Freeman Mbowe: "Mtu anaweza tu akashangiliwa kwenye majukwaa akapigiwa kura, lakini hakuna meritocracy (uwezo)". Je, dawa mujarabu ni ipi?

Freeman Mbowe: "Mtu anaweza tu akashangiliwa kwenye majukwaa akapigiwa kura, lakini hakuna meritocracy (uwezo)". Je, dawa mujarabu ni ipi?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
SWALI LANGU: Ni utaratibu upi mpya utumike katika kupata watendaji bora wa kisiasa mbali na huu wa sasa ambao baadhi ya wakongwe wa tasnia hii (Freeman Mbowe) wanaona kuwa haufai?

Habari zenu ndugu zangu wa jamiiforums.

Jana siku ya Jumatatu May 10, 2021, wakati ninapitia makala kadhaa katika magazeti mbalimbali ya hapa Tanzania (kama ilivyo kawaida yangu kila siku) nikakutana na statement hii fupi ya mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe alipofanya mahojiano na gazeti la Mwananchi. Mbowe alisema ya kwamba;

“Demokrasia ni nzuri lakini najua ilivyokuwa vigumu kupata watendaji wa kisiasa kwa kupitia kura za jumla. Ndiyo maana nilitaka huo utaratibu ubadilishwe, kwa sababu mtu anaweza tu akashangiliwa kwenye majukwaa akapigiwa kura, lakini hakuna meritocracy (uwezo),”
==========
20210511_214103fr.jpg

==========
Mheshimiwa Mbowe alitaka huo utaratibu ubadilishwe. Je ubadilike na uwe upi? Kwa wale ambao mpo karibia na Mheshimiwa huyu mnaweza kumuuliza alikuwa anamaanisha nini? Labda kuna jambo alikuwa anataka kupendekeza ambalo litakuwa na matokeo chanya katika siasa za hapa Tanzania.

Kama wewe ni mtaalam wa sayansi ya siasa (Political Science) unaweza kupambanua Mwenyekiti alikuwa anataka ku-suggest kitu gani kwa manufaa ya Tanzania yetu sote? Au alikuwa anamaanisha tupandishe kiwango cha elimu kutoka kuwa darasa la saba (kujua kusoma na kuandika tu) mpaka kufika kidato cha nne?

Ninaomba kutoa angalizo kwa wale washabiki wa siasa chafu kutoka pande zote (CCM na CHADEMA) kwamba tusimtukane mtu katika suala hili lakini changia kama unajua alichokua anataka ku-recommend mwanasiasa muandamizi wa upinzani.

Je, unafikiri Mwenyekiti Mheshimiwa Freeman yupo sahihi? Kama yupo sahihi, dawa mujarabu ya changamoto hii ya uchaguzi ni ipi?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya wadau;
==========
alichokua anamaanisha nahisi inabidi utaratibu wa kumpata kiongozi upitie mchakato wa wasomi wabobezi ambao watakua na uwezo wakuchambua hoja za wagombea na sio tu kuamuliwa na watu ambao huenda hawamchagui kiongozi kwa hoja bali kwa kufuata mkumbo na rushwa.
==========
Tatizo hata hawa wasomi wabobezi kwa sasa nao wanaweza kununulika pia.

Rushwa ipo katika chanja zote si juu au chini yaani imegusa mazingira yote kwa wenye vyeo vikubwa au vidogo.

Na chaguzi nyingi tutalaumu bure ilikuwa hivi mara vile ila ukweli ni vyote vinatendeka kwa uchafu mkubwa "RUSHWA"

Naona adui yetu mkubwa hapa ni Rushwa na vita juu ya Rushwa kwa mfumo tulionao ni kama wa kufikirika.

Mapendekezo ya viongozi wengi zaidi ya 89% wameangukia hapo kwa adui yetu kupata nafasi walizonazo.

Maneno "wajumbe" yatakuja na kuondoka nenda rudi ila yote kwa yote rushwa ndio adui namba moja wa haki.
==========
..kuna mazingira ambapo KURA zinafaa.

..Na kuna mazingira ambapo UTEUZI unafaa.

..tunatakiwa tujiulize tuwe na mfumo gani wa kupiga kura ili kutuepusha au kupunguza uwezekano wa kuchagua watu wengi wa hovyo-hovyo.

..pia mfumo wetu wa uteuzi uwe na namna gani ili ku-weed out candidates ambapo hawana uwezo au viwango kwa nafasi husika.

..ukiwa na tume ya hovyo na kuhuni ya uchaguzi unakuwa umekaribisha watu wa hovyo au chama cha hovyo kushinda uchaguzi.

..ukiwa na mfumo wa uteuzi wa kificho unaomtegemea mtu mmoja upo then upo uwezekano mkubwa wa watu wasio na sifa kuteuliwa.
==========
Au tuwe na mabunge mawili (mmoja la kuteuliwa liwe level ya juu)? Tunaweza kupunguza ukubwa wa bunge lililopo (na unapunguza malipo pia?) na ku create hilo bunge dogo (lakini la juu kimadaraka). Let say hilo bunge la juu, linakuwa na wabunge wa kuteuliwa (au namna nyingine ya kupatikana kwa merit - CV, uwezo?) mmoja kutoka kila mkoa wa Tz.

Unaweza pia kuondoa nafasi za RCs na DCs ili kupunguza gharama kwa nchi.
==========
Namaanisha kuweka standards ambazo zikifuatwa zitanufaisha raia bila kujali itikadi zao za vyama.
Aidha, mifumo mizuri ikiwekwa itawalazimu hata wasiotaka wafuate taratibu hizo zenye tija na maslahi kwa taifa.

Kama standards zilizowekwa ni nzuri, udhaifu wowote unaofanyika ndani ya vyama (bila kujali ni chama gani) utapimwa na kuonekana wazi. Hivyo mfumo utawakataa automatically.

Vyama na madaraka ni mambo ya muda, lakini mifumo mizuri inaishi hata baada ya tawala nyingi kupita. Kuweka standards ambazo zikifuatwa zitanufaisha raia bila kujali itikadi zao za vyama. Aidha, mifumo mizuri ikiwekwa itawalazimu hata wasiotaka wafuate taratibu hizo zenye tija na maslahi kwa taifa.

Kama standards zilizowekwa ni nzuri, udhaifu wowote unaofanyika ndani ya vyama (bila kujali ni chama gani) utapimwa na kuonekana wazi. Hivyo mfumo utawakataa automatically. Vyama na madaraka ni mambo ya muda, lakini mifumo mizuri inaishi hata baada ya tawala nyingi kupita.
==========
Tukajifunze Kenya Jaji mkuu anavyopatikana kwa mfano.

Au wabunge wa viti maalumu wanavyopatikana.

Au Mwanasheria mkuu wa serikali anavyopatikana nk....nk!
 
Mwambieni ndugu mwenyekiti ametuacha hewani kwa kutuambia tatizo linalokabili siasa zetu bila kutoa suggestions ya nini kifanyike. Mifumo bora ya kisiasa ina manufaa kwa wote chama tawala na upinzani.
 
Imekuwa ni desturi kwa chadema kujiona wana haki ya kukosoa tu!
Kwa muda mrefu uhuru wa habari kichwani mwa Chadema unamanisha ni kutukana na kukosoa wengine ila wao kukosolewa hapana.
Kwenye mada hii Mbowe kamtukana nani? Hii sio mada ya CCM na CHADEMA bali ni mfumo mzima wa chaguzi za kisiasa za Tanzania.

Mkuu, weka ukada pembeni kisha tujadili suala la manufaa kwa taifa letu.
 
alichokua anamaanisha nahisi inabidi utaratibu wa kumpata kiongozi upitie mchakato wa wasomi wabobezi ambao watakua na uwezo wakuchambua hoja za wagombea na sio tu kuamuliwa na watu ambao huenda hawamchagui kiongozi kwa hoja bali kwa kufuata mkumbo na rushwa.
 
Raha ya JamiiForums kuna mazuzu hayajui hata maana ya "MERITOCRACY", ila yatakuja kubisha na kumwaga povu mpaka mishipa ya sehemu za siri iyasimame.

Sihami JF ng'o, ntabakia kuwa member mpaka dakika za majeruhi.
 
Safi sana mkuu. Wewe una akili sana na upo tayari kuweka ufuasi kando na kujadili suala lenye manufaa kwa mfumo mzima wa siasa.
 
Kwenye mada hii Mbowe kamtukana nani? Hii sio mada ya CCM na CHADEMA bali ni mfumo mzima wa chaguzi za kisiasa za Tanzania.

Mkuu, weka ukada pembeni kisha tujadili suala la manufaa kwa taifa letu.
Huyo ni bora liende tu
Elitwege

Ova
 
alichokua anamaanisha nahisi inabidi utaratibu wa kumpata kiongozi upitie mchakato wa wasomi wabobezi ambao watakua na uwezo wakuchambua hoja za wagombea na sio tu kuamuliwa na watu ambao huenda hawamchagui kiongozi kwa hoja bali kwa kufuata mkumbo na rushwa.
Tatizo hata hawa wasomi wabobezi kwa sasa nao wanaweza kununulika pia.

Rushwa ipo katika chanja zote si juu au chini yaani imegusa mazingira yote kwa wenye vyeo vikubwa au vidogo.

Na chaguzi nyingi tutalaumu bure ilikuwa hivi mara vile ila ukweli ni vyote vinatendeka kwa uchafu mkubwa "RUSHWA"

Naona adui yetu mkubwa hapa ni Rushwa na vita juu ya Rushwa kwa mfumo tulionao ni kama wa kufikirika.

Mapendekezo ya viongozi wengi zaidi ya 89% wameangukia hapo kwa adui yetu kupata nafasi walizonazo.

Maneno "wajumbe" yatakuja na kuondoka nenda rudi ila yote kwa yote rushwa ndio adui namba moja wa haki.
 
Raha ya JamiiForums kuna mazuzu hayajui hata maana ya "MERITOCRACY", ila yatakuja kubisha na kumwaga povu mpaka mishipa ya sehemu za siri iyasimame.

Sihami JF ng'o, ntabakia kuwa member mpaka dakika za majeruhi.

Ungelifafanua hilo neno ungeondoa hizo bureaucracy za kuja kumpata mtu wa kulielezea. Haya ndiyo mambo yamesababisha juzi mechi imeahirishwa kishamba, raia wameporwa pesa zao na taimu zao na nguvu kazi. Shame!!!
 
Infantry Soldier ,

..Mbowe alikuwa anazungumzia suala / tukio specific wakati alipokuwa anashawishiwa kugombea Uenyekiti wa chama.

..Mbowe aliweka shinikizo kwamba akichaguliwa kuwa Mwenyekiti basi Katibu Mkuu awe Dr.Wilbroad Slaa.

..Mtizamo wa Mbowe ulikuwa kwamba Katibu Mkuu ni kama technocrat ktk chama hivyo mchakato wa kura kama wa kumpata Mwenyekiti, Makamu, etc etc unaweza usiwe njia nzuri ya kumpata mtu atakayejaza nafasi ya Katibu Mkuu.

..Hivyo ndivyo nilivyomuelewa alichokuwa akimaanisha Freeman Mbowe. Na kauli hiyo aliitoa wakati akihojiwa na Tundu Lissu kuhusu historia ya Chadema na ilikuwaje na nini kilitokea mpaka Mbowe akawa mwenyekiti wa Chadema.

Cc Man in the Middle
 
Lengo la Mbowe ni kutaka sheria itakayokuwa inaruhusu viti maalumu kwa jinsia zote, yani kwa wanaume na wanawake ili mgombea akiangukia pua ktk uchaguzi kama alivyoanguka yeye, basi aingie bungeni kwa kupitia mgongo wa viti maalumu kama ilivyotokea sasa hivi kwa kina Mdee na genge lake. Kitendo cha kina mdee kupiga hela kupitia vikao na mishahara ya bunge kina muumiza sana kichwa Mbowe na genge lake.
 
Mh Mbowe leñgo ni ukosefu wa viongozi waliochaguliwa kihalali hivyo nivigumu kupata competence leaders
 
..Mtizamo wa Mbowe ulikuwa kwamba Katibu Mkuu ni kama technocrat ktk chama hivyo mchakato wa kura kama wa kumpata Mwenyekiti, Makamu, etc etc unaweza usiwe njia nzuri ya kumpata mtu atakayejaza nafasi ya Katibu Mkuu.
Hayo maneno niliyo bold hajayasemwa na Mbowe katika mahojiano yale, sasa unafikiri wasomaji kama sisi tutaelewaje mkuu? Kwani kuna tofauti gani kati ya chaguzi za ndani ya vyama na zile za nje ya vyama (Wabunge na Madiwani)? Michakato mbona ni ni ile ile tu, come-pain (campaign) kwanza kisha box la kura linafuata.

Au aliyasema ila mimi ndio sijayaona? Unaweza kuniwekea screenshot basi mkuu. Alafu tangia lini katibu mkuu akapigiwa kura ndani ya chama chochote kile cha kisiasa hata CCM, NCCR na CUF hakuna hili sasa yeye alitaka kuiga kutoka wapi?
 
Tukajifunze Kenya Jaji mkuu anavyopatikana kwa mfano.

Au wabunge wa viti maalumu wanavyopatikana.

Au Mwanasheria mkuu wa serikali anavyopatikana nk....nk!
Asante kwa ushauri mzuri mkuu, ila kwanini Kenya na sio nchi nyingine?
 
Back
Top Bottom