Freeman Mbowe: "Mtu anaweza tu akashangiliwa kwenye majukwaa akapigiwa kura, lakini hakuna meritocracy (uwezo)". Je, dawa mujarabu ni ipi?

A. Kipaji cha kuongoza mtu halazimishwi au kujifunza kukipata akiwa tayari kwenye mfumo.
B. Bidii ya kazi hii unaweza kubadilika kulingana na wakati au watu unaofanya nao kazi.
C. Uwezo wa kuleta matokeo chanya kupitia uongozi na kazi zako, wengi ni bora liende.
Kuwapata hawa siyo jambo la kupangiana kiholela, mtu au kundi lenye ushawishi liamulie wengine.

Nadhani bado anayo nafasi ya kushauri zaidi ni njia gani bora au mfumo wa kupata viongozi wazuri.
 
Mkuu, hapa neno mfumo bila shaka una maanisha akiwa tayari ndani ya chama cha siasa? Au nimekosea?
Namaanisha kuweka standards ambazo zikifuatwa zitanufaisha raia bila kujali itikadi zao za vyama.
Aidha, mifumo mizuri ikiwekwa itawalazimu hata wasiotaka wafuate taratibu hizo zenye tija na maslahi kwa taifa.

Kama standards zilizowekwa ni nzuri, udhaifu wowote unaofanyika ndani ya vyama (bila kujali ni chama gani) utapimwa na kuonekana wazi. Hivyo mfumo utawakataa automatically.

Vyama na madaraka ni mambo ya muda, lakini mifumo mizuri inaishi hata baada ya tawala nyingi kupita.
 
Thanks bro.
 
A. Kipaji cha kuongoza mtu halazimishwi au kujifunza kukipata akiwa tayari kwenye mfumo.
B. Bidii ya kazi hii unaweza kubadilika kulingana na wakati au watu unaofanya nao kazi.
C. Uwezo wa kuleta matokeo chanya kupitia uongozi na kazi zako, wengi ni bora liende.
Kuwapata hawa siyo jambo la kupangiana kiholela, mtu au kundi lenye ushawishi liamulie wengine.

Nadhani bado anayo nafasi ya kushauri zaidi ni njia gani bora au mfumo wa kupata viongozi wazuri.
Swadakta
 
Tukajifunze Kenya Jaji mkuu anavyopatikana kwa mfano.

Au wabunge wa viti maalumu wanavyopatikana.

Au Mwanasheria mkuu wa serikali anavyopatikana nk....nk!
Mkuu Unamwaga madini hadi raha, sijui kwa nini mlikuwa mnajitoa akili kipindi cha jiwe, akili zimerudi sawa big up dogo tujenge nchi.
 
Muache mtu aongee freely wee jamaa
Hayo ni maoni yangu kwake, lakini yuko huru huru kabisa hata kutoa 'vapour'.
Kama member wa jf, nitacheka na labda ku comment, lakini sina kabisa uwezo wa kumzuia.
Hata hivyo ndugu, katika maisha, ukitaka kujifunza na kujipa nafasi ya kupanua uelewa wako, kamwe usichukie maoni hasa unapokosolewa. AMEN
 
Sawa kaka
 
Back
Top Bottom