Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Rais alimpa MBOWE pole baada ya kufiwa na Kaka yake, je Kuna uhusiano gani Kati ya rais na gaidi? Je Rais alikuwa misleaded au vyombo vya kumpasha rais habari za kinintelijensia ndio vilikuwa usingizini?
Zaidi ya hapo ni kwamba Gaidi Mbowe, ambaye tayari polisi walishampasha habari za ugaidi wake, kaachwa asafiri kwenda Mwanza na kuandaa kongamano.
Gaidi huyu analelewa na polisi hadi anapotishia kuendesha kongamano ndipo ugaidi wake uonekane kuwa hatari?

Hawa polisi wanajuwa waTanzania ni watu wasiochukulia mambo wa uzito wake.

Hata hawakumbuki wale magaidi waliomteka Mo yaliishia wapi? Na hakuna aliyeendelea kuuliza juu ya habari hizo hadi sasa.

Tunalo jeshi la polisi makini kweli kweli CCM inapohusika.
 
HAKUNA mtu anakufa kabla ya "muda".

Kufa kwako ndio muda wako umefika.

Kila kitu kina mwanzo na mwisho.

Narudia tena ,JPM aliishi na akatutimizia mengi mazuri ametuachia mengi mazuri tu, legacy yake inaishi.

1)Pale Ubungo
2)Pale Mfugale Tazara
3)Stendi ya Mbezi

HIZO NI ALAMA KUBWA

Sasa sijui wewe na mimi tutaacha kipi kwa wengi?

#KaziInaendelea
#NchiKwanza
 
Tulimkubalia mama alipotuonya tusihoji kuhusu kifo cha jiwemagu. Hawa polisi hawakumsikia?

Kwa akili yako, hata kama ana reasonable suspicion of foul play, ni kiongozi gani wa Serikali angeweza kuhamasisha umma kuhoji kifo cha Rais? Labda kama alitaka nchi iingie kwenye machafuko!
 
Hata kwa DC Sabaya wapo walio amini na wapo ambao hawakuamini lkn leo hii yupo mbele ya mahakama. Mahakama ndio Jukumu lake kuamua kama Mbowe na wenzake ni Magaidi au la.
tuache sheria ifanye kazi yake.
Mbowe na wenzake sio Malaika, ni binaadamu kama walivyo binaadamu wengine, mambo yake mengine ya siri hatuyajui.
 
Salam Wanandugu

Kwanza hilo mnalosema kwamba Mbowe alihusika na kifo cha Magufuli ni uongo. Kumuua rais wa nchi ni UHAINI na si ugaidi kama wasemavyo wakina fulani wa humu jukwaani.

Ugaidi ni upi?

Makosa ya ugaidi ni yale yale ya siku zote kama tuyajuavyo huko mashariki ya kati.

Kama vile kupanga na kutekeleza mashambulizi dhidi ya raia au miundombinu ya uma

Mbowe ataunganishwa na akina nani?

Mwenyekiti yeye ataunganishwa na baadhi ya majamaa waliotuishwa mzigo wa kariakoo kuwaka Moto japo kuwaka Moto kariakoo linaweza lisiwe tukio la kigaidi lakini ndio Mbowe atapewa hilo zigo ili wamsumbue sumbue
 
Tulivyokua fomfoo
Division one na two walienda fomfaiv.
Division three walipeleka vyuo Kama vya medical, misitu, technical college etc.
Division foo za mwanzo mwanzo ualimu.
Division foo point 33 yaani Ile ya mwisho yaani wale kichwa ngumu hata mwalimu aongee kimakonde walikua hawaelewi kitu lkn walikua wepesi kutumia nguvu kuliko akili walienda UPOLISI
Kama mtakumbuka Ile selfom ya fomfoo hata salary ya UPOLISI haikuonyeshwa paliandikwa VARIABLE.
I rest my case
 
Asanteni jeshi la police, mnafanya kazi nzuri sana. Huyu faru John na genge lake la mafia mwisho wao umefika.
 
Division three walipeleka vyuo Kama vya medical, misitu, technical college etc.
Siyo kweli, kuna division one na two walienda technical college pia. Naona ID yako ya hapa JF inaeleza mengi.
 
Pamoja na mengine yote...... Uongozi ni dhamana. Uongozi ni uwajibikaji. Unapokua kiongozi huwezi kujitoa kwenye mambo yahusuyo unaowaongoza sababu wao ni watendaji chini yako na wanatekeleza yale mliyokubaluana kwa ruhusa yako.

Ni ngumu sana kumtenganisha mwenyekiti na haya mambo, yeye mwenyewe hajawahi kuyakemea na hii inamaanisha anayajua na kuyabariki

Your browser is not able to display this video.


Wahenga wsnasema - Mchelea mwana kulia hulia yeye!
 
kumbe alianzisha harakati za katiba mpya kwa maksudi tu ili ikitokea anakamatwa na polisi basi iwe rahisi kutuhadaa na kuuhadaa ulimwengu eti kuwa kakamatwa kwa kudai katiba mpya!! aisee!!! Mbowe na kundi lake ni zaidi ya majambazi!!
Tunamuomba Msajili wa Vyama akichunguze kwa makini hiki chama cha Chadema inaonekana kuna mtandao mkubwa wa kigaidi/kihalifu/kijambazi nchi nzima, Jeshi letu la Polisi wafanye uchunguzi kwa umakini mkubwa ili kubaini mtandao wote ili washughulikiwe kikamilifu kabla hawaja sababisha madhara kwa wananchi.
Amani ya Tanzania ni Muhimu zaidi kuliko chama cha kigaidi.
Mungu ibariki Tanzania.
 
kumbe alianzisha harakati za katiba mpya kwa maksudi tu ili ikitokea anakamatwa na polisi basi iwe rahisi kutuhadaa na kuuhadaa ulimwengu eti kuwa kakamatwa kwa kudai katiba mpya!! aisee!!! Mbowe na kundi lake ni zaidi ya majambazi!

Tunamuomba Msajili wa Vyama akichunguze kwa makini hiki chama cha Chadema inaonekana kuna mtandao mkubwa wa kigaidi/kihalifu/kijambazi nchi nzima, Jeshi letu la Polisi wafanye uchunguzi kwa umakini mkubwa ili kubaini mtandao wote ili washughulikiwe kikamilifu kabla hawaja sababisha madhara kwa wananchi.

Amani ya Tanzania ni Muhimu zaidi kuliko chama cha kigaidi.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…