Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Tangu Mbowe aanze kwenda huko hakuna hata jambo moja lililowahi kufanyiwa kazi na serikali, sijui ugumu wa Samia kufanya hivyo unatoka wapi, na sijui uvumilivu wa Mbowe utaendelea mpaka lini, naona utani unazidi.

- Lissu bado hajarudi nchini, hii inawezekana bado hajahakikishiwa usalama wake.

- Mikutano ya vyama vya siasa bado haijaruhusiwa japo ni takwa la kisheria.

- Wale wahujumu uchumi 19 bado wanakumbatiwa na Spika kule bungeni kinyume cha sheria.
Kufikia uhuru na demokrasia kamili katika nchi yetu ni mapambano ya vita kamili. Lazima uwe na multiple specialized forces and tactics and strategies.
Lazima Chadema ijipange na ipigane in both frontiers.Lazima ivipige vita vyema kipropoganda, kiuchumi, kidipromasia, kisheria,kisiasa, kiroho nk. Mfano mie si askari wa mtandao ingawa nipo hapa. Uwanja wangu ni vita vya kiroho na huko naupiga mwingi. Waache askari wa diplomasia au wa kisheria Kama akina Kibatala waupige mwingi kwenye special tactical area zao.
Kazi ya muhimu zaidi ni kujenga jeshi lenye vitengo vyote na kuviimarisha kwa Kila aina ya silaha na mbinu.
Kuishinda CCM inabidi kupigana nayo ardhini, majini, angani, chini ya ardhi, anga la juu na zaidi.
 
Wakuu,

Muda huu M/Kiti wa CHADEMA na viongozi waandamizi 9 wa chama hicho wapo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Tutarajie jambo gani jipya? Ndo ukurasa mpya wa Siasa za Tanzania?

UPDATE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha majadiliano pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Mei, 2022.

Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waliohudhuria Kikao hicho ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Saidi Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Chama hicho.

View attachment 2232248View attachment 2232250
View attachment 2232257View attachment 2232258View attachment 2232259

View attachment 2232260
View attachment 2232570
Mfupi kuliko wote ndiye mkubwa kuliko wote
 
Mkuu badala yake wafanye nini? Waandamane? Wako wapi waandamanaji
Waingie msituni? Liko wapi jeshi la kuingia msituni?

Hakuna kwenda kwenye mazungumzo ya kitapeli, watu hawawezi kuandamana hiyo ni kweli, lakini wanaweza kuhamasishwa ususiaji wa chaguzi, kutoshirikiana na wanaccm kwenye mambo ya kijamii, njia hii ya utengano ni salama na isiyoacha maumivu na vifo kwa wafuasi wao. Hayo mazungumzo ya kitapeli sina imani nayo hata chembe.
 
Chadema imegawanyika kwenye hili, Wamarangu na Machame wako na con man Mbowe na wanaona ni sawa ili kumlinda corrupt Mbowe na chadema second class wa Mikoa mingine wana doubt hii move, ngoja tuone itakavyokuwa!
Kutofautiana Ni kawaida sio Kama CCM hakuna wa kumkosoa mwenyekiti
 
CDM

Tengeneza kuungwa mkono na jamii, ivuteni jamii iwe upande wenu, na ndio siasa haswaa

Hii ya kutengeneza moves kupata keki ya taifa mtaishia second runners always if not forever..Na always mtakuwa watu wa kubeg

Kuna makosa na dhambi mmeifanya kwa raia wa Tanzania

Leo nyie hamna mvuto kwa raia...samia yes atawavuta, atawapenda

Ila CCM haitawavuta na kuwapenda!

Mko na bidii kutafuta kupendwa na mkuu wa nchi ila sio kwa wananchi
 
Hakuna kwenda kwenye mazungumzo ya kitapeli, watu hawawezi kuandamana hiyo ni kweli, lakini wanaweza kuhamasishwa ususiaji wa chaguzi, kutoshirikiana na wanaccm kwenye mambo ya kijamii, njia hii ya utengano ni salama na isiyoacha maumivu na vifo kwa wafuasi wao. Hayo mazungumzo ya kitapeli sina imani nayo hata chembe.
Mkuu lakini hayo yameshafanyika. Chadema wamesusia chaguzi na bunge bila shaka unakumbuka. Lakini tazama pia impact ya kususia inavyokuwa haileti matokeo makubwa kwa sababu wako wapi wananchi wakususia drastically?

Baada ya kususia na kupaza sauti what next? Si inabidi mkae muweke hoja mezani? Kwa nini tusiamini pia hii meza wanayokaa ni impact ya kususia vikao vya kamati ya Zitto,bunge nk
 
Chadema mkae macho sana na hawa watu, wanazitaka sana hizi picha za pamoja kwaajili ya kuwarubuni wafadhili, wakati hali halisi uwandani haiko hivyo na matendo yao yamejaa uhuni huni tu. Kama wananchi tunataka baada ya vikao vyenu mnatoka na statement ya pamoja kwa wwatanzania na siyo hizo picha zenu. Pia statement inayotolewa ifanane na matendo yatakayofuata baada ya kikao. Kama vipi achaneni nao hao Ccm nanyi mrudi kwa wananchi kwani walishawaelewa longtime.
Na kama hamjagundua joto la siasa lipo juu sana sasa hivi tena bila hata mikutano ya hadhara, hivyo wanatumia mbinu ya kuwaita na kupiga picha ili kusafiria nyota ya Chadema na kushusha temper ya wananchi. Lakini wanasahau baada tu ya siku mbili tatu unakuta wameshachafua hali ya hewa. Wameshazoea vya kunyonga hao.
CDM anatafuta faraja!!!
 
Tangu Mbowe aanze kwenda huko hakuna hata jambo moja lililowahi kufanyiwa kazi na serikali, sijui ugumu wa Samia kufanya hivyo unatoka wapi, na sijui uvumilivu wa Mbowe utaendelea mpaka lini, naona utani unazidi.

- Lissu bado hajarudi nchini, hii inawezekana bado hajahakikishiwa usalama wake.

- Mikutano ya vyama vya siasa bado haijaruhusiwa japo ni takwa la kisheria.

- Wale wahujumu uchumi 19 bado wanakumbatiwa na Spika kule bungeni kinyume cha sheria.
Mkuu,
Huwezi kufuta legacy za dikteta meko kwa siku moja.

90% ya viongozi waliwekwa na meko.

Kuanzia Tulia akson
 
Chadema mkae macho sana na hawa watu, wanazitaka sana hizi picha za pamoja kwaajili ya kuwarubuni wafadhili, wakati hali halisi uwandani haiko hivyo na matendo yao yamejaa uhuni huni tu. Kama wananchi tunataka baada ya vikao vyenu mnatoka na statement ya pamoja kwa wwatanzania na siyo hizo picha zenu. Pia statement inayotolewa ifanane na matendo yatakayofuata baada ya kikao. Kama vipi achaneni nao hao Ccm nanyi mrudi kwa wananchi kwani walishawaelewa longtime.
Na kama hamjagundua joto la siasa lipo juu sana sasa hivi tena bila hata mikutano ya hadhara, hivyo wanatumia mbinu ya kuwaita na kupiga picha ili kusafiria nyota ya Chadema na kushusha temper ya wananchi. Lakini wanasahau baada tu ya siku mbili tatu unakuta wameshachafua hali ya hewa. Wameshazoea vya kunyonga hao.
Sahihi kabisa kama alivyofanya TL wakati ule🤣
 
denooJ kwani unataka mwisho wa siku afanyeje? Aache kukutana na Rais?

Maridhiano ni mchakato (process). Unaweza usiyaone matunda ya kazi hii njema mara moja na papo kwa papo...

Let's be patient..

Surely, I personally see bright future ahead..

It's very difficult. But, surely there's hope..
True
 
Wakuu,

Muda huu M/Kiti wa CHADEMA na viongozi waandamizi 9 wa chama hicho wapo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Tutarajie jambo gani jipya? Ndo ukurasa mpya wa Siasa za Tanzania?

UPDATE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha majadiliano pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Mei, 2022.

Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waliohudhuria Kikao hicho ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Saidi Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Chama hicho.

View attachment 2232248View attachment 2232250
View attachment 2232257View attachment 2232258View attachment 2232259

View attachment 2232260
View attachment 2232570
Binfsi nitakua wa mwisho unga mkono hili ,mh Mbowe,Said Issa,Mnyika,Heche, Catherine,
 
Back
Top Bottom