Pre GE2025 Freeman Mbowe nyamaza au Ingia CCM 100% maana wewe ni mtoa taarifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Siasa tunazichukulia serious sana sie akina "kalikonji" ila wao hyo ni biashara kama biashara zingine.

Mbowe, kikwete na Zitto ni marafiki sana, wanakula bata sio mchezo, wala hawana njaa kama zetu.

Kama kuna mtu anaamini eti CCM na Upinzani sijui CHADEMA, ACT, NK wapo kwa ajili yao.. huyo mtu atakua hamnazo na hajui lolote kuhusu siasa za nchi hii ya Tanzagiza.
 

Acheni unafiki. Juzi mlikuwa mnamuita Mbowe gaidi, Leo mmebadilisha usemi.
 

Umenena kweli, tukileta uccm na CHADEMA kwenye mambo ya kanisa na misikiti, tutaharibu Sana.
 
watu wamΓ©kasilika mbowe kukosolewa!
na hao wanaongoza kuikosoa ccm

Unamkosoa mwenyekiti wa harambee ya kanisa kisa kapokea pesa ya mchango kutoka kwa rais?. Yani ulitaka Mbowe akatae pesa ya ujenzi kisa imetoka CCM. Halafu fuatilieni ibada nzima sio kuweka vi clip, maana waliochangia ni wengi sana Hadi Wazuri Mkuu majaliwa.
 

Tofautusha personalities na chama Kama chombo kinachojitegemea. Mbowe kuwa na urafiki haimanishi CHADEMA Kama chama ni marafiki wa Kikwete.
 

Kosa la Mbowe ni lipi? kuwa Mwenyekiti wa Harambee na kusoma waliotoa pesa za mchango. Maana alisoma majina karibia thelathini na la mwisho likawa la Rais Samiah. Kosa lake lipi?. Halafu Mbowe kaanza kuwa Mbunge tangu mwaka 2000. Huko kote kaonewa huruma?. Punguza unafiki
 
Hivi Mbowe ameshindwa Nini kutumia ukaribu wake na Samia kujua kuhusu Ben Saanane

Kwa hivyo Mbowe ndio jeshi la polisi?. Yani jeshi la polisi lipo kimya wewe unahangaika na Mbowe. Baadala upige kelele kwa jeshi la polisi wewe unahangaika na raia .
 

Mchango ni wa KKKT si wa Mbowe. Mbowe ni kiongozi tu wa harambee. Na waliochangia ni Wendi sana.
 
Mwenyekiti wa chama cha siasa kaacha kujenga ofisi ya chama ya hadhi kitaifa, kaenda kujenga kanisa lake kwao.

Mpaka hapo hata kama hujui kusoma, hiyo picha tu unatakiwa kuielewa.

Hivi kanisa la KKKT kajenga Mbowe?. Msilazimishe uongo.
 
Huwa wacheka sana nikimuona mtu anasema mbowe ni kiongozi wao [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hivi unakubali vipi kuongozwa na mtu mpumbavu na mpuuzi kama Dj mbowe[emoji53][emoji53][emoji53][emoji53] ngoja tu ninyamaze .

Ukiona mtu anakimbilia matusi Kama wewe huyo ndio mpumbavu.
 
................ Magufuli aliharibu watu na propaganda za chuki!
 
Mchango ni wa KKKT si wa Mbowe. Mbowe ni kiongozi tu wa harambee. Na waliochangia ni Wendi sana.
Kitu cha kwanza kabisa, rais hatakiwi kuchangia shughuli za dini. Hili linaharibu Separation of Church and State.

Kitu cha pili, kila mtu mwenye kanisa lake akitaka rais achangie shilingi milioni 150 rais hataweza. Rais anajiwekea mazingira ya kuonekana anapendelea sehemu fulani kisiasa.

Kitu cha tatu, denokrasia si tu inatakiwa ifanyike, bali pia inatakuwa kuonekana kuwa imefanyika. Hapa kuna muonekano wa kumuhonga Mbowe. Kqma mchango ninwa KKKT kwa nini Samia hakuchangia Uyole kaenda kuchangia kanisa la kwa Mbowe?

Kitu cha nne, Samia hajachaguliwa kujenga makanisa. Hili halimo katika ilani ya CCM. Katika nchi ambayo haifuati dini, haya ni matumizi mabaya ya pesa za wananchi. Waacheni waumini wachangishane wenyewe makanisani.

Kitu cha tano, Mbowe anajiwekea mazingira ya kutoweza kumkemea Samia inavyotakiwa. Utamkemea vipi Boss Lady anayekufadhili mpaka kwenye kujenga kanisa?

Kwa sasa niishie hapa tu.
 
Hivi kanisa la KKKT kajenga Mbowe?. Msilazimishe uongo.
Unaelewa Separation of Church and State ni nini?

Au unabisha kienyejienyeji tu?

Ni hivi, katika nchi secular kama yetu, rais kuchangia ujenzi wa kanisa lolote tayari ni makosa.

Mbowe kumualika rais kuchangia ujenzi wa kanisa kwao ni makosa zaidi, kwa rais na kwa Mbowe.

Nyerere alikuwa Mkatoliki kindakindaki, yule wa kwenda kanisani kila siku St. Peter's pale. Lakini hakufanya ujinga huu. Alielewa Separation of Church and State ni nini.

Umeelewa somo hilo?
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Hii hoja naona watu wanapuyanga tu...

Yaani hatujui jinsi shughuli za uchangishaji zinavyofanyika??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…