Fredrick Lowassa: Kama sio Rais Samia, Baba asingefika juzi

Fredrick Lowassa: Kama sio Rais Samia, Baba asingefika juzi

Hao watoto wasiruhusiwe press yoyote kwa sasa, maana mpaka hapo wameonesha bado akili haijatulia!

Kawaida, Kwa Mungu kila kitu kimepangwa kwenye maisha yetu, sasa huwezi kusema eti Rais Aweza kurefusha uhai wa mtu ambao Mwanadamu amepewa na Mungu kama dhamana tu

Ni kufuru,

Wasiruhusiwe kuongelea chochote kumhusu baba yao
Kusifiwa Rais kunaumiza moyo wako?. Vipi kuhusu zile sifa anazopewa akiwa mbali kabisa na uwezo wako wa kupata habari?.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]kbsaa yaani cdm wamechukizwa na speach hii
Kikubwa kutenda mema. Kujua baada ya kufa kuna maisha. Maisha ya kuhesabiwa dhambi na thawabu. Atakaefuzu ni yule muumini wa kweli. Jukumu langu na lako kumtafuta nani muumin wa kweli?
 
Hivi nauliza kuna Mwanasiasa ambae alimzidi Marehemu kwa Moyo wa kutoa?

Lowassa hakuwa na mkono wa Birika sio hawa wa sasa ambao wao ni mwendo wa kwenda kuzificha CHINA halafu wanagawana wao kwa wao.

Wengi wanaoenda kuzika Monduli hawaendi Kivyama wala Kiitikadi wanaenda kumzikq Binadamu mwenzao.
Kama hawa wahutu walivyogawana hela za plea bargaining na kwenda kuzificha China na Mauritius
JamiiForums1190257988.jpg
JamiiForums839866055.jpg
JamiiForums291438778.jpg
JamiiForums-1904098435.jpg
 
Mpaka ww chawa umeona huu ni uchawa uliovuka mipaka!
Baki na tafsiri yako isiyo na ukweli wowote, na bahati mbaya kabisa nilishakataa utumwa wa kukubali kila lisemwalo

Chadema wakikosea nawaponda, CCM siwapendi hata kuwaona, naamini katika fikra pevu na siyo kushikiwa akili mkuu
 
"Lakini katika vita yake hii ya kupigania maisha yake lazima niseme kipekee naomba sana kutoa shukrani za familia kwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, niseme ukweli kutoka moyoni, kama isingekuwa mama Samia Suluhu Hassan baba yetu asingefika hata hiyo juzi, mama Samia amekuwa ni ndugu, amekuwa mzazi na mlezi wetu hatuna cha kumlipa" - Fredrick Edwad Lowassa, Mtoto wa Hayati Lowassa

Waziri Mkuu Mstaafu anatunzwa na serikali hata baada ya kustaafu, mambo ya sijui asante mama n.k ni sifa zilizopitiliza...

Unless labda Fred anataka kusema wakati wa JPM mzee alibaniwa stahiki zake, na SSH kazirejesha zote...
 
Nadhani alipaswa kusema kuwa isingekuwa Mwenyezi Mungu kumtumia mama Samia then......,ila inawezekana tension za msiba na nini,tumemsamehe,yuko kwenye machungu ya kufiwa,ameshindwa kupangilia maneno vizuri.
 
Samia ni mwema sana kwa matajiri/watu maarufu na wanasiasa lakini walio chini kabisa kila siku wanazidi kulia kwa hali mbaya na ugumu wa maisha.
Huwezi pendezesha makundi yote,
aidha unahudumia matajiri wachache au masikini wengi, ulimwengu wote iko hivyo.

JK alipendwa zaidi na Matajiri, JPM alipendwa zaidi na masikini, Nyerere alijinasibisha zaidi na masikini. Marekani, Obama sera zake mf za OBAMACARE zililenga zaidi masikini au marginalized groups Marekani, Trump yeye alisimama zaidi na mabwenyenye.
 
Back
Top Bottom