Fredrick Lowassa: Kama sio Rais Samia, Baba asingefika juzi

Fredrick Lowassa: Kama sio Rais Samia, Baba asingefika juzi

Hao watoto wasiruhusiwe press yoyote kwa sasa, maana mpaka hapo wameonesha bado akili haijatulia!

Kawaida, Kwa Mungu kila kitu kimepangwa kwenye maisha yetu, sasa huwezi kusema eti Rais Aweza kurefusha uhai wa mtu ambao Mwanadamu amepewa na Mungu kama dhamana tu

Ni kufuru,

Wasiruhusiwe kuongelea chochote kumhusu baba yao

Mpaka ww chawa umeona huu ni uchawa uliovuka mipaka!
 
Mama anaupiga mwingi. Kila sehemu yenye changamoto yupo. Maskini wengi mnapenda kumtaja Mungu hata kwenye mambo yaliyo kwenye uwezo wa binadamu. Mungu alitupa akili tuzitumie kwahiyo tufanye wajibu wetu huku tukimwomba Mungu. Kama mnabisha nenda katoe
mashine ya oxygen kwa mgonjwa kisha subiri miujiza. Mama Samia alitimiza wajibu wake ndo maana Fred kashukuru.
 
Kwa hiyo ukiwa na figo mbovu nikakutolea yangu .ukisema nimekuonhezea uhai umemkufuru mungu
Yawezekana ukanitolea yako na nikafa wakati wa operesheni ya kuniwekea. Au yawezekana nikawekewa figo yako ikaleta complications kuliko nilivyokuwa nayo yangu mbovu, nikafa siku chache baadaye. Sasa sijui utakuwa umeniongezea au umenipunguzia muda wa kuishi
 
Chadema watakuja kumponda huyo mtoto...na kutukana...wao walitaka kusikia lawama zinaenda Ccm na ikiwezekana Kwa Rais Samia

Malizia kwa kusema walitaka lawama zienda kwa Samia maana ni muisilamu.
 
Hii ni zaidi ya kufuru, kumpa mwanadamu mwenzako utukufu sawa na mwenyezi Mungu.

Badala ya kuwashukuru madaktari yeye anashukuru Mama .... kwa vile tu pesa ya nchi hii haitoki bila mkono wa Mama.Mungu mtu wa Bongo....!!

Yaani Kijana anasauhu kuwa baba yake alikuwa ni Waziri Mkuu, hivyo anastahili huduma zote za matibabu kama first class citizen.

Halafu wakienda kuzika Monduli watamshukuru Maza tena kwa kuwasaidia mazishi .... hii Tanzania yetu ni balaa tupu.
 
Pamoja na utajiri tulioaminishwa anao, pamoja na pension yake kama kiongozi mwandamizi mstaafu, pamoja na incentives zote anazopewa na serikali, bado SSH alimpa msaada.

Asiye nacho ananyimwa hata kile kidogo, mwenye nacho anapewa zaidi.

Pole kwa familia.
 
Chadema watakuja kumponda huyo mtoto...na kutukana...wao walitaka kusikia lawama zinaenda Ccm na ikiwezekana Kwa Rais Samia
Hayo ni mawazo yako potofu,mkipishana mawazo huko CCM lazima muitaje Chadema, una huko CCM nyie woooote mko programmed kufikiri kila kitu sawasawa nyie ni misukule? Chuki yako iliyopitiliza kwa Chadema imepunguza uwezo wako wa kufikiri, yaani umejishusha sana hapa jukwaani.
 
Mama anaupiga mwingi. Kila sehemu yenye changamoto yupo. Maskini wengi mnapenda kumtaja Mungu hata kwenye mambo yaliyo kwenye uwezo wa binadamu. Mungu alitupa akili tuzitumie kwahiyo tufanye wajibu wetu huku tukimwomba Mungu. Kama mnabisha nenda katoe
mashine ya oxygen kwa mgonjwa kisha subiri miujiza. Mama Samia alitimiza wajibu wake ndo maana Fred kashukuru.

Huu uchawa huko ccm uko muda mrefu, ila baada ya dhalimu magu kuwa rais, uchawa ukawa unafanyika hadharani bila aibu. Kwa Sasa wanaccm umeupdate uchawa wenu Hadi mnafanya kufuru.
 
Acheni siasa zenu, kuna mazingira ambayo unaweza kumpongeza mwanadamu kwa juhudi zake alizozifanya japo kifo tunaamini kimepangwa na Mungu,, na wale waliotekwa na kufa mbona hamkusema ni mipango ya Mungu? Kwa mfano angesema kwamba baba yao angekua bado anaishi mpaka sasa kama sio Samia,, pia mngesema ni mipango ya Mungu??
 
Matajiri ndio huwa huwa wanaandamwa na maradhi zaidi kama Shinikizo la Damu Kisukari nk.
Hapana
Maskini wanaumwa hayo maradhi ila kutokana na umaskini wao wanawahi kufariki mfano maskini figo zikifeli lazima ufe tu sababu laki 2 za kila dialysis huwezi kuwa nazo na week unaweza fanya hadi mara tatu

Matajiri wana hela ndo maana wanapambana nayo kwa mda mrefu na hata kwenye dialysis wengi ni wale wenye fedha ndo wanaweza pambana na gharama za dialysis
 
Hayo ni Maradhi yako kutokana na Life Style zaidi Tajiri hatembei kwa miguu anatembea kwa Motokari Tajiri anakula kula vyakula kama unavyojua Diet za Kiafrika mkaango mwingi.

Masikini kwa upande mwingine anatembea kwa miguu sana anakula Ugali na Nsansa akibahatika na Kauzu maskini wa Kiafrika maradhi yake labda Ujinga.
 
Hivi nauliza kuna Mwanasiasa ambae alimzidi Marehemu kwa Moyo wa kutoa?

Lowassa hakuwa na mkono wa Birika sio hawa wa sasa ambao wao ni mwendo wa kwenda kuzificha CHINA halafu wanagawana wao kwa wao.

Wengi wanaoenda kuzika Monduli hawaendi Kivyama wala Kiitikadi wanaenda kumzika Binadamu mwenzao.
 
Back
Top Bottom