Freeman Mbowe: Rais Samia Suluhu anateswa na kivuli cha Magufuli

Freeman Mbowe: Rais Samia Suluhu anateswa na kivuli cha Magufuli

..Mbowe anatakiwa kuuma na kupuliza.

..kwa maoni haya naona kama ameuma bila kupuliza.

..Kuna wana-ccm ambao wanapinga azma ya Rais Samia Suluhu kuboresha mazingira ya kisiasa nchini.

..Ni vizuri Mh.Mbowe na viongozi wa CDM wasizungumze kwa namna ambayo inamvunja moyo Rais Samia ktk kuleta maridhiano ya kisiasa nchini.

..Kwa kifupi sijayapenda maoni ya Mh.Mbowe.
Mimi ninachojiuliza Mbowe alitaka Samia afanye nini ili arizike? Avunje bunge au?
 
Ni dhahiri Jamii za kiafrika na Duniani kote zinawachukulia Wanawake kuwa weak,na ukweli wenyewe ndio huo always wanawake ni weak mbele ya Wanaume lakini kama kiongozi kulisemea Mara kwa Mara Opposite linakufanya uwe weak zaidi.
 
Sasa pamoja na unyama ule uliotendwa kulikuwa na haja gani ya mama kujitangaza kwamba yeye ni sehemu ya unyama ule , hawa watu walipofikia kwenye nchi hii haiwezekani tena kuwabembeleza , tuzungumze bila kumung'unya maneno
Kwahiyo wewe ulitaka Samia afanyeje?
 
Hivi kwa akili ya kawaida mwenzetu unaona kulikuwa na uchaguzi 2020...!!?
Ndugu toka mwaka 2000 mnadai tume huru lakini kila uchaguzi mnashiriki kama unaona hakuna uchaguzi why mlikubali kushiriki? Mwaka 2015 CUF Zanzibar waligoma kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar wale ndo walifanya kile ambacho kila mtu aliona wana haki hata ya kutoutambua Uchaguzi wa marudio lakini nyinyi mmeshiriki kuanzia kampeni mpk uchaguzi matokeo mnakataa huoni ni sawa na mwanamke ambae anasema hataki huku anavua nguo??
 
Sa100 na Magufuli ningumu kuwatenganisha kwa haraka hivyo CCM na Sa100 kuwatenganisha ni kwamba atakuwa na status kama ya kina Mdee n wenzake
.......chamsingi tumwache bimdashi kwanza mwelekeo wake baada ya miezi 6,kwa hali ilivyo ni ngumu bimdashi kukurupuka tu na kumdis Jeipiemu.....nadhani atakuwa anabadirika na kuweka mambo mukide mdogomdogo.

Mbowe angetulia kwanza kidogo, Ila ndugu mwenyekiti bado kamati haijatoa taarifa kwa mama Astrazeneca badobado
 
Naona Bavicha wameshangilia sana kusikia rais Samia amepanga kukutana na viongozi wa kisiasa nchini bila kujua kuwa hata hayati rais Magufuli alikutana na viongozi wa kisiasa akina Seif, Lipumba ,Mbatia ,Nk.

Lakini hata rais Samia akikutana nao anataka wajadili jinsi ya kufanya siasa zenye tija kwa nchi.

Maana yake baada ya kukutana hatutarajii kuwaona akina Lisu wakiponda Atcl, Sgr, bwawa la Nyerere kuwa ni miradi ya hovyo badala yake wataanza kusema hiyo ni miradi ya watanzania.

Lakini kwa akili zao wanahisi mama ataenda kuwaruhusu kufanya maandamano kila siku.!!!
 
Ndugu toka mwaka 2000 mnadai tume huru lakini kila uchaguzi mnashiriki kama unaona hakuna uchaguzi why mlikubali kushiriki? Mwaka 2015 CUF Zanzibar waligoma kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar wale ndo walifanya kile ambacho kila mtu aliona wana haki hata ya kutoutambua Uchaguzi wa marudio lakini nyinyi mmeshiriki kuanzia kampeni mpk uchaguzi matokeo mnakataa huoni ni sawa na mwanamke ambae anasema hataki huku anavua nguo??
Mkuu, mimi siyo part ya hao unsowafikiria. Mi ni dependent person... Just sharing my thoughts.
 
Sasa Mkuu ikiwa Mama anasema anafuata nyayo za Magufuli aliyekimbiza wawekezaji lakini wakati huohuo anataka kurudisha imani ya wawekezaje wewe unaelewa nini ?
Sasa Mkuu wewe za kuambiwa si unachanganya na zako? Wewe angalia anafanya nini, kama unaona kuna mwelekeo mzuri mpe credit kisha tuone tunaendaje, amerudia kuwa atachukua mazuri atayaendeleza lakini unaona kabisa muelekeo masuala ya Covid, uwekezaji, diplomasia, demokrasia n.k Mambo ya task force nk alishakataa waziwazi, na ndio maana kwa kuona hilo Mbowe akatoa malalamiko yake na kuomba kuonana naye. Nini Mkuu hujaelewa, cha msingi tumuombee kwa sababu hata huko ndani ya CCM hasa lile genge halifurashwi,
 
Naona Bavicha wameshangilia sana kusikia rais Samia amepanga kukutana na viongozi wa kisiasa nchini bila kujua kuwa hata hayati rais Magufuli alikutana na viongozi wa kisiasa akina Seif, Lipumba ,Mbatia ,Nk.

Lakini hata rais Samia akikutana nao anataka wajadili jinsi ya kufanya siasa zenye tija kwa nchi.

Maana yake baada ya kukutana hatutarajii kuwaona akina Lisu wakiponda Atcl, Sgr, bwawa la Nyerere kuwa ni miradi ya hovyo badala yake wataanza kusema hiyo ni miradi ya watanzania.

Lakini kwa akili zao wanahisi mama ataenda kuwaruhusu kufanya maandamano kila siku.!!!
Dj kwisha habari
Screenshot_20210422-225234_WhatsApp.jpg
 
Back
Top Bottom