaye mimi amenifundisha kiswahili wanaita 'kufa na mtu wako'. Yaani akisema Paschal ni rafiki yangu hata aje nani kumwambia nini, anasema hapana, mimi Paschal namuamini ni rafiki yangu na angekaa nae mpaka mwisho na ndio jambo limemjengea heshma na upendo kwa watu wengi sana kwasababu yeye hakuwahi kumsaliti rafiki yake hata mmoja katika historia yake ya uongozi yote, ni mtu ambae amewafia rafiki wote mwanzo mpaka mwisho.

Hilo ni jambo kubwa na la kipekee sana ambalo kwakweli kwa wanasiasa ni wachache sana wenye kipawa hicho. Amewafia watu wake wote vizuri sana, nadhani hilo jambo mimi nimejifunza, namshukuru Mungu sana.
Yuda Iskarioti alijinyonga na kutupa vipande vya fedha alizipewa, je huyu atafanyaje
 
Kipo wapi sasa? Nchi hii hakuna kiongozi mwenye kulitamka hilo neno toka moyoni .
Country first is not for Africa. Roho mbaya na unafiki mkubwa wa siasa za kichawi ndiyo msingi mkuu wa maisha yao.
Imebadilishwa na HE Samia Suluhu Hassan ambaye amejaribu kuyaleta makundi yote pamoja...Yeye amefanya ila makundi ndiyo yanagoma kuunganishwa
 
Maisha ya dunian ni survive for the fittest. Hakuna anaekupenda Zaid ya Mungu wako na hakuna anaetaka umpite kwa utajiri au umashuhuri zaid ya baba yako. Ukijua hilo life utalibalance ndio maana kuna kitu inaitwa mikataba. Kwangu Mimi hakuna sehemu tulipoteza chance muhimu kama 2005. Lowassa angeshika urais baada ya mkapa hii nchi ingekuwa mbali sana. Watu wakaacha kiongoz wakamweka msanii. Alipoingia ikulu kakuta hazina imejaa pesa akaanza kugawa kila Kijiji million 50. Wajanja wakapita nazo. Baada ya lowassa wamweke magufuli hii nchi ingekuwa Singapore. Lakin ndio hivyo tena tunachojua ni simba na yanga lakin kujua tutakuwa wapi miaka 40 ijayo ni ngumu. Ndio maana vitu vya hovyo vinapewa vipaumbele vile vya ukweli hakuna mwenye muda navyo. Kitu pekee tunachozalisha kwasasa ni chawa.
 
Fred Lowassa akihojiwa na Millard baada msiba wa Lowassa ameongea mambo kadhaa kuhusu baba yake. Moja ya swali aliloulizwa ni kipi hawezi kusahau kutoka kwa baba yake.

Fred amesema kitu kikubwa alichokuwa nacho mzee wake ni 'Loyalty' akiita kama 'kufa na mtu wako' kwani katika historia yake ya uongozi yote hajawahi kumsaliti rafiki hata mmoja na ndio kilichomjengea heshima mzee Lowassa na amewafia rafiki zake wote kwenye siasa.

======

Swali(Mwandishi Paschal): Kipi ambacho hutasahau kutoka kwa Baba?

Fred Lowassa: Niseme Loyalty, yaani ni mtu ambaye mimi amenifundisha kiswahili wanaita 'kufa na mtu wako'. Yaani akisema Paschal ni rafiki yangu hata aje nani kumwambia nini, anasema hapana, mimi Paschal namuamini ni rafiki yangu na angekaa nae mpaka mwisho na ndio jambo limemjengea heshma na upendo kwa watu wengi sana kwasababu yeye hakuwahi kumsaliti rafiki yake hata mmoja katika historia yake ya uongozi yote, ni mtu ambae amewafia rafiki wote mwanzo mpaka mwisho.

Hilo ni jambo kubwa na la kipekee sana ambalo kwakweli kwa wanasiasa ni wachache sana wenye kipawa hicho. Amewafia watu wake wote vizuri sana, nadhani hilo jambo mimi nimejifunza, namshukuru Mungu sana.
Amedanganya eti alikuwa wanawasiliana sana hata baada ajali ya siasa mtu ameumwa miaka 3 bila hata kupita hospital kumjulia hali hii inaitwaje kama sio unafiki kiwango cha SGR? JK ni mnafiki hana la kusema....juu hili...mengine watajuana wenyewe ila kumjulia hali hapanaa huo unafiki.....hata msibani ameenda kufanya nini? Ameenda nyumbani akaandika kitabu akaondoka hata ndani hakuingia....kumpa pilw mjane....aishi milele na unafiki wake
 
Hili jibu la Fred limekuja kupigilia msumari wa mwisho kwa nini jina la JK halikutajwa kwenye mazishi ya Lowassa.

Kumbe JK anaonekana msaliti kwenye familia ya Lowassa. Palikuwepo na muda mrefu wa kurekebisha haya mambo, sijajua kwanini yakaachwa mpaka yafike hapa.

Funzo nimelipata hapa, kumbe duniani kuna wakati mnaweza kuishi kama marafiki, lakini mwishowe mkaja kuzikana maadui.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Ujinga na uzembe wa J.K ndio ulifanya kwa mara ya kwanza Urais usiwe na mtu alieandaliwa ndio tukapitisha mtu haraka haraka. Tukaja kupata Rais wa kwanza alieleta ukabila wa wazi wazi katika serikali . Na sasa tunaona S.S.H anafuata nyayo za Rais aliyepita. J.K angekubali kumalizana maana Lowasssa ndiye aliyekuwa amejiandaa vizuri kwa ajili ya Uchaguzi wa 2015. Vile vile kwa kuwa walitofautiana Uongozi wake ungekuwa wa kitofauti na J.K. Hata J.P.M huko aliko akiangalia Serikali inavyoendeshwa, Kizimkazi imekuwa Chato mpya na Watu wa visiwani wamekuwa Wasukuma wa zama hizi atashangaa ana kujilaumu kwa nini hakusikilizi washauri. Hakuna nchi ambayo ina machafuko ilipata Uhuru kwa njia ya amani. Unapoongoza viongozi wajao wata-refer uongozi wako katika kufanya maamuzi yao. Utamwambia nini Mama kuhusu kizimkazi mama wakati J.P.M alijenga Airpot Chato ?
 
Hili jibu la Fred limekuja kupigilia msumari wa mwisho kwa nini jina la JK halikutajwa kwenye mazishi ya Lowassa.

Kumbe JK anaonekana msaliti kwenye familia ya Lowassa. Palikuwepo na muda mrefu wa kurekebisha haya mambo, sijajua kwanini yakaachwa mpaka yafike hapa.

Funzo nimelipata hapa, kumbe duniani kuna wakati mnaweza kuishi kama marafiki, lakini mwishowe mkaja kuzikana maadui.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Wakati lowasa anarudi ccm.hatukumuona mzee wa Msoga alipongeza pale ikulu
 
Only my close family ndio rafiki zangu, zaidi ya hapo mimi sinaga rafiki, i employ people ( hire) and fire once kuna ujinga anafanya, tokea malaika Mkuu ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Mwenyezi Mungu na akageuka shetani, mimi sitaki urafiki na kiumbe chochote, except my close family, na hii imeniletea furaha kubwa, na binadamu usimwamini kamwe
 
Maisha ya dunian ni survive for the fittest. Hakuna anaekupenda Zaid ya Mungu wako na hakuna anaetaka umpite kwa utajiri au umashuhuri zaid ya baba yako. Ukijua hilo life utalibalance ndio maana kuna kitu inaitwa mikataba. Kwangu Mimi hakuna sehemu tulipoteza chance muhimu kama 2005. Lowassa angeshika urais baada ya mkapa hii nchi ingekuwa mbali sana. Watu wakaacha kiongoz wakamweka msanii. Alipoingia ikulu kakuta hazina imejaa pesa akaanza kugawa kila Kijiji million 50. Wajanja wakapita nazo. Baada ya lowassa wamweke magufuli hii nchi ingekuwa Singapore. Lakin ndio hivyo tena tunachojua ni simba na yanga lakin kujua tutakuwa wapi miaka 40 ijayo ni ngumu. Ndio maana vitu vya hovyo vinapewa vipaumbele vile vya ukweli hakuna mwenye muda navyo. Kitu pekee tunachozalisha kwasasa ni chawa.
Magufuli ameiharibu nchi vibaya sana ukiangalia hata hizi siasa za uchawa na kuzunguka nchi nzima na msururu wa magari yeye ndio ameanzisha. Alikuwa na kasoro kubwa sana ya kuigawa nchi na kutofuata ushauri wa wataalamu. Hauwezi kuwa na kiongozi anakiuka maadili na wewe unamkingia kifua kama Rais. Hapo lazima utaleta matatizo makubwa sana. Mambo yalikuwa mengi C.A.G prof Assad ni mtu makini sana. Lakini JPM akaja kukataa ushauri wake na kumchafua. Hauwezi kufanya kila kitu wewe mwenyewe lazima uwe na timu ya watu makini na wenye maono. Ukichagua team kisa ni kabila moja na wewe au mnatokea kanda moja hauwezi kufanikiwa hata siku moja. Maana hata ukiambiwa mabaya ya watu wako hautoamini. Alimuamini sana Makonda, Kigangwala wakaja wakamwuangusha vibaya sana. Mwishowe alikosa mtu wa kumteua mpaka Bashiru Ally alipewa vyeo viwili. JPM alitakiwa ajenge team ya watu ambao wako competent katika nafasi zao. Mwisho wa siku akaja kumkaribisha Rostam na kumpa mradi wa gesi na kumpa kiwanda Morogoro. Rostam alipiga hela kipindi cha Kikwete, Magufuli na Samia. Tujiulize kuna tofauti katika awamu hizi. Tofauti ya Magufuli na kikwete ni Wizara tu. Kikwete alitoka wizara yamambo ya nje kwa hiyo upigaji wake ulitegemea kusafiri na kuomba misaada. Na JPM alitoka wizara ya ujenzi upigaji wake ulitokana na miradi ya ujenzi. CCM kama chama kikuu cha serikali inabidi iunde team hauwezi kuendesha nchi ukiwa na kiongozi mwenye elimu ya kuunga ya form four katika kamati kuu ya chama. CCM waamke waiangalie Rwanda na pia waaangalie CV za viongozi wao. Haya mambo ya uchawa na yalishafanyika enzi za Mobutu hakuna jipya duniani. Tusipoangalia tukiendelea hivi kila Rais anaekuja na kumkandia Rais aliyepita na kuwaza kupiga hela. Ndani ya miaka kumi ijayo tutakuwa kama Congo sitanii. Maana uzembe unaanza polepole unakuja kushtuka mambo yameshaharibika.
 
Fred Lowassa akihojiwa na Millard baada msiba wa Lowassa ameongea mambo kadhaa kuhusu baba yake. Moja ya swali aliloulizwa ni kipi hawezi kusahau kutoka kwa baba yake.

Fred amesema kitu kikubwa alichokuwa nacho mzee wake ni 'Loyalty' akiita kama 'kufa na mtu wako' kwani katika historia yake ya uongozi yote hajawahi kumsaliti rafiki hata mmoja na ndio kilichomjengea heshima mzee Lowassa na amewafia rafiki zake wote kwenye siasa.

======

Swali(Mwandishi Paschal): Kipi ambacho hutasahau kutoka kwa Baba?

Fred Lowassa: Niseme Loyalty, yaani ni mtu ambaye mimi amenifundisha kiswahili wanaita 'kufa na mtu wako'. Yaani akisema Paschal ni rafiki yangu hata aje nani kumwambia nini, anasema hapana, mimi Paschal namuamini ni rafiki yangu na angekaa nae mpaka mwisho na ndio jambo limemjengea heshma na upendo kwa watu wengi sana kwasababu yeye hakuwahi kumsaliti rafiki yake hata mmoja katika historia yake ya uongozi yote, ni mtu ambae amewafia rafiki wote mwanzo mpaka mwisho.

Hilo ni jambo kubwa na la kipekee sana ambalo kwakweli kwa wanasiasa ni wachache sana wenye kipawa hicho. Amewafia watu wake wote vizuri sana, nadhani hilo jambo mimi nimejifunza, namshukuru Mungu sana.
Ni kweli sikumbuki yeye kumgeuka rafiki yake mkubwa jk sema baadhi ya maelewano huenda yalikua kwa jk ngumu kutunza baada ya kua rais.
 
Back
Top Bottom