Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Mimi nadhani anachokifanya Mbowe ni kumhakikishia kuwa kuna watu wanamfuatilia kwa makini matendo yake na asi wa take for granted. Kwa upande mwingine msimamo na matamshi ya Mbowe yanamjengea legitimacy katika chama chake kama mrithi wa JPM. Kwa CCM wengi adui namba moja ni Mbowe na angeonyesha kuwa anamkubali kwa aina yeyote Mheshimiwa Rais wetu ungewafanya wamtilie mashaka, kwa maneno mengine ingekuwa ndio busy la kifo kwake. Wapambe wako wengi ( Zitto n.k.) Mbowe hahitajiki kujiunga nao. Huu msimamo unawajenga wote wawili, Mbowe kama mpinzani asiyetetereka na Mheshimiwa Rais kuwa yeye ni mrithi sahihi wa Mwendazake...Mbowe anatakiwa kuuma na kupuliza.
..kwa maoni haya naona kama ameuma bila kupuliza.
..Kuna wana-ccm ambao wanapinga azma ya Rais Samia Suluhu kuboresha mazingira ya kisiasa nchini.
..Ni vizuri Mh.Mbowe na viongozi wa CDM wasizungumze kwa namna ambayo inamvunja moyo Rais Samia ktk kuleta maridhiano ya kisiasa nchini.
..Kwa kifupi sijayapenda maoni ya Mh.Mbowe.
Amandla...