Pre GE2025 Freeman Mbowe kuona ni kuamini, achana na siasa za mkia wa mbuzi, jeuri na kiburi sio mtaji kuelekea uchaguzi 2024/2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Uchawa hufanywa na punguani. Maandamano ya amani hufanywa na watu wanaojitambua ikiwa ni njia shirikishi zaidi ya kufikisha maoni yao kwa watawala. Maandamano hupima ni watu wengi kiasi gani wanaguswa na suala husika. Ndiyo maana kwa nchi zilizostaarabika, kama maandamano ni ya amani, watawala huweza kujitokeza mbele ya waandamanaji na kutoa majibu ya yale yaliyowafanya waandamane.
Maandamano yapi ya amani? Nendeni mkaandamane Siha.
 
Na;
Hamis Abeid Baruani
UDASA, UDSM.

Kwa masikitiko makubwa leo Mbowe ameushangaza umma kwa kuongea mambo mawili ambayo hadi sasa yamepingwa kila kona ya nchi.

1. Katangaza kususia maridhiano
2. Kaitisha anayoyaita maandamano ya amani.

a) Mhe. Mbowe kabla ya kususia MARIDHIANO unakumbuka lakini majuzi tu 31.12.2023 pale Hai wakati unaongoza Harambee ya kumalizia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika wa NSHARA MACHAME, Rais Dkt. Samia alichangia Tsh Milioni 150, haya yakiwa ni matunda ya MARIDHIANO ya kisiasa hapa nchini.

b) Mnakumbuka CDM mlikuwa na ziara pamoja na mikutano mikoa mbalimbali na mkafanya kwa amani hakuna mtu alienyooshewa kidole hata mmoja inamaana mmesahau kama hayo ni matunda ya MARIDHIANO

c) Maridhiano haya unayotaka kuyakataa hukumbuki kuwa ndio yamefanya viongozi wa CDM waliokuwa nje ya nchi kurejea nchini kufanya siasa kwa amani bila wasiwasi

d) Hujiulizi hata tukio la leo limefanyika vizuri kwa amani na umepewa ushirikiano wa namna zote kwenye vyombo vya habari kwasababu ya matunda ya MARIDHIANO yaliyoletwa na Rais Dkt. Samia

e) Hata umuhimu wa RUZUKU ambao pengine umepelekea kuhamisha Ofisi toka Kinondoni kwenda Mikocheni nao huoni kama ni matunda ya MARIDHIANO

Tujifunze kuwa waungwana tunapofanyiwa uungwana.

Wakati unafikiria kuandamanisha watu kumbuka wananchi wa sasa sio wa miaka ile, wananchi wanaona mambo makubwa yanayofanywa na Serikali yao, wanaona jitihada za Rais Samia kuwapigania. Ngoja niwakumbushe kidogo:-

1. Januari za miaka ya nyuma Wazazi walikuwa wanateseka kwa michango ya ujenzi wa madarasa na kununua madawati ila sasahivi hakuna mzazi hata mmoja nchini anaesumbuliwa na michango hii, Rais Samia kajenga madarasa mengi nchi nzima lakini pia Serikali kila mwezi inatoa takribani Bilioni 33.3 kugharamia elimu kwa wanafunzi wa ngazi ya awali, msingi na sekondari.

2. Rais Samia amesambaza Vifaa vya Afya Majimbo yote nchini kama ifuatavyo kwa ujumla
a) Vitanda vya wagonjwa 3080
b) Vitanda vya kujifungulia 1000
c) Magodoro 5500
d) Mashuka 36,808
e) Meza za Vitanda 306
f) Pia kasambaza magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) kila kona

Hii inaonesha namna gani ana huruma na wananchi na anajali afya zetu.

3. Takribani asilimia 95% ya Madai ya Watumishi yamefanyiwa kazi ndani ya muda mfupi. (Ulipaji madeni, Ongezeko la Posho, Mikataba ya hali bora, Ajira mpya, Mazingira bora ya Kazi).

4. Wakati wananchi wanajiuliza michango yao mliochangisha CDM kuipeleka Hanang haijulikani imeenda wapi na hakuna jibu kuwa mlikusanya shilingi ngapi,

Rais Samia ametenga ekari 100 kwaajili ya makazi mapya ya wahanga wa Hanang, lakini Serikali itawajengea nyumba 101 ambazo kila moja itakuwa na vyumba vitatu na eneo litawekewa huduma zote za kijamii.

5. Kwa muda mfupi mno wa Rais Samia kuwa madarakani sasahivi kati ya Vijiji 10, Vijiji 9 vina umeme, hii ni hatua kubwa mno.

Hawa wana vijiji huwezi ukawaambia habari za kuandamana wakakuelewa.

6. Ndani ya muda mfupi tu Waalimu takribani 227,263 wamepandishwa madaraja na wanaendelea kuchapa kazi, hawa wataandamana kushukuru na kumpongeza Rais Dkt. Samia.

7. Kwenye kuongeza mapato makubwa hivi karibuni Serikali inatatajia kuanza kuchimba MAKAA YA MAWE katika mradi wa MCHUCHUMA, Tani karibia 315,000 zitachimbwa.

8. Wakulima wanafurahia Ruzuku kwenye Pembejeo za Kilimo ambazo zimefanya hali ya kilimo kuwa vizuri.

9. Ndani ya muda mfupi fedha za kigeni zimeongezeka baada ya kuongeza biashara nje ya nchi.

Mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi yameongezeka kwa asilimia 17.8
  • Novemba 2022 tuliuza Trilioni 29.8
  • Novemba 2023 tuliuza Trilioni 35.1

Mfano; Desemba 2022 hadi Desemba 2023 tumeuza NYAMA Tani 20,500 nje ya nchi, takribani mara mbili ya mauzo ya mwaka uliopita.

Hii inaonyesha ni namna gani Serikali inapambana kuleta maendeleo.

10. Miradi ya Maji nchi nzima inaendelea ili lengo la kumtua Mama Ndoo Kichwani litimie, mfano kwa Wilaya ya Ubungo kuna Miradi mikubwa miwili a) Tegeta A na b) Mshikamano
Ambayo itamaliza kabisa tatizo la maji.

Hawa wananchi hawahitaji maandamano bali wanahitaji kutoa pongezi kwa kazi kubwa inayofanywa.

Ni mengi yaliyofanyika na yote yana lengo la kumfaidisha Mwananchi ili aendelee kuwa na imani na Serikali yake.

Tusikubali kuyumbishwa na SIASA ZA MKIA WA MBUZI.

Kila Chama kijipange tukutane kwenye DEBE muda ukifika.

Ahsanteni.
Umeandika kipuuz. So kama samia alichangia maana yake sasa alimnunua Mbowe? Unatufanya wote CCM tuonekane vilaza. Kila mtu atimize wajibu. Nyie ndo mnamkuza kwa kumwogopa sana Mbowe.
 
Mbowe kakunja pesa. Anataka watu waandamane. Atangulie yeye na watoto wake.
 
Mbowe kapoteza sera. Siasa zake za 1996 bado anataka azofanye leo.
 
Mkuu ulichokiandika ni maoni yako na siyo uhalisia.

"Timiza Wajibu Dai Haki Yako" CDM kupitia Kiongozi wake Mkuu Mh Mbowe wamefanya hivyo. Kama wametimiza wajibu wao kwenye dawati la maridhiano na Wenzao wa upande wa pili wakawapuuza, kwanini wasidai Haki hiyo??

Pesa alizotoa kule Hai kwajili ya Ujenzi wa Kanisa isitumike kama njia ya kuwaziba midomo watu kudai Haki zao. Lile Kanisa siyo mali ya CDM Bali ni la Wakristo wote bila kujali itikadi zao za Vyama vya Siasa.

Suala la shule kuwa elimu bure ni kiini macho. Bado michango inaendeshwa kama kawaida ikiwemo michango ya Taaluma na Ujenzi. Kama mwanafunzi hajalipa anarudishwa nyumbani. Fuatilia utagundua namaanisha nini. Suala la afya nafikiri umeshasikia kama siyo kushuhudia Wamama wajawazito wakipoteza maisha kwa kukosa huduma stahiki kisa michango ya afya.

Kwa kifupi ni kwamba " Mtu anakupora Shamba lako kisha wakati wa mavuno anakupatia 1% ya mavuno yote nawe eti umpongeze na kumshukuru kwa uungwana wake" ndivyo wanavyofanyiwa Watz na Watawala.
 
Mimi kinachonishangaza ni wanasiasa kutumia hali ya wananchi wake kutokwenda shule (illiteracy) km mtaji wao. Tangu Uhuru wananchi wsmefanywa mandondocha, hakuna kuhoji wala kutoa maoni kwa kibwagizo Cha neno chama Dola.

Wajinga wengine (ashskumu so matusi) utawaskia wanaita Tz eti nchi ya "mama". Seriously, mtu ulietumia kodi ya wananchi maskini hujui hata maana ya nchi na uongozi. Kwa vile wanaongoza familia zao na kujiita kichwa Cha nyumba na baba mwenye nyumba, basi ujinga huo huo wanahamishia kwenye Mali ya Watanzania ambako kila raia ana hisa.

Mbaya zaidi ni kuwatumia watoto wadogo kwenye huu mchezo mchafu (siasa) kwa kigezo Cha halaiki nk. Yani mtoto wa chekechea una mvalisha sare za chama eti unamjengea uzalendo. This is incureable nonsense. Kwenye mambo ya msingi ukitaka kuwatumia utaskia "hao ni watoto wadogo,".
 
WAPUMBAVU NILIWAAMBIA KUWA WANASHANGILIA KIFO CHA MAGUFULI
 
Hayo ndio matatizo yenu mnawatukana wananchi kwa kuwaita Illiterate huku hao ndio wapiga kura.
Hamna sera za maana za kushawishi wapiga kura bali matusi na kejeli.
Mngeweka bajeti kivuli na sera madhubuti za kuendeleza Nchi mngeeleweka.Mmegeuza siasa kama ni ushabiki wa kupinga kila kitu na kufurahia yanapotokea matatizo kwa Nchi.Majukwaani mmekuwa walalamikaji kwa lugha za matusi na kejeli.Sera zenu hazieleweki kwani mmekuwa wanaharakati zaidi kuliko wanasiasa.Hamna sera za kushawishi.Hata hapa JF wengi wenu hamna nguvu za hoja bali hoja za nguvu,matusi na kejeli.
 
Na;
Hamis Abeid Baruani
UDASA, UDSM.

Kwa masikitiko makubwa leo Mbowe ameushangaza umma kwa kuongea mambo mawili ambayo hadi sasa yamepingwa kila kona ya nchi.

1. Katangaza kususia maridhiano
2. Kaitisha anayoyaita maandamano ya amani.

a) Mhe. Mbowe kabla ya kususia MARIDHIANO unakumbuka lakini majuzi tu 31.12.2023 pale Hai wakati unaongoza Harambee ya kumalizia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika wa NSHARA MACHAME, Rais Dkt. Samia alichangia Tsh Milioni 150, haya yakiwa ni matunda ya MARIDHIANO ya kisiasa hapa nchini.

b) Mnakumbuka CDM mlikuwa na ziara pamoja na mikutano mikoa mbalimbali na mkafanya kwa amani hakuna mtu alienyooshewa kidole hata mmoja inamaana mmesahau kama hayo ni matunda ya MARIDHIANO

c) Maridhiano haya unayotaka kuyakataa hukumbuki kuwa ndio yamefanya viongozi wa CDM waliokuwa nje ya nchi kurejea nchini kufanya siasa kwa amani bila wasiwasi

d) Hujiulizi hata tukio la leo limefanyika vizuri kwa amani na umepewa ushirikiano wa namna zote kwenye vyombo vya habari kwasababu ya matunda ya MARIDHIANO yaliyoletwa na Rais Dkt. Samia

e) Hata umuhimu wa RUZUKU ambao pengine umepelekea kuhamisha Ofisi toka Kinondoni kwenda Mikocheni nao huoni kama ni matunda ya MARIDHIANO

Tujifunze kuwa waungwana tunapofanyiwa uungwana.

Wakati unafikiria kuandamanisha watu kumbuka wananchi wa sasa sio wa miaka ile, wananchi wanaona mambo makubwa yanayofanywa na Serikali yao, wanaona jitihada za Rais Samia kuwapigania. Ngoja niwakumbushe kidogo:-

1. Januari za miaka ya nyuma Wazazi walikuwa wanateseka kwa michango ya ujenzi wa madarasa na kununua madawati ila sasahivi hakuna mzazi hata mmoja nchini anaesumbuliwa na michango hii, Rais Samia kajenga madarasa mengi nchi nzima lakini pia Serikali kila mwezi inatoa takribani Bilioni 33.3 kugharamia elimu kwa wanafunzi wa ngazi ya awali, msingi na sekondari.

2. Rais Samia amesambaza Vifaa vya Afya Majimbo yote nchini kama ifuatavyo kwa ujumla
a) Vitanda vya wagonjwa 3080
b) Vitanda vya kujifungulia 1000
c) Magodoro 5500
d) Mashuka 36,808
e) Meza za Vitanda 306
f) Pia kasambaza magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) kila kona

Hii inaonesha namna gani ana huruma na wananchi na anajali afya zetu.

3. Takribani asilimia 95% ya Madai ya Watumishi yamefanyiwa kazi ndani ya muda mfupi. (Ulipaji madeni, Ongezeko la Posho, Mikataba ya hali bora, Ajira mpya, Mazingira bora ya Kazi).

4. Wakati wananchi wanajiuliza michango yao mliochangisha CDM kuipeleka Hanang haijulikani imeenda wapi na hakuna jibu kuwa mlikusanya shilingi ngapi,

Rais Samia ametenga ekari 100 kwaajili ya makazi mapya ya wahanga wa Hanang, lakini Serikali itawajengea nyumba 101 ambazo kila moja itakuwa na vyumba vitatu na eneo litawekewa huduma zote za kijamii.

5. Kwa muda mfupi mno wa Rais Samia kuwa madarakani sasahivi kati ya Vijiji 10, Vijiji 9 vina umeme, hii ni hatua kubwa mno.

Hawa wana vijiji huwezi ukawaambia habari za kuandamana wakakuelewa.

6. Ndani ya muda mfupi tu Waalimu takribani 227,263 wamepandishwa madaraja na wanaendelea kuchapa kazi, hawa wataandamana kushukuru na kumpongeza Rais Dkt. Samia.

7. Kwenye kuongeza mapato makubwa hivi karibuni Serikali inatatajia kuanza kuchimba MAKAA YA MAWE katika mradi wa MCHUCHUMA, Tani karibia 315,000 zitachimbwa.

8. Wakulima wanafurahia Ruzuku kwenye Pembejeo za Kilimo ambazo zimefanya hali ya kilimo kuwa vizuri.

9. Ndani ya muda mfupi fedha za kigeni zimeongezeka baada ya kuongeza biashara nje ya nchi.

Mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi yameongezeka kwa asilimia 17.8
  • Novemba 2022 tuliuza Trilioni 29.8
  • Novemba 2023 tuliuza Trilioni 35.1

Mfano; Desemba 2022 hadi Desemba 2023 tumeuza NYAMA Tani 20,500 nje ya nchi, takribani mara mbili ya mauzo ya mwaka uliopita.

Hii inaonyesha ni namna gani Serikali inapambana kuleta maendeleo.

10. Miradi ya Maji nchi nzima inaendelea ili lengo la kumtua Mama Ndoo Kichwani litimie, mfano kwa Wilaya ya Ubungo kuna Miradi mikubwa miwili a) Tegeta A na b) Mshikamano
Ambayo itamaliza kabisa tatizo la maji.

Hawa wananchi hawahitaji maandamano bali wanahitaji kutoa pongezi kwa kazi kubwa inayofanywa.

Ni mengi yaliyofanyika na yote yana lengo la kumfaidisha Mwananchi ili aendelee kuwa na imani na Serikali yake.

Tusikubali kuyumbishwa na SIASA ZA MKIA WA MBUZI.

Kila Chama kijipange tukutane kwenye DEBE muda ukifika.

Ahsanteni.
Huko UDASA wewe ni mfagia ofisi.
 
Sipendi maandamano na kashi kashi za kisiasa ila maridhiano ilikuwa njia muafaka ya kuleta maendeleo ktk nchi yetu.

Siasa hizi ambazo zinataka kuanza zinaweza zikaaribu kabisa twaswira ya nchi yetu hapa ilipofikia na ikafifisha hatua xa maendeleo tuliyopiga kwa kipindi hiki cha Mama samia. maandamano yataambana na kamata kamata na vipigo kwa wananchi na kiwango cha uhasama na chuki baina ya watu na serkali inazidi kupandishwa kila kona, Mitandaoni, mikutano ya hadhara na maongezi baina ya mtu na mtu.

Niseme kuwa Serikali ya CCM ilifanya vizuri sana kuhakikisha inapata maoni ya wadau ili kuweza kuleta uchaguzi ulio huru na haki lakini maoni hayo hayajazingatiwa vilivyo na watu bado wana machungu ya kile walichofanyiwa 2019 na 2020 hii inaweza ikasababisha kuibua rabsha rabsha ambazo si muafaka ktk kipindi hiki ambacho ndiyo kwanz tunachemea kujenga uchumi wetu kutokana na majanga mbali mbali yaliyo ikumba Dunia.

CDM ni chama cha siasa kinafanya taratibu za kisiasa mimi ninachogopa ni pale yatakapo tokea makundi ya kigaidi na kufanya vitendi vya gigaidi kwa visingizio vya kisiasa. Mungu ibariki Tanzania na watu wake
Ukitaka kuishi vizuri na Wahuni ishi kihuni. CCM wanafanya maigizo wakiona wenzao kama wajinga. Huwezi kuwa na maridhiano aambayo Hakuna hata 1 Kati ya madai yako linqtekelezwa. CDM ni wavumilivu Sana.
 
Mbowe kakaa kwenye uenyekiti zaidi ya miaka 20. Je, yeye ni mfalme wa CDM?
 
Hayo ndio matatizo yenu mnawatukana wananchi kwa kuwaita Illiterate huku hao ndio wapiga kura.
Hamna sera za maana za kushawishi wapiga kura bali matusi na kejeli.
Mngeweka bajeti kivuli na sera madhubuti za kuendeleza Nchi mngeeleweka.Mmegeuza siasa kama ni ushabiki wa kupinga kila kitu na kufurahia yanapotokea matatizo kwa Nchi.Majukwaani mmekuwa walalamikaji kwa lugha za matusi na kejeli.Sera zenu hazieleweki kwani mmekuwa wanaharakati zaidi kuliko wanasiasa.Hamna sera za kushawishi.Hata hapa JF wengi wenu hamna nguvu za hoja bali hoja za nguvu,matusi na kejeli.
Hivi mnufaika wa ujinga wa wapiga kura ni nani. Usimtaje tu maana unamjua.
 
Inasikitisha kusoma upuuzi kutoka kwa "msomi" wa UDASA. JIELEKEZE KWENYE HOJA ALIZOTOA MH. MBOWE.
 
Mbowe kakaa kwenye uenyekiti zaidi ya miaka 20. Je, yeye ni mfalme wa CDM?
Vyama vya ukombozi vyote kukiwa na mtu mwenye uwezo wa kuongoza huwa anaachwa madarakani mpaka ukombozi upatikane, acha kwanza mbowe awanyooshe kisha atamwachia Tundulisu
.
 
Back
Top Bottom