Tuache utapeli wa siasa kumfananisha mbowe na regends wapigania uhuru Afrika.labda uniambie kuwa mbowe ni mpigania madaraka Tanzania zaidi ya miaka ishirini na kitu bila mafanikio.kama kweli mpigania uhuru na democrasia mbona alifanya haya.
1) kumtosa Dr slaa na wenzake kwenye kiti cha urais aliyesota nao siku zote usiku na mchana na kuingiza mamluki ndani ya chama na kugombea urais
2) mbona alikula matapishi yake aliyohubiri miaka yote ambayo JPM alitekeleza asilimia kubwa ya ilani ya chadema lakini akaishia kumpinga na kusema wanahitaji maendeleo ya watu sio vitu ndo democrasia na uhuru
3) kama kweli mpenda mageuzi na mwanademocrasia mbona alikuwa mkwepa kodi za serikali kwa kutolipa deni alikokuwa anadai na serikali billicanas jengo la NHC
4)Anamwambia mama yetu afate haki je? Yeye ni muumini wa haki? Mbona aliwashurutisha wabunge wa chadema wasusie vikao vya bunge kisa corona angali wabunge wengi hasa ccm wakiwa bungeni bila kujali janga la corona hiyo ndo kupigania uhuru na demicrasia?
5)Nchi ipo kwenye majonzi kwa kufiwa na Rais JPM yeye anafanya matembezi Nchi nzima kumtukana Marehemu na kudai katiba mpya ambayo JK aliwapa wafanye mchakato ila mwishoni wkasusia yeye na wafuasi wake ndo democrasia na kupigania uhuru ivo?
Mpigania uhuru na democrasia wa kweli
1) yeye kwanza anajikana nafsi yake na kutetea wanyonge kwa maneno na vitendo bila kujali gharama za maisha yake huko mbeleni
2) anakuwa kioo kwa jamii kitabia na maadili kufuata sheria na miongozo ya tawala zilizopo na kudai uhuru na democrasia kwa kufata sheria
3)Anakuwa wa kwanza kusimamia shughuli za maendeleo na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora bila kujali itikadi za chama chake Nchi na wananchi kwanza chama baadae
4)Anakuwa mshauri kwa viongozi wenzi sio kulalamika na kukejeli wenzie na mengine mengi mazuri