Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Hii mbinu waliitumia kwa Maalim Seif (Mwafaka) kule Zanzibar. Maalim aliposhinda uchaguzi wakafuta matokeo. Ni hivyo hivyo itakuwa kwa CHADEMA. Wanawapumbaza ili waongoze kwa amani hadi 2025 watakapoiba uchaguzi tena. Mbowe asiwe mjinga.
Unadhani wewe hiyo mbinu unaijua zaidi kuliko Mbowe?
 
Wakuu,

Muda huu M/Kiti wa CHADEMA na viongozi waandamizi 9 wa chama hicho wapo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Tutarajie jambo gani jipya? Ndo ukurasa mpya wa Siasa za Tanzania?

UPDATE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha majadiliano pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Mei, 2022.

Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waliohudhuria Kikao hicho ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Saidi Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Chama hicho.

View attachment 2232248View attachment 2232250
View attachment 2232257View attachment 2232258View attachment 2232259

View attachment 2232260
View attachment 2232570
Katika kipindi ambacho wanachama na viongozi wengi wa CDM bado wanakabiliwa na kesi nyingi za uchochezi ambazo walibambikiwa katika zama za utawala wa giza, huku wengine miongoni mwao wakiwa bado wapo korokoroni.

Katika kipindi ambacho baadhi ya wanachama ni wahanga wa kujishughulisha na shughuli za kisiasa ambao walilazimika kuikimbia nchi yao kwa ajili ya usalama wa uhai wao na kuamua kutafuta hifadhi katika nchi za ughaibuni

Katika kipindi ambacho wanachama wengi wamekuwa wahanga kwa kuonyesha mapenzi ya dhati kwa chama chao hasa pale walipiwajibika kukitetea kwa hali na mali na kujikuta wakidhulumiwa na kufilisiwa fedha zao.

Yapo mengi ya kuzungumza ili kufuta kumbukumbu mbaya iliyokuwepo kipindi cha utawala wa JPM. Madhila yaliyotokea katika kipindi cha utawala wa giza hayawezi kuachwa yapite tu, kipindi ambacho makada wa CDM waliishii kwa hofu, matesi, dhiki, taabu, jasho, machozi na damu ili kulipia mapenzi yao ya dhati kwa chama chao na kushiriki katika siasa.

Huu ndio muda muafaka wa kufanya mazungumzo, tena ya mara kwa mara, ili kuweza kufikia mustakabali mwema wa taifa letu. Hongera Rais wetu SSH kwa kuwa tayari na kukunjua mikono ya mazungumzo haya yanayoendelea.
 
Mkuu badala yake wafanye nini? Waandamane? Wako wapi waandamanaji
Waingie msituni? Liko wapi jeshi la kuingia msituni?
Ukiangalia hizo picha, inaonyesha upande mmoja, ukimtoa Rais, hakuna mshiriki mwanamke. Swali jeee, huko hakuna wanawake ambao wangefaa kwenye mazungumzo hayo?
 
Wanafuata nini ikulu kila mara kama sio kupotezeana muda?
Wewe kama ulikuwa kwenye akili yangu. Hivi kwanini Mambo yaliyomo kwenye katiba yaombwe kama hisani toka kwa rais?

Kwa kufanya hivi vyama vya upinzani vinajifunga miguu na mikono vyenyewe. Maana vinapoenda ikulu kuomba hisani kwa Mambo ambayo ni haki ya kikatiba rais anqvimba kichwa
 
Ukiangalia hizo picha, inaonyesha upande mmoja, ukimtoa Rais, hakuna mshiriki mwanamke. Swali jeee, huko hakuna wanawake ambao wangefaa kwenye mazungumzo hayo?
IMG_20220520_234403.jpg

Wewe ni muongo
 
Binafsi nimefurahi sana kuwaona viongozi wa juu wa Chadema wamepiga picha na raisi
 
Yule aliyetaka upinzani ufe kabla ya 2020 atakua anaramba ndimu sasa hivi.
SIASA SIO UGOMVI. NANI ANGEAMINI KUWA LEO KATAMBI AU SILINDE NI MAWAZIRI?

SUKUMA GANG WANAMALIZA BANDO KUTUKANA ILA:
mashinji
Gekuli
Silinde
Waitara
Katambi
Nasari
...
....
....
....
Ndio wanaolamba asali sasa hivi.
 
Na mimi nawashangaa wanaoshindwa kuelewa hii move ya Mama Samia.

Mjue Mama amezungukwa na viatu wengi.
Kama spika wa bumge yuko pale kwa lura za wizi.. unategemea ataacha kuchukua maamuzi ya kizandiki na maelekezo
 
Back
Top Bottom