Sasa wewe unabishana na mtoto wa Marehemu? Wao ndio wanajua ipi ni stahili yao na kipi walisaidiwa
Hakuna anayebishana na mtoto wa marehemu kwa sababu stahiki za viongozi wakuu ziko wazi na zimeainishwa katika sheria ya " Political Service Retirement Benefits Act ya mwaka 2015 ( Cap.225. R.E.2015) ambayo inasema mtu aliyewahi kuwa Waziri Mkuu anastahiki zifuatazo:
1. Posho itakayofanana na 80% ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyopo.
2. Gratuity itakayokuwa sawa na nusu ya pesa alizopokea kama mshahara wakati akiwa kazini.
Schedule C ya hiyo sheria inasema:
1. Yeye na mwenza wake watakuwa na pasi za kidiplomasia.
2. Atagharamiwa matibabu ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
3. Gari moja lenye uzito usio pungua tani 3 ambalo litakuwa linabadilishwa kila baada ya miaka mitano.
4. malipo yatakayotosha kulipa mishahara kwa wafuatao kwa kima cha chini:
a. Personal Assistant mmoja.
b. Mpishi mmoja.
c. Dobi mmoja.
d. Mfanyakazi wa ndani mmoja.
e. Shamba boi mmoja.
f. Dereva mmoja.
5. matumizi ya VIP lounge.
6. Gharama zote za kuzikwa.
Ibara ya 14 (2) inasema yeye na familia yake watapewa ulinzi wote unaostahili.
Sheria pia inasema kuwa wanaohusika ni wale wote waliowahi kuwa mawaziri wakuu bila caveats yeyote.
Mtoto wa marehemu anaweza kujua zaidi kuhusu utajiri na mali za mzazi wake lakini sio kwenye stahiki zake. Labda kama aliwahi kunyang'anywa kinyume na sheria na Rais akamrudishia.
Amandla...