Jamani Mie ni CCM damu lakini Mbowe apewe heshima yake,kuongoza Chama cha upinzani Afrika ni zaidi ya kuwa hata Rais wa Jamhuri ya Tanzania maana unakuwa unapambana na MTU ambaye una resources zote ambazo anaweza kutumia kukumaliza.
Ni ngumu sana kukijenga Chama,ila unaweza kukibomoa ndani tu ya Siku ikawa hasara hata kwa Wananchi kuna kujenga Chama kingine tena cha upinzani kufikia level ambapo imefika CDM.
Imagine Leo hii Ndio Chama angekabidhiwa Kitila Mkumbo/Zitto au Yule Marehemu Chacha wangwe-hiyo CDM ingekuwepo??.huwezi kuongoza Chama cha Upinzani kama huna pesa utaishia mikononi kwa Chama tawala tu.
Kama Mbowe ataachia Chama amkabidhi Lissu au Prof Safari hao ndio pekee nawaona sana upinzani toka Damuni,tatizo lao kubwa hawana pesa hivyo ni ngumu kuongoza Chama.