Pre GE2025 Freeman Mbowe nyamaza au Ingia CCM 100% maana wewe ni mtoa taarifa

Pre GE2025 Freeman Mbowe nyamaza au Ingia CCM 100% maana wewe ni mtoa taarifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Siasa tunazichukulia serious sana sie akina "kalikonji" ila wao hyo ni biashara kama biashara zingine.

Mbowe, kikwete na Zitto ni marafiki sana, wanakula bata sio mchezo, wala hawana njaa kama zetu.

Kama kuna mtu anaamini eti CCM na Upinzani sijui CHADEMA, ACT, NK wapo kwa ajili yao.. huyo mtu atakua hamnazo na hajui lolote kuhusu siasa za nchi hii ya Tanzagiza.
 
Comrade Makonda hakuongea kwa bahati mbaya wala kukurupuka, aliongea ukweli mtupu. Freeman Mbowe, Ntobi, Salim Mwalimu, na Bonifas Mwita ni baadhi tu, ya watoa taarifa ndani ya Chadema. Imefika muda tuseme kila kitu kwa uwazi kwamba, Chadema ina wazalendo wachache. Wengine wote wachumia tumbo na watoa Taarifa wakiongozwa na Freeman Mbowe.

Majuzi, Mr. Mbowe akita KKKT NSHARA Machame, alitangaza hadharani kwamba, Rais Samia alitoa mchango wa TZS 150million, ambayo kwa lugha nyingine ni “Endorsement” ya Rais Samia 2025. Mbowe amewatangazia watanzania kwamba mgombea wake 2025 ni Samia Suluhu Hassan. Bila kumung’unya maneno niulize maswali mawili tuu. Zile Toyota Landcruiser Mr. Mbowe alizitoa wapi? Na ile Chopper, fedha zake zilitoka wapi?

Kadhalika, Mr. Freeman Mbowe aliwaalika Covid-19 wakiongozwa na Mr. Alima Mdee kwenye hiyo harambee ikimaanisha kwamba, kwa muda mrefu, Mr. Mbowe amekuwa akiwakumbatia COVID-19 ndani ya CDM. Jiulizeni, Tulia Ackson anatoa wapi jeuri ya kuwakumbatia hao COVID-19? Wote wanalindwa na Mr. Freeman Mbowe na hawakwenda KKKT NSHARA Machame Kimakosa. Wote walienda kueneza mema ya viongozi wa CCM kwa mualiko wa Mr. Mbowe..Kwa maana hiyo, Mr. Mbowe na Covid-19 ni kitu kimoja. Kadhalika Samia na Mbowe ni kitu kimoja. Mbowe ni mtoa taarifa

Tukiwa wana CCM. Hawa watu wa CHADEMA wanatukera. Either waingie CCM au wanyamaze. Sisi hatuwataki maana wanaonyesha kufanya siasa za makueni. wanaunga mkono siasa za makundi. Wanamuunga mkono kundi la Samia.

Mr. Freeman Aikeli Mbowe, chagua moja. Baki ndani ya CDM mazima, au njoo ccm kundi la Samia 100%. Hatupendi unalolifanya maana unawavuruga Chadema na wana CCM vilevile. Kama umeshiba asali, basi jiuzulu uenyekiti na kukaa kimya, ila sisi hatukutaki ndani ya CCM. Tunajua lengo lako, ni kutengeneza ukaribu tena na Rais Samia, maana taarifa zilikufikia za Samia kuchukia ulivyomponda majukwaani baada ya kula hela zake za kukodi Elicopter na Magari ya Mikutano mikoani.

Acheni unafiki. Juzi mlikuwa mnamuita Mbowe gaidi, Leo mmebadilisha usemi.
 
Mleta uzi punguza bangi. Mbowe ni mtu mwenye busara sio kama Mdude. Mbowe anaifahamu hii nchi kuliko viongozi wengi wa serikali. Hawezi kuitanguliza CHADEMA kabla ya Tanzania. Acha siasa za chuki zisizo na tija. Watu hawawezi kuishi kama maadui hadi kwenye maisha ya kawaida. CHADEMA na CCM zinapambana kisiasa kwa hoja sio hadi kwenye shughuli za kijamii kama ujenzi wa kanisa

Umenena kweli, tukileta uccm na CHADEMA kwenye mambo ya kanisa na misikiti, tutaharibu Sana.
 
watu wamékasilika mbowe kukosolewa!
na hao wanaongoza kuikosoa ccm

Unamkosoa mwenyekiti wa harambee ya kanisa kisa kapokea pesa ya mchango kutoka kwa rais?. Yani ulitaka Mbowe akatae pesa ya ujenzi kisa imetoka CCM. Halafu fuatilieni ibada nzima sio kuweka vi clip, maana waliochangia ni wengi sana Hadi Wazuri Mkuu majaliwa.
 
Siasa tunazichukulia serious sana sie akina "kalikonji" ila wao hyo ni biashara kama biashara zingine.

Mbowe, kikwete na Zitto ni marafiki sana, wanakula bata sio mchezo, wala hawana njaa kama zetu.

Kama kuna mtu anaamini eti CCM na Upinzani sijui CHADEMA, ACT, NK wapo kwa ajili yao.. huyo mtu atakua hamnazo na hajui lolote kuhusu siasa za nchi hii ya Tanzagiza.

Tofautusha personalities na chama Kama chombo kinachojitegemea. Mbowe kuwa na urafiki haimanishi CHADEMA Kama chama ni marafiki wa Kikwete.
 
Mbowe anataka haonewe uruma na Samia amwachie kiti cha ubunge jimbo la Hai maisha yaendelee, Tanganyika tunakuja kupata upinzani wa kweli kizazi hiki cha Mbowe/Zitto kikitoweka maana hawa Sio wanasiasa bali wajasilisiasa, Siasa wanaifanya kama ujasiriamali wao wanaangalia furusa kwa watawala, halafu wanakuja na maneno mepesi eti Siasa sio uhadui, labda wawadanganye wajingawajinga ambao hawajui mambo ya Siasa,ukiwa mwanasiasa kwelikweli lazima uwe adui wa watawala.Mbowe kaisha ramba asali tusidanganyane.

Kosa la Mbowe ni lipi? kuwa Mwenyekiti wa Harambee na kusoma waliotoa pesa za mchango. Maana alisoma majina karibia thelathini na la mwisho likawa la Rais Samiah. Kosa lake lipi?. Halafu Mbowe kaanza kuwa Mbunge tangu mwaka 2000. Huko kote kaonewa huruma?. Punguza unafiki
 
Kwanza naandika kama Mtanzania independent ambaye sina chama, na kwa kweli nina sympathy na upinzani zaidi.

Kwa hiyo, siandiki kama chawa wa CCM.

Kwa maneno mengine, ningefurahi sana Mbowe angekuwa anafanya vizuri.

Mbowe ana ji contradict sana. Kama Mwenyekiti wa CHADEMA alitakiwa kuelewa kanuni za msingi za Separation of Church and State.

Kwa kumualika Samia na kukubali mchango wa shilingi milioni 150 kwenye shughuli ya kanisa lake kwao, inakuwa kama kakubali kuhongwa na Samia.

Mimi sikuwa na tatizo Mbowe kushiriki maongezi ya maridhiano, angeweza kusema yeye ni kiongozi moderate aliyekuwa anatafuta maridhiano tu. Ingawa hata hayo yalikuwa yanakwenda kwenye dead end, tulijua tu. Lakini, mara nyingine kiongozi wa upinzani anahitaji kuchukua njia inayompeleka kwenye dead end ili kutuonesha kuwa alikuwa na nia ya maridhiano, lakini upande wa pili umekwamisha hapa na hapa. Ndiyo maana hata mahakamani upinzani huwa unafungua kesi ambazo tunajua utashindwa, lakini wanataka kuweka rekodi kwamba tulifungua kesi hivi, mahakama ikatuonea hivi.

Kwa hiyo, hata kwenye maridhiano alikopingwa na watu wengi, mimi niliona kuwa Mbowe bado ana nafasi ya ku make sense.

Lakini huku kwenye kumualika Samia atoe shilingi milioni 150, Mbowe kajitia doa sana. Yani hata kiongozi wa CCM kumualika Samia na Samia kuchangia shilingi milioni 150 kwenye kanisa la huyo kiongozi ni tatizo. Anavunja kanuni za Separation of Church and State.

Nyerere katawala miaka 24. Alikuwa anakwenda kanisani kila siku akiwa Dar. St. Peters asubuhi kabisa utamkuta pale. Lakini hakufanya mchezo huu wa kuchangia kanisa pesa. Si kwa style na kiasi hiki.

Mbowe kama Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, anatakiwa kujua kuwa, demokrasia ni pamoja na separationnof church and state.

This is such a big disappointment.

Kama huyu kiongozi mkubwa hivi CHADEMA anaweza kufanya strategic mistake kubwa hivi hadharani, huko nyuma ya pazia anaboronga vipi?

In law, there is a principle. Justice must not only be done. It must appear to be done. Democracy as part of the rule of law falls under the same principle. It must not only be fulfilled, it must appear to be fulfilled.

Appearances matter. Right now, it appears as if Mr. Mbowe has been bought. Very cheaply indeed.

Kwa uongozi huu bado CHADEMA inategemea kuishinda CCM?

Au hawa viongozi wa CHADEMA wanajua kabisa CCM hawawezi kuishinda, wameamua kugawana mazuri ya nchi tu huku wakiwapiga wananchi magirini tu?

Mchango ni wa KKKT si wa Mbowe. Mbowe ni kiongozi tu wa harambee. Na waliochangia ni Wendi sana.
 
Mwenyekiti wa chama cha siasa kaacha kujenga ofisi ya chama ya hadhi kitaifa, kaenda kujenga kanisa lake kwao.

Mpaka hapo hata kama hujui kusoma, hiyo picha tu unatakiwa kuielewa.

Hivi kanisa la KKKT kajenga Mbowe?. Msilazimishe uongo.
 
Huwa wacheka sana nikimuona mtu anasema mbowe ni kiongozi wao [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hivi unakubali vipi kuongozwa na mtu mpumbavu na mpuuzi kama Dj mbowe[emoji53][emoji53][emoji53][emoji53] ngoja tu ninyamaze .

Ukiona mtu anakimbilia matusi Kama wewe huyo ndio mpumbavu.
 
Sijui kwanini wengi wanalalamika Mbowe kupewa na Samia hizo pesa kwaajili ya mchango wa kanisa.

Tatizo ni ile mindset ya siasa za kukunjana mashati ndio bado naiona vichwani mwa wengi, ajabu imefikia hatua kuamini hakuna jema lolote linaloweza kufanywa kati ya wanasiasa wa pande hizi mbili, huu ni ujinga ambao ni lazima ufutwe vichwani.

Hawa wanasiasa nao ni wanadamu, wana hisia za kibinadamu, hivyo msitarajie waishi kama wanyama mbugani kila wakati kuwindana, vyema mkumbuke, hata wanyama nao kuna wakati simba akiwa ameshiba humuona swala na kumuacha aende zake.

Swali la Samia alizipata wapi zile pesa, hilo mimi jibu sina, lakini kama alikuwa nazo na akaamua kutoa, ndio ameshatoa, uchoyo nao sio sifa, ndio maana wakasema kutoa ni moyo..

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
................ Magufuli aliharibu watu na propaganda za chuki!
 
Mchango ni wa KKKT si wa Mbowe. Mbowe ni kiongozi tu wa harambee. Na waliochangia ni Wendi sana.
Kitu cha kwanza kabisa, rais hatakiwi kuchangia shughuli za dini. Hili linaharibu Separation of Church and State.

Kitu cha pili, kila mtu mwenye kanisa lake akitaka rais achangie shilingi milioni 150 rais hataweza. Rais anajiwekea mazingira ya kuonekana anapendelea sehemu fulani kisiasa.

Kitu cha tatu, denokrasia si tu inatakiwa ifanyike, bali pia inatakuwa kuonekana kuwa imefanyika. Hapa kuna muonekano wa kumuhonga Mbowe. Kqma mchango ninwa KKKT kwa nini Samia hakuchangia Uyole kaenda kuchangia kanisa la kwa Mbowe?

Kitu cha nne, Samia hajachaguliwa kujenga makanisa. Hili halimo katika ilani ya CCM. Katika nchi ambayo haifuati dini, haya ni matumizi mabaya ya pesa za wananchi. Waacheni waumini wachangishane wenyewe makanisani.

Kitu cha tano, Mbowe anajiwekea mazingira ya kutoweza kumkemea Samia inavyotakiwa. Utamkemea vipi Boss Lady anayekufadhili mpaka kwenye kujenga kanisa?

Kwa sasa niishie hapa tu.
 
Hivi kanisa la KKKT kajenga Mbowe?. Msilazimishe uongo.
Unaelewa Separation of Church and State ni nini?

Au unabisha kienyejienyeji tu?

Ni hivi, katika nchi secular kama yetu, rais kuchangia ujenzi wa kanisa lolote tayari ni makosa.

Mbowe kumualika rais kuchangia ujenzi wa kanisa kwao ni makosa zaidi, kwa rais na kwa Mbowe.

Nyerere alikuwa Mkatoliki kindakindaki, yule wa kwenda kanisani kila siku St. Peter's pale. Lakini hakufanya ujinga huu. Alielewa Separation of Church and State ni nini.

Umeelewa somo hilo?
 
Sasa akiwatangazia maandamano mnasusa mnataka Nini Sasa? Nyie wenyewe mko mguu ndani mguu nje ni Bora ashughurike na issue zake tu mana kuwatatea watanzania ni sawa na kunyinyinga mwenyewe. Mijitu haijielewi kabisa. Mnataka wengine wanitoe kafala wakati nyie waoga kutetea maslahi yenu. Angalia alienda jela kwa kusingiziwa eti ni gaidi ni nani mtanzania alienda barabarani kuandamana. Lisu alishindiliwa lisasi 32 na jpm ni nani alisimama nayewalau kupinga zaidi ya familia yake kuteseka na tena mkamkejeli eti ameenda ubeligiji kiolewa na mabwana zake. Kila mtu ashuke hamsini zake ebo!
👏👏👏
 
Hii hoja naona watu wanapuyanga tu...

Yaani hatujui jinsi shughuli za uchangishaji zinavyofanyika??
 
Back
Top Bottom