Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
SWALI LANGU: Ni utaratibu upi mpya utumike katika kupata watendaji bora wa kisiasa mbali na huu wa sasa ambao baadhi ya wakongwe wa tasnia hii (Freeman Mbowe) wanaona kuwa haufai?
Habari zenu ndugu zangu wa jamiiforums.
Jana siku ya Jumatatu May 10, 2021, wakati ninapitia makala kadhaa katika magazeti mbalimbali ya hapa Tanzania (kama ilivyo kawaida yangu kila siku) nikakutana na statement hii fupi ya mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe alipofanya mahojiano na gazeti la Mwananchi. Mbowe alisema ya kwamba;
“Demokrasia ni nzuri lakini najua ilivyokuwa vigumu kupata watendaji wa kisiasa kwa kupitia kura za jumla. Ndiyo maana nilitaka huo utaratibu ubadilishwe, kwa sababu mtu anaweza tu akashangiliwa kwenye majukwaa akapigiwa kura, lakini hakuna meritocracy (uwezo),”
==========
==========
Mheshimiwa Mbowe alitaka huo utaratibu ubadilishwe. Je ubadilike na uwe upi? Kwa wale ambao mpo karibia na Mheshimiwa huyu mnaweza kumuuliza alikuwa anamaanisha nini? Labda kuna jambo alikuwa anataka kupendekeza ambalo litakuwa na matokeo chanya katika siasa za hapa Tanzania.
Kama wewe ni mtaalam wa sayansi ya siasa (Political Science) unaweza kupambanua Mwenyekiti alikuwa anataka ku-suggest kitu gani kwa manufaa ya Tanzania yetu sote? Au alikuwa anamaanisha tupandishe kiwango cha elimu kutoka kuwa darasa la saba (kujua kusoma na kuandika tu) mpaka kufika kidato cha nne?
Ninaomba kutoa angalizo kwa wale washabiki wa siasa chafu kutoka pande zote (CCM na CHADEMA) kwamba tusimtukane mtu katika suala hili lakini changia kama unajua alichokua anataka ku-recommend mwanasiasa muandamizi wa upinzani.
Je, unafikiri Mwenyekiti Mheshimiwa Freeman yupo sahihi? Kama yupo sahihi, dawa mujarabu ya changamoto hii ya uchaguzi ni ipi?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Maoni ya wadau;

==========alichokua anamaanisha nahisi inabidi utaratibu wa kumpata kiongozi upitie mchakato wa wasomi wabobezi ambao watakua na uwezo wakuchambua hoja za wagombea na sio tu kuamuliwa na watu ambao huenda hawamchagui kiongozi kwa hoja bali kwa kufuata mkumbo na rushwa.
==========Tatizo hata hawa wasomi wabobezi kwa sasa nao wanaweza kununulika pia.
Rushwa ipo katika chanja zote si juu au chini yaani imegusa mazingira yote kwa wenye vyeo vikubwa au vidogo.
Na chaguzi nyingi tutalaumu bure ilikuwa hivi mara vile ila ukweli ni vyote vinatendeka kwa uchafu mkubwa "RUSHWA"
Naona adui yetu mkubwa hapa ni Rushwa na vita juu ya Rushwa kwa mfumo tulionao ni kama wa kufikirika.
Mapendekezo ya viongozi wengi zaidi ya 89% wameangukia hapo kwa adui yetu kupata nafasi walizonazo.
Maneno "wajumbe" yatakuja na kuondoka nenda rudi ila yote kwa yote rushwa ndio adui namba moja wa haki.
==========..kuna mazingira ambapo KURA zinafaa.
..Na kuna mazingira ambapo UTEUZI unafaa.
..tunatakiwa tujiulize tuwe na mfumo gani wa kupiga kura ili kutuepusha au kupunguza uwezekano wa kuchagua watu wengi wa hovyo-hovyo.
..pia mfumo wetu wa uteuzi uwe na namna gani ili ku-weed out candidates ambapo hawana uwezo au viwango kwa nafasi husika.
..ukiwa na tume ya hovyo na kuhuni ya uchaguzi unakuwa umekaribisha watu wa hovyo au chama cha hovyo kushinda uchaguzi.
..ukiwa na mfumo wa uteuzi wa kificho unaomtegemea mtu mmoja upo then upo uwezekano mkubwa wa watu wasio na sifa kuteuliwa.
==========Au tuwe na mabunge mawili (mmoja la kuteuliwa liwe level ya juu)? Tunaweza kupunguza ukubwa wa bunge lililopo (na unapunguza malipo pia?) na ku create hilo bunge dogo (lakini la juu kimadaraka). Let say hilo bunge la juu, linakuwa na wabunge wa kuteuliwa (au namna nyingine ya kupatikana kwa merit - CV, uwezo?) mmoja kutoka kila mkoa wa Tz.
Unaweza pia kuondoa nafasi za RCs na DCs ili kupunguza gharama kwa nchi.
==========Namaanisha kuweka standards ambazo zikifuatwa zitanufaisha raia bila kujali itikadi zao za vyama.
Aidha, mifumo mizuri ikiwekwa itawalazimu hata wasiotaka wafuate taratibu hizo zenye tija na maslahi kwa taifa.
Kama standards zilizowekwa ni nzuri, udhaifu wowote unaofanyika ndani ya vyama (bila kujali ni chama gani) utapimwa na kuonekana wazi. Hivyo mfumo utawakataa automatically.
Vyama na madaraka ni mambo ya muda, lakini mifumo mizuri inaishi hata baada ya tawala nyingi kupita. Kuweka standards ambazo zikifuatwa zitanufaisha raia bila kujali itikadi zao za vyama. Aidha, mifumo mizuri ikiwekwa itawalazimu hata wasiotaka wafuate taratibu hizo zenye tija na maslahi kwa taifa.
Kama standards zilizowekwa ni nzuri, udhaifu wowote unaofanyika ndani ya vyama (bila kujali ni chama gani) utapimwa na kuonekana wazi. Hivyo mfumo utawakataa automatically. Vyama na madaraka ni mambo ya muda, lakini mifumo mizuri inaishi hata baada ya tawala nyingi kupita.
Tukajifunze Kenya Jaji mkuu anavyopatikana kwa mfano.
Au wabunge wa viti maalumu wanavyopatikana.
Au Mwanasheria mkuu wa serikali anavyopatikana nk....nk!