Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Leo wanasema heri Magufuli
Wanacdm hawana jema
Tukisema Samia anafanya mabaya ambayo hata Magufuli, pamoja na udikteta wake na ukatili wake wote hakuwahi kufanya, wala haina maana ya kusema heri Magufuli. Magufuli ana mabaya mengi mno, wala hakuna uheri wowote.

Na ni kweli, Samia alifanya mengi tu mazuri mwanzoni, na kwa kuwa sisi ni Waungwana, tulimpongeza, tukamshauri aendelee. Tusiangefanya hivyo, pia tungelaumiwa kwamba kazi yetu kupinga kila kitu, hamna hata jema moja?

Lakibi ni Samia aliyeahidi kukutana na wapinzani, na ni yeye aliyeingia mitini.

Baadae anaibuka na kujitetea eti "ratiba ilibana" mfyuuuu!!
Alipoonya kwamba kuna chokochoko zimeanza, wananchi wawapuuze, alikuwa anamwongelea nani? Acheni upuuzi!
 
Hii issue stearing ni mkwe wa macho kumchuzi,yani siro n tiss wanafanya kazi kwa maelekezo ya mvuvi mcherengwa...mama yupo hapo hajui nini maana ya kua rais
 
Polisi watapeleka ushahidi mahakama itaamua
 
Hivi ikitokea polisi wakashindwa katika ushahid wao,nani anapaswa kuwajibishwa.

Maana wanakuwa kama hawana kazi za msingi hivyo wanajitafutia tu kazi za kufanya.

Kuwa sasa tutengeneze kesi ya aina fulani,tuhangaike nayo kishatuachane nayo.

Nashauri,polisi inaposhindwa kuthibitisha basi wale maafisa inchaji watoswe tu,maana weredi wao utakuwa ni duni.
 
Apewe muda ili ajipange kuua watu?

Rais makini haitaji kupewa muda

Ana uwezo kutoa order kila kitu kinafanyika hàta ndani ya mwezi mmoja

Muda wa nini ngoja sasa uone watakavyompiga chini.

Nakwambia akifika 2025 ni bahati sana.
Nyie dawa yenu ni kutulizwa hivi hivi afu mtaishia kulia Lia kwenye keyboard.
 
Linafungika kwani gaidi kapatikana. Asubili mvua ya miaka 30akitoka viboko vunamhusu pia
 
Umeambiwa pasipo kificho kuwa aliwekewa mtego na kutokana na uzezeta wake amenasa
 
Mpaka sasa jeshi la Polisi bado halijauambia umma wa watanzania ni kwanini Msemaji wake ndugu Davido Misime alisema kua Mbowe alikabiliwa na kesi ya Kupanga njama ya kuua viongozi wa juu wa serikali na hii tuhuma kwanini waliiondoa kwenye hati ya mashtaka na ikabaki ya kulipua vituo vya mafuta na Uhujumu uchumi? Kwanini DPP hakuleta Shtaka hili? Polisi walidanganya kwa maslahi ya nani? Waliogopa kuumbuka kwa kukosa ushahidi?

Shaka kua mashtaka dhidi ya Mbowe ni ya uongo na kubambikiza na yanafanana na hili waliloliondoa, waliogopa kukosa ushahidi maana wangesema ni kiongozi yupi wa juu wa serikali mpaka Mbowe apange njama za kumuua. Kama mashtaka haya ni ya kubambikiza basi hii dhambi itamuadhibu mtu muda ukifika.

Hii ilikua ni aibu sana kutaja kitu ambacho hakipo ili kumchafua taswira yake ya kisiasa kwa maslahi ya kikundi kidogo cha watu wachache.Na kamwe hili halitakubalika na mwisho wake ni mgumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…