Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Hii sio bahati mbaya kuona anatuhumiwa na ugaidi. Ni chaguoa maalum la jeshi la polisi au wanasiasa kuhakikisha anakosa dhamana.

Uwepo wa upenyo wa polisi kueka watu ndani bila ya mahakama, ndio tatizo sugu. Sheria hii ilitumika kuwaweka ndani masheikh wa UAMSHO, ilikuwa pia chaguo maalum kwa polisi kukwepa mahakama.

Vita ya wananchi sio tuu watu kutolewa, bali iwe ni vita ya mabadiliko ya kuondoa sheria kandamizi za namna hii.
 
Hakuna kiongozi yeyote makini anaetaka amani na utulivu akawavumilia chadema na huu ndo ukweli Chadema mnafanya siasa za kizamani sana mnafanya siasa zilizokuwa zinafanyika enzi za kupigania uhuru

JPM ndo aliwaweza vzr Gwanda zilikuwa night dress mnazivaa usk wkt wa kulala
Uko sahihi, wako katika harakati za kupigania uhuru. Kama wewe unaiona uko huru, basi wewe ni mtawala. Kama hakuna katiba inayo elekeza mipaka na majukumu ya mtawala na mtawaliwa, hapo mtawaliwa hayuko huru.
 
nafikiri hilo ni suala la mahakama. police ni wawezashaji tu. mahaka ndio wahamuzi
mkuu Detective J
Kwa professional uliyonayo ya uspy unasemaje kuhusu Mbowe kua na tuhuma za UGAIDI

Maana tunajua mziki wa magaidi ulivyo unaweza ukamfunga jela kiongozi wao halafu akawa anatoa oda Toka jela vijana wa kazi washambulie kujitoa mhanga maeneo muhimu!

Refer Alishabibi na alikaida!
😜😜
 
mi sidhani kama katiba mpya ni dawaya kuifanya nchi ikaishi kama iko peponi katiba mpya ni tamaatu ya madaraka kwa upande wampili yaani wapinzani ambao wanaamini kila uchaguzi wanaibiwa kura wanachowinda hapo ni tume huru ya uchaguzi tu
Katiba ya nchi inatambuliwa kuwa ni sheria kuu au ya msingi inayoweka mihimili mikuu mitatu ambayo ni Dola, Bunge na Mahakama. Inafafanua majukumu ya kila mhimili na kutoa mgawanyo wa madaraka miongoni mwa mihimili hiyo. Tovuti Kuu ya Serikali: Katiba www.tanzania.go.tz/home/pages/8

Katiba ni sheria au kanuni zinazoainisha jinsi ambavyo nchi, chama, au shirika vitakavyoendesha shuguli zao.. Kwa upande wa nchi, katiba ni sheria mama inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali.Katiba za nchi pia huainisha haki za msingi za Katiba - Wikipedia, kamusi elezo huru .

Katika nchi yoyote msingi wa uendeshaji wa nchi unategemea Katiba. Katiba ni sheria kuu au sheria mama katika nchi yoyote. Sheria nyingine zote zinategemea au zinatungwa kwa mujibu wa katiba, wakati mwingine katiba hutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kijamii kati ya watawala na wananchi (watawaliwa).-Nini Maana ya Katiba ya Nchi na umuhimu wake? | Dhana ya "kujenga uchumi"
 
Siasa usipokuwa makini maneno yako mwenyewe yanaweza kukuzika mwenyewe.Mngeacha tu mambo ya serikali yajiendeshe yenyewe maana na hata kuwekana wanawekana wenyewe.Utachagua lakini walioikalia serikali watamweka wanaemtaka yeye.Sasa wewe digdig unaacha kukazana na kuitawala familia yako kiuchumi ilmradi nawe uwepo wako home uonekane...umekazana mama samia mama samia.Mnajiumiza bure tu.
Bila katiba ya kueleweka, juhudi za mwananchi ni bure, hutapata maendeleo yoyote. Kwa nini mali za watu zilitaufishwa? Kwa nini leo serikali inakunyang'anya pesa yako kupitia agizo la tozo za miamala? Wanajua huna pa kulalamika. Mahakama wameishika, ukinyosha kidole kuhoji, unanyamazishwa, utapotezwa. Ukihurumiwa utapelekwa huko mahakamani na nini kiamuliwe kitapangwa na dola.
 
Uko sahihi, wako katika harakati za kupigania uhuru. Kama wewe unaiona uko huru, basi wewe ni mtawala. Kama hakuna katiba inayo elekeza mipaka na majukumu ya mtawala na mtawaliwa, hapo mtawaliwa hayuko huru.
Uhuru tunaotakiwa kupigania ni wa uchumi .
 
Bila katiba ya kueleweka, juhudi za mwananchi ni bure, hutapata maendeleo yoyote. Kwa nini mali za watu zilitaufishwa? Kwa nini leo serikali inakunyang'anya pesa yako kupitia agizo la tozo za miamala? Wanajua huna pa kulalamika. Mahakama wameishika, ukinyosha kidole kuhoji, unanyamazishwa, utapotezwa. Ukihurumiwa utapelekwa huko mahakamani na nini kiamuliwe kitapangwa na dola.
Tuambie Katiba Mpya itazuiaje tozo
 
Hii movie kuhusu viongozi wa CHADEMA imeandaliwa kwa kiwango cha chini mno na inaabua maswali mengi kuliko majibu kuzidi hata ile ya kutekwa kwa MO.

Na kwakuwa jambo hili linaonekana kugusa hisia za watu wengi na kuvuka mipaka ya nchi huku shinikizo likiongezeka, sitashangaa wakati wiwote wakatafutwa watu wa kubebeshwa lawama na hao wanaweza kuwa ni Sirro na pengine hata Boss wa TISS

Inawezekana Mama asiwe na wazo la kubebesha mtu lawama kwa makosa yake, ila wanasiasa wenzake na ambao ni wakongwe ndani ya chama, wanaweza kumshauri afanye uamuzi wa kuwato watu mbuzi wa kafara ili kulinda image yake.

Tuhuma hizi ni nzito, ngumu kuzithibitisha na inaonekana walizi-underestimate huku dunia ikifuatilia, hivyo ni lazima wajisafishe na katika kujisafusha huko, Sirro ndio anaeweza kuwa wa kwanza kubebeshwa zigo la lawama kwa kuondolewa katika nafasi yake huku Boss wa TISS nae akikalia kuti kavu.

Tusubiri.
Potelea mbali.
 
Unajuaje kama polisi ni waongo, kwani ww uko ktk intelijensia yao. Usiropoke tu, kama wametuhumu kwa ugaidi watampeleka OPEN COURT na ushahidi wao na kila kitu kitawekwa wazi. Be informed please...
Hivi unafikiri mimi ni mpumbavu kama wewe uliyeweka akili zako matakoni!

Mshenzi usiye na haya!
 
Hili li Mb(o)w(e)a bora likafie jela huko... lina mambo mengi ya kipuuzi sana... hv mzazi wako anakuomba na kukusihi namna ile we unambeza na unaishi kwake unadhani atakuacha we km nani?

bora likafie jela hili lip*mbav*
We sho*g*a bora ukaolewe huko

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo kipofu huwa hana FIKRA?!!!!

Namkumbuka mwalimu wangu wa HESABU...alikuwa ni MLEMAVU wa macho(KIPOFU)!

#KaziIendelee
#VivaCCM
Wewe ni mgumu wa kuelewa tu!
Nimekwambia ,, wewe ni kipofu usiye na fikra:- kwa maana vipofu huwa na fikra kama binadamu wengine ,, lakini KIPOFU WEWE HAUNA FIKRA.

Na sababu itakuwa ni ushamba au ubinafsi.
Ushamba - kwamba bado haujajua dunia ilivyo na inakoelekea.
Ubinafsi - ni kwamba ukishiba wewe basi hautaki na wengine washibe.


Nimeona nikufafanulie usije ukasema nakutukana.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Bila katiba ya kueleweka, juhudi za mwananchi ni bure, hutapata maendeleo yoyote. Kwa nini mali za watu zilitaufishwa? Kwa nini leo serikali inakunyang'anya pesa yako kupitia agizo la tozo za miamala? Wanajua huna pa kulalamika. Mahakama wameishika, ukinyosha kidole kuhoji, unanyamazishwa, utapotezwa. Ukihurumiwa utapelekwa huko mahakamani na nini kiamuliwe kitapangwa na dola.
Wenye low IQ kila kitu tutatupia katiba

Hatujui hata katiba ya sasa ikoje lakini tushabeba agenda za watu na kukimbia nazo

Wenzetu wanalipwa kuleta drama na Sisi ndio mitaji yao
 
Nisahihi kabisa atakuwa gaidi na wanashirikiana na makamu wake kuhakikisha nchi haitawaliki HILI ndiyo lengo kuu la magaidi wote Duniani.

Wamuongeze na kosa la kuhamasisha maambukizi ya corona kwa kukusanya wananchi wa Mwanza kinyume na maelekezo ya serikali na kufifisha jitihada za kupambana na corona kama zilivyotolewa na shirika la afya Duniani.
Mchimba shimo huingia mwenyewe ngoja amalize wapinzani aje kwenu si ulimsikia Antony Diallo

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Sintofahamu ni kubwa sana kwa anae jua awese tusaidia nani ni mkweli

Jeshi la polisi lina nyezo na weredi wakuweza kujua nini kinaendelea juu ya mwenyekiti

Lakini wanachama wachadema pia wanaweza kujua namna ya kiongozi wao jinsi alivyo

Tusaidiwe hapa sisi wananchi wa kawaida tuweze nani yupo sahihi

Nina imanin na jeshi la polisi lakini nina imani na mwenyekiti.
 
Baada ya upekuzi wa Polisi kukamilika nyumbani Kwa M.Kiti Mbowe, tumepokea taarifa za kushtua na kushangaza kuwa Polisi wamemwambia kuwa ataunganishwa kwenye kesi ya Ugaidi na watuhumiwa walioko gereza mojawapo DSM. Tutaendelea kutoa taarifa za kina hapo baadaye.

View attachment 1862953

====

UPDATES;

=====

TAARIFA KWA UMMA

JESHI LA POLISI LAMTUHUMU MWENYEKITI WA CHAMA
MHE.FREEMAN MBOWE NA "MAKOSA YA UGAIDI"

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Freeman Mbowe alifikishwa Dar es Salaam jana majira ya saa tatu usiku chini ya ulinzi wa Polisi , walimpeleka nyumbani kwake Mikocheni Kwa ajili ya kumfanyia upekuzi ambao ulichukua takribani saa mbili na nusu.

Baada ya upekuzi huo Polisi waliondoka na Kompyuta mpakato (Laptop) na Vishikwambi (tablets) za watoto wake, Kompyuta mpakato moja ya kwake na modem ya Internet Kwa ajili ya uchunguzi wao.

Leo majira ya saa Saba mchana Polisi walimfikisha Mhe. Freeman Mbowe Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano na kuchukua maelezo yake.

Polisi walitaka maelezo kutoka Kwa Mhe. Freeman Mbowe kuhusiana na kosa waliloliita 'KULA NJAMA ZA KUTENDA KOSA LA UGAIDI'

Baada ya maelezo hayo ya Polisi Mhe. Freeman Mbowe alitumia haki yake ya kisheria na aliamua kutokutoa maelezo yoyote Polisi kwa mujibu wa Sheria. Baada ya maelezo hayo Polisi wamemrejesha Mhe. Freeman Mbowe katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay ,Jijini Dar es Salaam.

Aidha , viongozi wengine waliokuwa wanashikiliwa Mkoani Mwanza wameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi na baadhi yao walifanyiwa upekuzi nyumbani kwao na vyumba vya hotel ambako walikuwa wameshukia .

Waraka wa Mbowe kwa Watanzania
Mwenyekiti Taifa Mhe. Freeman Mbowe ametuma waraka kwa Watanzania kama ifuatavyo;
"Hatimaye madai ya Katiba Mpya yamenisababishia kesi ya ugaidi, nipo tayari kwa mashtaka ya kuchongwa siogopi. Ninaamini Dunia itaujua ukweli wa kile kinachoendelea Tanzania na kile tunachokipitia Watanzania. Lakini pia itajua ukweli juu ya makosa haya ya kuchongwa.

Natoa wito kwa watanzania kuendeleza mapambano, haki hutafutwa” Mhe.
Freeman Mbowe.”

Imetolewa leo Alhamisi tarehe 22 Julai, 2021.

John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.

=====

UPDATE:

View attachment 1863559
View attachment 1863560
Nani apange njama ya kuua mijitu yenyewe yalishaharibu mahusiano yao na Mungu. Acha wafe kwa utaratibu wa Mungu,hakuna mkono wa binadamu hapo kama walivyokuwa wanataka Sept.7!
 
Ulisikia kuhusu kesi 147 kufutwa? Kesi ambazo polisiccm walijidhirisha kwamba kuna ushahidi wa kutosha kumbe ni wa kubambikia!? Unamkumbuka Erick Kabendera?
 
Yaani mbowe pamoja na misala yote alio nayo unategemea lap top yake iwe na ushahidi mpaka muda huo wanapoenda kwake? polisi wajitahid kuwa wanatengeza movie nzuri basi za kuvutia mbona wanafeli kupanga matukio mpaka watoto wadogo wanajua kwamba huu ni uongo kbsa
 
Kuna charges zozote za ugaidi zimefanywa au ndio midemko Tu kama kawa?
 
Back
Top Bottom