Freeman Mbowe: "Mtu anaweza tu akashangiliwa kwenye majukwaa akapigiwa kura, lakini hakuna meritocracy (uwezo)". Je, dawa mujarabu ni ipi?

Freeman Mbowe: "Mtu anaweza tu akashangiliwa kwenye majukwaa akapigiwa kura, lakini hakuna meritocracy (uwezo)". Je, dawa mujarabu ni ipi?

Tunapendekeza Rais ajaye awe na haiba kama za mama Samia ili aendeleze ukuaji wa uchumi wa kati.
Wakati wa kipindi cha uchaguzi mwaka jana 2020, siku tatu Rais Samia alikuwa amepumzika nyumbani kwa maana alikuwa na uhakika wa ushindi kwa zaidi ya 95%.
 
Wakati wa kipindi cha uchaguzi mwaka jana 2020, siku tatu Rais Samia alikuwa amepumzika nyumbani kwa maana alikuwa na uhakika wa ushindi kwa zaidi ya 95%.
Anajua kuwa WALIPORA?
Kuna watu leo watakuja kusema SSH ,PM hawajui chochote katika Uporaji ule wa Uchaguzi mkuu na wa /Mitaa
 
Wakati wa kipindi cha uchaguzi mwaka jana 2020, siku tatu Rais Samia alikuwa amepumzika nyumbani kwa maana alikuwa na uhakika wa ushindi kwa zaidi ya 95%.
CCM Wengi ni waadilifu kama Rais Samia. Huyu mama Samia anapaswa kuwa role model ya wanawake wachapakazi hapa Tanzania.
 
CCM Wengi ni waadilifu kama Rais Samia. Huyu mama Samia anapaswa kuwa role model ya wanawake wachapakazi hapa Tanzania.
Waambie hao Chadema kuwa siasa za kihuni zimepitwa na muda na sasa wamuombe msamaha mama yetu Rais Samia.
 
Rais Samia anafanya kazi ya ziada kuhusu ardhi na sasa inarudi kwa Wananchi maana mikoa mingi Wananchi waliteseka sana.
Waambieni hao chadema kuwa Shauri yao kwa maana Rais Samia ni kiboko yao na anakubalika internationally.
 
SWALI LANGU: Ni utaratibu upi mpya utumike katika kupata watendaji bora wa kisiasa mbali na huu wa sasa ambao baadhi ya wakongwe wa tasnia hii (Freeman Mbowe) wanaona kuwa haufai?

Habari zenu ndugu zangu wa jamiiforums.

Jana siku ya Jumatatu May 10, 2021, wakati ninapitia makala kadhaa katika magazeti mbalimbali ya hapa Tanzania (kama ilivyo kawaida yangu kila siku) nikakutana na statement hii fupi ya mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe alipofanya mahojiano na gazeti la Mwananchi. Mbowe alisema ya kwamba;

“Demokrasia ni nzuri lakini najua ilivyokuwa vigumu kupata watendaji wa kisiasa kwa kupitia kura za jumla. Ndiyo maana nilitaka huo utaratibu ubadilishwe, kwa sababu mtu anaweza tu akashangiliwa kwenye majukwaa akapigiwa kura, lakini hakuna meritocracy (uwezo),”
==========
View attachment 1781350
==========
Mheshimiwa Mbowe alitaka huo utaratibu ubadilishwe. Je ubadilike na uwe upi? Kwa wale ambao mpo karibia na Mheshimiwa huyu mnaweza kumuuliza alikuwa anamaanisha nini? Labda kuna jambo alikuwa anataka kupendekeza ambalo litakuwa na matokeo chanya katika siasa za hapa Tanzania.

Kama wewe ni mtaalam wa sayansi ya siasa (Political Science) unaweza kupambanua Mwenyekiti alikuwa anataka ku-suggest kitu gani kwa manufaa ya Tanzania yetu sote? Au alikuwa anamaanisha tupandishe kiwango cha elimu kutoka kuwa darasa la saba (kujua kusoma na kuandika tu) mpaka kufika kidato cha nne?

Ninaomba kutoa angalizo kwa wale washabiki wa siasa chafu kutoka pande zote (CCM na CHADEMA) kwamba tusimtukane mtu katika suala hili lakini changia kama unajua alichokua anataka ku-recommend mwanasiasa muandamizi wa upinzani.

Je, unafikiri Mwenyekiti Mheshimiwa Freeman yupo sahihi? Kama yupo sahihi, dawa mujarabu ya changamoto hii ya uchaguzi ni ipi?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya wadau;
==========

==========

==========

==========

==========

==========
Kwa Lugha rahisi ntakupa mfano wa anachokimanisha...Chukulia mfano leo hii Babutale anateuliwa kuwa waziri wa Kilimo au Msukuma anateuliwa waziri wa Afya au kibajaji anapewa wizara ya Fedha..sheria ziko wazi kusudi uwe waziri lazima uwe mbunge kwanza...
 
Babu Tale ni kilaza sana aisee sijui hata CCM waliwaza nini mpaka kumpa shavu kubwa na kuwaacha akina Pascal Mayalla.
 
Rais Samia ni mbeba maono Kwa jinsi uchumi wa Tanzania unavyokuwa kwa kasi hadi 2025 tutakuwa tumeipiku south Africa.
Lissu hakuna kituo hata kimoja aliweza kuwa mbele ya Samia na JPM mwaka uchaguzi wa 2020. Kipigo alichopewa October 2020 kilimfanya awachukie Watanzania wote.
 
Back
Top Bottom