Freeman Mbowe: Rais Samia Suluhu anateswa na kivuli cha Magufuli

Freeman Mbowe: Rais Samia Suluhu anateswa na kivuli cha Magufuli

Mbowe analalamika kwamba Samia kwenye hotuba yake hajajitofautisha na Magufuli, mimi najiuliza Mbowe alitaka Samia afanye nini? Aseme mimi najitoa ccm nahamia chadema au?....
Yani katika wapuuzi wewe ndiye kiongozi wao nahisi hata mama yako akisoma uzi wako atalaani siku aliyekuzaa
 
Labda atabadilika baada ya miezi michache ya kuwepo Ikulu lakini kwa mwendo huu matumaini makubwa niliyokuwa nayo kwake ya kuongoza nchi kwa kuheshimu Katiba, haki, usawa na sheria za nchi yamefifia.

Sioni dalili ya kupata katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi kabla ya 2025.
Kwani asingeyasema hayo Mama yetu jamani angepungukiwa nini? Kauli zake kwa kweli zinakinzana na malengo / maono yake —hazijengi upya nchi iliyotoka kwenye dhoruba kali miaka mitano iliyopita (mfano kuvutia hao wawekezaji na kadhalika); sana sana ni kutia watu hofu tu kuwa nchi haina jipya lolote. Naona kama na yeye anapenda kupigiwa makofi makofi.!
 
Naona umekimbia kulinda kaburi la dhalimu saa hii unatapika tu uzalendo uchwara hapa. Nilitarajia utaomba kuzikwa kaburi moja na yule ibilisi, kumbe umeacha aende mwenyewe.
[emoji23][emoji23][emoji23]Hivi mpaka sasa hivi mnapigania kipi?

Naona mnashangilia sana kufa kwa Magufuli, vipi na ccm na mifumo yake nayo imekufa?

Msipojielewa mtatepeta sana tu
 
Mbowe ameshangaza sana!
Hata akikutana anataka wajadili jinsi ya kufanya siasa zenye tija kwa nchi.

Maana yake baada ya kukutana hatutarajii kuwaona akina Lisu wakiponda ATCL, SGR, bwawa la Nyerere kuwa ni miradi ya hovyo badala yake wataanza kusema hiyo ni miradi ya Watanzania.

Kwa akili zao wanahisi mama ataenda kuwaruhusu kufanya maandamano kila siku.
 
Kauli za maza ni kinyume na matendo, ni kama marehemu dikiteta magufuli alipenda kusema maendeleo hayana vyama lkn akipita majimbo ya kina bwege na wapinzani wengine, anatukana na kufokea wananchi kuwa hawezi kuwaletea maendeleo Sababu walikosea kuchagua.
Mbona Dj mbowe analalamika sasa?
 
Sasa pamoja na unyama ule uliotendwa kulikuwa na haja gani ya mama kujitangaza kwamba yeye ni sehemu ya unyama ule , hawa watu walipofikia kwenye nchi hii haiwezekani tena kuwabembeleza , tuzungumze bila kumung'unya maneno
Tuvumilie kwanza, tukumbuke kwamba ccm ni ile ile, SSH ni wale wale, Kwa hiyo akiongea pale lazima azungumze lugha yao, hata kama ana nia njema ya kuboresha demokrasia! Au tuseme tu ukweli, Mazaa anaweza Vipi fasta fasta aseme, “mwendazake alikua deshi deshi, sipo naye tena, nipo na wapinzani!” Hata Sisi Tutashangaa!

Anaenda nao mdo mdo, labda tarehe 30 akisha kabidhiwa mikoba ya chama cha mboga mboga, tutaanza kuona makali yake!

Kwa sasa, ni kweli, Mbowe yupo sahihi, give it time, muda utaongea! Na pia kugomelea alichosema ni sawa pia, huwezi kuacha kukaba eti kisa ni mechi ya kirafiki!
 
Mbowe analalamika kwamba Samia kwenye hotuba yake hajajitofautisha na Magufuli, mimi najiuliza Mbowe alitaka Samia afanye nini? Aseme mimi najitoa ccm nahamia chadema au?...

sku wakija kujielewa nadhan ndo itakua sku nyumbu wanapata akili pia
 
..Mbowe anatakiwa kuuma na kupuliza.

..kwa maoni haya naona kama ameuma bila kupuliza...
Hata mimi nilitarajia Mbowe amsome Mama katikati ya mistari, aone mkakati unaochezwa, asiwe na papara ya kuchapisha maoni hadi wapinzani watakapopata fursa ya kukutana ana kwa ana na Rais.

Certainly, Samia Suluhu Hassan hawezi kuwa kama JPM. Lakini kuna kazi ngumu ya kuondosha sumu iliyokwishasambazwa katika uongozi na jamii kwa ujumla.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Hivi mpaka sasa hivi mnapigania kipi?

Naona mnashangilia sana kufa kwa Magufuli, vipi na ccm na mifumo yake nayo imekufa?

Msipojielewa mtatepeta sana tu

Afe dhalimu tusishangilie kivipi? Ulitaka tupiganie kipi?
 
Back
Top Bottom