Sijajua Mbowe na Chadema wanatumia akili gani kwani wanapenda siasa nyepesi nyepesi sana, maana baada ya kufariki Magufuli walimchukulia Mama kama Bawacha hivi hawa wazima kweli, kuanzia yule wa Ubeligiji hivyo hivyo. Haya mambo ya kusubiri embe chini ya msufi mtakaa sana, jengeni taasisi hata Lowassa kipenzi chenu aliwashauri hilo.
Nimeshangaa Mbowe anataka kumtenganisha Mama na Magufuli na Mama na CCM hivi kwa akili hizi ninyi wa mtandaoni kwanini msitoe ushauri kwa mwenyekiti kuwa Yanga ni Yanga na Simba ni Simba.
Mimi ngoja nitumbue jipu, Mzee Mbowe mapumziko yako kule Segerea hasa wakati wa sikukuu kama Iddi, Pasaka na Krisimas bado yanaendelea ndiyo kama yanaanza wale wapambe waliokuwa wanamuelekeza Magu wapo hawajafa tena wanahasira.