Kufikia uhuru na demokrasia kamili katika nchi yetu ni mapambano ya vita kamili. Lazima uwe na multiple specialized forces and tactics and strategies.Tangu Mbowe aanze kwenda huko hakuna hata jambo moja lililowahi kufanyiwa kazi na serikali, sijui ugumu wa Samia kufanya hivyo unatoka wapi, na sijui uvumilivu wa Mbowe utaendelea mpaka lini, naona utani unazidi.
- Lissu bado hajarudi nchini, hii inawezekana bado hajahakikishiwa usalama wake.
- Mikutano ya vyama vya siasa bado haijaruhusiwa japo ni takwa la kisheria.
- Wale wahujumu uchumi 19 bado wanakumbatiwa na Spika kule bungeni kinyume cha sheria.
Lazima Chadema ijipange na ipigane in both frontiers.Lazima ivipige vita vyema kipropoganda, kiuchumi, kidipromasia, kisheria,kisiasa, kiroho nk. Mfano mie si askari wa mtandao ingawa nipo hapa. Uwanja wangu ni vita vya kiroho na huko naupiga mwingi. Waache askari wa diplomasia au wa kisheria Kama akina Kibatala waupige mwingi kwenye special tactical area zao.
Kazi ya muhimu zaidi ni kujenga jeshi lenye vitengo vyote na kuviimarisha kwa Kila aina ya silaha na mbinu.
Kuishinda CCM inabidi kupigana nayo ardhini, majini, angani, chini ya ardhi, anga la juu na zaidi.