Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Kama ni movie ya kiwango Cha chini kelele za nini?
 
Apewe muda ili ajipange kuua watu?

Rais makini haitaji kupewa muda

Ana uwezo kutoa order kila kitu kinafanyika hàta ndani ya mwezi mmoja

Muda wa nini ngoja sasa uone watakavyompiga chini.

Nakwambia akifika 2025 ni bahati sana.
 
Mahakamank ndio itadhibitisha kuwa mbowe na wezake CYO magaidi
 
Interested.....
 
Mwana JF mmoja mtundu wa sheria.
Nadhani aliandika mtiririko baada ya Lisu kutaka kubambikiwa kesi kama hii.
Kijana yule aliandika Alivyodhani mtiririko wa maswali na majibu yatakavyokua huko mahakamani,baada ya mtiririko ule siku ya kesi serikali ikaachana na kesi Ile.

Mfano:
Mbowe unashitakiwa kwa kufanya Ugaidi,
Mbowe: sio kweli,
Unashitakiwa kwa kutaka kuua Viongozi,
Mbowe: kiongozi gani au viongozi gani nilitaka kumuua au kuwaua,
Au kiongozi gani nilikwisha muua,

Hapo ndio penye utata.

Kwa sababu viongozi wengine tuliambiwa walikufa kwa matatizo ya moyo.
Watu watahoji alas kumbe waliuwawa,
Watu watahoji,kumbe viongozi wetu hawako salama kiasi hicho?
Watu watahoji kwa Nini Mbowe hakukamatwa kabla na kwa Nini amekamatwa baada ya kudai katiba mpya?
Watu watahoji mengi,na Yale ambayo serikali haikutaka yajulikane yajulikane.


Wakiendelea kumlazimisha Mbowe akubali tuhuma feki basi Kuna hatari watuhumiwa wakaongezeka na wengine kutoka ndani ya chama tawala.
Hapo ndio tutakua kama kweli tulidanganywa juu ya Vifo vya baadhi ya viongozi wetu.

Namuomba yule mtundu wa sheria atuwekee Tena mtiririko wa maswali na majibu ya tuhuma za Mbowe zitakavyokua huko mahakamani.
 
Basi sawa jeshi la polisi...ngoja tusubiri maana yajayo yanafurahisha
 
Mbona unang'ang'ania kuzungumzia katika hali hasi shule za kata , au una shule ya private imekosa wanafunzi
 
Aje na utundu pia wamabomu ya Arusha.Magaidi wale walifungwa wapi
 
Kwa organ sensitive kama hii palipaswa kuwe na mtu makini wa kuandaa taarifa hizi...

Official doc ina spelling mistakes kibao, tarehe ya mwaka jana, organization ya idea ipo very low... Serious jamani?
 
sasa kwani kabambikwa si ya ukweli acheni police wa deal naye hakuna kesi za kubambia siku hizi
 
uchunguzi uendelee tena kwa umakini na weledi, mtandao wa kigaidi bado upo.........................wapo.........lazima wakamatwe wote, wanao fadhila njama za kuuwa watu/viongozi, wanao ratibu, wanao shauri, wanao tumika n.k, mtandao wote huo lazima uwe terrorized completely.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…