Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Hii movie kuhusu viongozi wa CHADEMA imeandaliwa kwa kiwango cha chini mno na inaabua maswali mengi kuliko majibu kuzidi hata ile ya kutekwa kwa MO.

Na kwakuwa jambo hili linaonekana kugusa hisia za watu wengi na kuvuka mipaka ya nchi huku shinikizo likiongezeka, sitashangaa wakati wiwote wakatafutwa watu wa kubebeshwa lawama na hao wanaweza kuwa ni Sirro na pengine hata Boss wa TISS

Inawezekana Mama asiwe na wazo la kubebesha mtu lawama kwa makosa yake, ila wanasiasa wenzake na ambao ni wakongwe ndani ya chama, wanaweza kumshauri afanye uamuzi wa kuwato watu mbuzi wa kafara ili kulinda image yake.

Tuhuma hizi ni nzito, ngumu kuzithibitisha na inaonekana walizi-underestimate huku dunia ikifuatilia, hivyo ni lazima wajisafishe na katika kujisafusha huko, Sirro ndio anaeweza kuwa wa kwanza kubebeshwa zigo la lawama kwa kuondolewa katika nafasi yake huku Boss wa TISS nae akikalia kuti kavu.

Tusubiri.
Kama ni movie ya kiwango Cha chini kelele za nini?
 
HAO CHADEMA WANGEMPA MAMA ANGALAU MUDA WA MWAKA MOJA AIPANGE SERIKALI YAKE, HALAFU BAADA YA HAPO WAONYESHE KUKOSA UVUMILIVU, TUNGEELEWA. LAKINI RAISI MPYA MADARAKANI SIKU 120 TU WANAMFANYIA VITIMBWI VYOTE HIVYO?!!! HAYO NI MAJARIBU YALIYOPITILIZA. HATA HIZO TAASISI ZA KIMATAIFA HAZIJAAMBIWA UKWELI.
Apewe muda ili ajipange kuua watu?

Rais makini haitaji kupewa muda

Ana uwezo kutoa order kila kitu kinafanyika hàta ndani ya mwezi mmoja

Muda wa nini ngoja sasa uone watakavyompiga chini.

Nakwambia akifika 2025 ni bahati sana.
 
Mahakamank ndio itadhibitisha kuwa mbowe na wezake CYO magaidi
 
Stori yenyewe inamkwenda hivi:
Mtu mmoja was Singida ALIJIDAI yeye mgonjwa,mgonjwa was akili,nadhani. Akalazwa hospitali Mwenge.
Halafu yule mtu akaamka usiku akataka k0653111598uiba,akaiba silaha chache(kutoka kwenye amoury ya Jeshi,Jeshi maana yake,JWTZ),chache maana yake mbili,tatu.
Mlinzi akamstukia,akamshugulikia. Yule mhalifu sasa yuko ahera.
Kuanzia hapo ndio kuna mjadala,watu wanapojaribu kuelewa exactly what happened. Yule mhalifu katoka wapi? Katumwa na Nani? All kinds of questions arise.
Interested.....
 
Mwana JF mmoja mtundu wa sheria.
Nadhani aliandika mtiririko baada ya Lisu kutaka kubambikiwa kesi kama hii.
Kijana yule aliandika Alivyodhani mtiririko wa maswali na majibu yatakavyokua huko mahakamani,baada ya mtiririko ule siku ya kesi serikali ikaachana na kesi Ile.

Mfano:
Mbowe unashitakiwa kwa kufanya Ugaidi,
Mbowe: sio kweli,
Unashitakiwa kwa kutaka kuua Viongozi,
Mbowe: kiongozi gani au viongozi gani nilitaka kumuua au kuwaua,
Au kiongozi gani nilikwisha muua,

Hapo ndio penye utata.

Kwa sababu viongozi wengine tuliambiwa walikufa kwa matatizo ya moyo.
Watu watahoji alas kumbe waliuwawa,
Watu watahoji,kumbe viongozi wetu hawako salama kiasi hicho?
Watu watahoji kwa Nini Mbowe hakukamatwa kabla na kwa Nini amekamatwa baada ya kudai katiba mpya?
Watu watahoji mengi,na Yale ambayo serikali haikutaka yajulikane yajulikane.


Wakiendelea kumlazimisha Mbowe akubali tuhuma feki basi Kuna hatari watuhumiwa wakaongezeka na wengine kutoka ndani ya chama tawala.
Hapo ndio tutakua kama kweli tulidanganywa juu ya Vifo vya baadhi ya viongozi wetu.

Namuomba yule mtundu wa sheria atuwekee Tena mtiririko wa maswali na majibu ya tuhuma za Mbowe zitakavyokua huko mahakamani.
 
Basi sawa jeshi la polisi...ngoja tusubiri maana yajayo yanafurahisha
 
Sijibu maswali ya kipuuzi mimi. Kama unakuja kuandika ujinga wako humu huku ukiwa hujui yale yanayojiri nchini huo ni upumbavu wako.
Nenda kamuulize Mpango sababu za Nchi wafadhili na mashirika ya kimataifa kukata misaada yao kwenye bajeti. Umeathirika na elimu ya kuunga unga ya shule za kata. Eti nimekuuliza maswali hujibu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] wewe kweli ZWAZWA!!!
Mbona unang'ang'ania kuzungumzia katika hali hasi shule za kata , au una shule ya private imekosa wanafunzi
 
Aje na utundu pia wamabomu ya Arusha.Magaidi wale walifungwa wapi
 
Baada ya upekuzi wa Polisi kukamilika nyumbani Kwa M.Kiti Mbowe, tumepokea taarifa za kushtua na kushangaza kuwa Polisi wamemwambia kuwa ataunganishwa kwenye kesi ya Ugaidi na watuhumiwa walioko gereza mojawapo DSM. Tutaendelea kutoa taarifa za kina hapo baadaye.

View attachment 1862953

====

UPDATES;

=====

TAARIFA KWA UMMA

JESHI LA POLISI LAMTUHUMU MWENYEKITI WA CHAMA
MHE.FREEMAN MBOWE NA "MAKOSA YA UGAIDI"

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Freeman Mbowe alifikishwa Dar es Salaam jana majira ya saa tatu usiku chini ya ulinzi wa Polisi , walimpeleka nyumbani kwake Mikocheni Kwa ajili ya kumfanyia upekuzi ambao ulichukua takribani saa mbili na nusu.

Baada ya upekuzi huo Polisi waliondoka na Kompyuta mpakato (Laptop) na Vishikwambi (tablets) za watoto wake, Kompyuta mpakato moja ya kwake na modem ya Internet Kwa ajili ya uchunguzi wao.

Leo majira ya saa Saba mchana Polisi walimfikisha Mhe. Freeman Mbowe Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano na kuchukua maelezo yake.

Polisi walitaka maelezo kutoka Kwa Mhe. Freeman Mbowe kuhusiana na kosa waliloliita 'KULA NJAMA ZA KUTENDA KOSA LA UGAIDI'

Baada ya maelezo hayo ya Polisi Mhe. Freeman Mbowe alitumia haki yake ya kisheria na aliamua kutokutoa maelezo yoyote Polisi kwa mujibu wa Sheria. Baada ya maelezo hayo Polisi wamemrejesha Mhe. Freeman Mbowe katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay ,Jijini Dar es Salaam.

Aidha , viongozi wengine waliokuwa wanashikiliwa Mkoani Mwanza wameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi na baadhi yao walifanyiwa upekuzi nyumbani kwao na vyumba vya hotel ambako walikuwa wameshukia .

Waraka wa Mbowe kwa Watanzania
Mwenyekiti Taifa Mhe. Freeman Mbowe ametuma waraka kwa Watanzania kama ifuatavyo;
"Hatimaye madai ya Katiba Mpya yamenisababishia kesi ya ugaidi, nipo tayari kwa mashtaka ya kuchongwa siogopi. Ninaamini Dunia itaujua ukweli wa kile kinachoendelea Tanzania na kile tunachokipitia Watanzania. Lakini pia itajua ukweli juu ya makosa haya ya kuchongwa.

Natoa wito kwa watanzania kuendeleza mapambano, haki hutafutwa” Mhe.
Freeman Mbowe.”

Imetolewa leo Alhamisi tarehe 22 Julai, 2021.

John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.

=====

UPDATE:

View attachment 1863559
View attachment 1863560
Kwa organ sensitive kama hii palipaswa kuwe na mtu makini wa kuandaa taarifa hizi...

Official doc ina spelling mistakes kibao, tarehe ya mwaka jana, organization ya idea ipo very low... Serious jamani?
 
Mh. Mbowe na wenzake waliwahi tena kutuhumiwa kupanga njama za kulipua vituo vya mafuta ya petrol hapa DSM, lakini wakaachiwa huru. Sasa kwa speed ya ajabu ya jeshi letu shupavu la polisi wanatuhuma mzito za ugaidi. Rais Samia kati ya matamko yake maarufu tangu aingie madarakani ni kutaka jeshi la polisi kuacha kubambikizia wananchi kesi.
sasa kwani kabambikwa si ya ukweli acheni police wa deal naye hakuna kesi za kubambia siku hizi
 
uchunguzi uendelee tena kwa umakini na weledi, mtandao wa kigaidi bado upo.........................wapo.........lazima wakamatwe wote, wanao fadhila njama za kuuwa watu/viongozi, wanao ratibu, wanao shauri, wanao tumika n.k, mtandao wote huo lazima uwe terrorized completely.
 
Back
Top Bottom