Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Leo wanasema heri Magufuli
Wanacdm hawana jema
Tukisema Samia anafanya mabaya ambayo hata Magufuli, pamoja na udikteta wake na ukatili wake wote hakuwahi kufanya, wala haina maana ya kusema heri Magufuli. Magufuli ana mabaya mengi mno, wala hakuna uheri wowote.

Na ni kweli, Samia alifanya mengi tu mazuri mwanzoni, na kwa kuwa sisi ni Waungwana, tulimpongeza, tukamshauri aendelee. Tusiangefanya hivyo, pia tungelaumiwa kwamba kazi yetu kupinga kila kitu, hamna hata jema moja?

Lakibi ni Samia aliyeahidi kukutana na wapinzani, na ni yeye aliyeingia mitini.

Baadae anaibuka na kujitetea eti "ratiba ilibana" mfyuuuu!!
Alipoonya kwamba kuna chokochoko zimeanza, wananchi wawapuuze, alikuwa anamwongelea nani? Acheni upuuzi!
 
Hii movie kuhusu viongozi wa CHADEMA imeandaliwa kwa kiwango cha chini mno na inaabua maswali mengi kuliko majibu kuzidi hata ile ya kutekwa kwa MO.

Na kwakuwa jambo hili linaonekana kugusa hisia za watu wengi na kuvuka mipaka ya nchi huku shinikizo likiongezeka, sitashangaa wakati wiwote wakatafutwa watu wa kubebeshwa lawama na hao wanaweza kuwa ni Sirro na pengine hata Boss wa TISS

Inawezekana Mama asiwe na wazo la kubebesha mtu lawama kwa makosa yake, ila wanasiasa wenzake na ambao ni wakongwe ndani ya chama, wanaweza kumshauri afanye uamuzi wa kuwato watu mbuzi wa kafara ili kulinda image yake.

Tuhuma hizi ni nzito, ngumu kuzithibitisha na inaonekana walizi-underestimate huku dunia ikifuatilia, hivyo ni lazima wajisafishe na katika kujisafusha huko, Sirro ndio anaeweza kuwa wa kwanza kubebeshwa zigo la lawama kwa kuondolewa katika nafasi yake huku Boss wa TISS nae akikalia kuti kavu.

Tusubiri.
Hii issue stearing ni mkwe wa macho kumchuzi,yani siro n tiss wanafanya kazi kwa maelekezo ya mvuvi mcherengwa...mama yupo hapo hajui nini maana ya kua rais
 
Hii movie kuhusu viongozi wa CHADEMA imeandaliwa kwa kiwango cha chini mno na inaabua maswali mengi kuliko majibu kuzidi hata ile ya kutekwa kwa MO.

Na kwakuwa jambo hili linaonekana kugusa hisia za watu wengi na kuvuka mipaka ya nchi huku shinikizo likiongezeka, sitashangaa wakati wiwote wakatafutwa watu wa kubebeshwa lawama na hao wanaweza kuwa ni Sirro na pengine hata Boss wa TISS

Inawezekana Mama asiwe na wazo la kubebesha mtu lawama kwa makosa yake, ila wanasiasa wenzake na ambao ni wakongwe ndani ya chama, wanaweza kumshauri afanye uamuzi wa kuwato watu mbuzi wa kafara ili kulinda image yake.

Tuhuma hizi ni nzito, ngumu kuzithibitisha na inaonekana walizi-underestimate huku dunia ikifuatilia, hivyo ni lazima wajisafishe na katika kujisafusha huko, Sirro ndio anaeweza kuwa wa kwanza kubebeshwa zigo la lawama kwa kuondolewa katika nafasi yake huku Boss wa TISS nae akikalia kuti kavu.

Tusubiri.
Polisi watapeleka ushahidi mahakama itaamua
 
Hivi ikitokea polisi wakashindwa katika ushahid wao,nani anapaswa kuwajibishwa.

Maana wanakuwa kama hawana kazi za msingi hivyo wanajitafutia tu kazi za kufanya.

Kuwa sasa tutengeneze kesi ya aina fulani,tuhangaike nayo kishatuachane nayo.

Nashauri,polisi inaposhindwa kuthibitisha basi wale maafisa inchaji watoswe tu,maana weredi wao utakuwa ni duni.
 
Apewe muda ili ajipange kuua watu?

Rais makini haitaji kupewa muda

Ana uwezo kutoa order kila kitu kinafanyika hàta ndani ya mwezi mmoja

Muda wa nini ngoja sasa uone watakavyompiga chini.

Nakwambia akifika 2025 ni bahati sana.
Nyie dawa yenu ni kutulizwa hivi hivi afu mtaishia kulia Lia kwenye keyboard.
 
Hawa jamaa kwa ujinga wao, wamefanya wananchi waanze kuamini upya kuwa Chuma aliuawa, Sasa watu mitaani wanataka majibu ni nani alihusika na kula njama hizo, Je wastaafu wanaotajwa walishirikiana na Mbowe kutekeleza hizo njama?

Wamefungua Pandora box wasiloweza kulifunga
Linafungika kwani gaidi kapatikana. Asubili mvua ya miaka 30akitoka viboko vunamhusu pia
 
Yaaani kama Sirro na huyu diwani na mwanasheria mkuu wa serikali ndio vichwa vinavyotegemewa na rais katika usalama wake basi taifa la Tanzania liko hatarini kama mbuzi wa kufugwa aliyetupwa mbuga ya wanyama pori wala nyama.
Kipindi cha mwendazake walijaribu kumbambikia Mbowe kesi ya madawa kupitia makonda lakini walivyochekecha labda mwendazake alishtuka kuwa watamshabishia yeye amiri jeshi madhara kuliko faida.
Sasa amiri jeshi aliyepo hajashtuka kwa hili famba la polisi.
Madhara yake kwa taifa ni makubwa kuliko hata janga la korona.
Umeambiwa pasipo kificho kuwa aliwekewa mtego na kutokana na uzezeta wake amenasa
 
Mpaka sasa jeshi la Polisi bado halijauambia umma wa watanzania ni kwanini Msemaji wake ndugu Davido Misime alisema kua Mbowe alikabiliwa na kesi ya Kupanga njama ya kuua viongozi wa juu wa serikali na hii tuhuma kwanini waliiondoa kwenye hati ya mashtaka na ikabaki ya kulipua vituo vya mafuta na Uhujumu uchumi? Kwanini DPP hakuleta Shtaka hili? Polisi walidanganya kwa maslahi ya nani? Waliogopa kuumbuka kwa kukosa ushahidi?

Shaka kua mashtaka dhidi ya Mbowe ni ya uongo na kubambikiza na yanafanana na hili waliloliondoa, waliogopa kukosa ushahidi maana wangesema ni kiongozi yupi wa juu wa serikali mpaka Mbowe apange njama za kumuua. Kama mashtaka haya ni ya kubambikiza basi hii dhambi itamuadhibu mtu muda ukifika.

Hii ilikua ni aibu sana kutaja kitu ambacho hakipo ili kumchafua taswira yake ya kisiasa kwa maslahi ya kikundi kidogo cha watu wachache.Na kamwe hili halitakubalika na mwisho wake ni mgumu.
 
Back
Top Bottom