Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii si ndio Golden chance ya kumuondowa Mbowe kupitia danduku la kura? Au mimi ndio sielewi?
Kama Mbowe yuko powerful hivi maana yake huyo ndio mtu sahihi, wakutane kwenye box namba zitaongea, hiyo ndio Demokrasia sasa, ccm mwenyekiti inatoka fomu moja tu na mapovu hayawatoki, sasa Chadema mmepewa fursa mumchaguwe mnayetaka mnaweweseka, binafsi siwaelewi.
Siwezi kuyasema mengi kwa heshima ya hiki chama kwani nimesitisha tu kwa muda uanachama wangu. Ila kuna upuuzi mwingi sana.
 
Wanaoimiliki CDM wanamuamini Mbowe zaidi na si vinginevyo.

Elites walio behind the scene ambao ndio wamiliki wa CDM Kwa bahati mbaya malengo yao sio kama mnavyoiona CDM msioijua.

Nilishatoa angalizo, Lissu kama Yuko serious kweli akaanzishe chama ahame na wafuasi wake wakafanye siasa huko.
CDM Ina malengo mengine kabisa nje ya hizi siasa za kuchukua dola.
Hata Leo hii Lissu akiwa mwenyekiti, bado malengo ya CDM yapo palepale, either atakuwa compromised au atafiksiwa kivingine.
Bahati mbaya sana Tanzania ni nchi ya sintofahamu na behind the scenes nyingi sana, wananchi Kwa zaidi ya 70% wapo manipulated.

Siku wengi wenu mkipata akili ndio mtanielewa.
Hoja hii inahitaji akili kubwa kuielewa
 
Siwezi kunywa sumu kwa vile nina maisha bora sana nje siasa. Sijawahi kunufaika hata kwa senti moja na siasa bali nimetoa pesa zangu kuchangia Chadema. Hivyo sana sana nimekuwa relieved. Ninachosikitika tu ni kuwa katika kilichokuwa kinaendelea kwa wiki kadhaa ndani ya Chadema CCM ndiyo imeibuka kidedea. Imekwisha .
Hakuna kilichoharibika, Kapigeni kura.
Hamtaki kupiga kura mnataka nini sasa?

Tatizo mnajiunga vyama kwa kufuata mtu
 
CHADEMA haitakufa

Tutawapa Wanachama na Viongozi wengine wapya wasio vibaraka wa mabeberu.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi

Kidumu Chama Tawala
kibaraka wenu ni mbowe atawarahisishia ushindi wa mafuriko na kimbunga ila mpeni wabunge na madiwani wawili watatu mpotezee mambo kuwa mmeshinda kihalali
 
Ndio watu wa lissu hao. Useless
Usinilishe maneno mkuu, mimi Lissu wakwangu Mbowe pia wa kwangu, ila msimamo wangu kwa sasa ,wajumbe Mleteni lissu, Mbowe kama chama hatakiwi kuachwa bado anahitajika ila kwa sasa wajumbe Mleten lissu period Mungu bariki mikono ya wajumbe, na ni matumaini yangu Mbowe pia atampigia lissu kura
 
Sasa wakulungwa kuna haja gani ya Lissu kusubiri uchaguzi ufanyike wakati uhakika wa kushinda ni mdogo, au asubiri matokeo ndio chama kipasukepasuke mbowe aanze upya kukisuka? ila itachukua miaka mingi chama hicho kuja kuwa na nguvu tena kama kitakuwepo mpaka wakati huo
Yani Lisu aipasuwe Chadema kwa sababu ya kuropoka? Atakapokimbilia Belgium ndio wote mtakuja kujijuwa hamna akili.
 
Wakati wowote kuanzia sasa Mhe Freeman Mbowe kutoa tamko rasmi la ama atagombea Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa ama laa.

Mtakumbuka Mhe Freeman Mbowe ameitumikia nafasi hii kwa zaidi ya miongo miwili sawa na miaka 21 mfululizo.

Endapo atatangaza kugombea tena atakuwa ni mgombea wa nne nyuma ya Tundu Lissu na Odero Odero,

Je, kama Taifa tunatarajia nini kutoka Upinzani kuelekea 2025?

Usiondoke hapa Jf kwa habari zaidi

=======================================

Siku ya leo Disemba 12, 2024 Freeman Mbowe ametangaza rasmi kugombea kwa mara nyingine nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Mbowe amsema kuwa kutokana na Uchaguzi mkuu ambao unakuja si vyema kubadilisha "makamanda" na kwamba bado yupo sana kuongoza chama hicho na mara baada ya mkutano anaenda kuchaukua fomu kwenye makao makuu ya chama hicho, Mikocheni.

"Kwa kuzingatia yote haya na mengine mengi ambayo sitaki kuwachosha. Nilisema mara nyingi kuwa nilitamani kuondoka lakini siwezi kuondoka katikati ya minyukano iliyopo. Kwa hiyo CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea"

View attachment 3181677



View: https://www.youtube.com/live/8WGa7Xv3hKo?si=JjooipgRmN035_2F

Kwa heri Chadema.Kweli Chama hicho ni Saccos ya watu.
 
Back
Top Bottom