Freeman Mbowe: Rais Samia Suluhu anateswa na kivuli cha Magufuli

Freeman Mbowe: Rais Samia Suluhu anateswa na kivuli cha Magufuli

Mbowe analalamika kwamba Samia kwenye hotuba yake hajajitofautisha na Magufuli, mimi najiuliza Mbowe alitaka Samia afanye nini? Aseme mimi najitoa ccm nahamia chadema au?

Wafuasi wake humu wanashangilia na kusema ccm watakoma,. Naomba kuuliza Samia anaetawala kupitia ccm amefanya nini au atafanya nini cha kuwakomesha ccm na kuwafurahisha chadema mpaka wana chekelea hivi?

Mimi naomba kuuliza tume huru tayari? Katiba tayari? Maana hayo ndio huwa wanasema yanawanyima ushindi! Au ile mifumo mibovu wanayosemaga kaondoka nayo Magufuli?

Niwakumbushe tu, aliekufa ni Magufuli ila ccm na mifumo yake iko vile vile tena safari hii itaimarika zaidi.
Msije sema hatukuwaambia.
 
Hivi hata angenyamaza tu ingekuwaje , unamuungaje mkono mtu wa namna ile hadharani ?
Sisi ambao tunatumia hii mitandao ndo tunafahamu hivyo,
Majority ambao kimsingi ndo watanzania wa kawaida hawawezi kuelewa mizaniavya ubaya wa kiasi hicho unaouelezea kwa Mwendazake JPM
 
Kwani kosa la mama Samia ni lipi, kuna vitu ambavyo Maghufuli alizingua mama yupo tayar kuvirekebisha , eg democracy , Uhuru wa habari , uwekezaji na mengine mengi , Yale ya mhimu ataendelea nayo au mnataka awe anamtukana JPM kwenye majukwaa , hyo ni impossible wakuu
 
Kauli za maza ni kinyume na matendo, ni kama marehemu dikiteta magufuli alipenda kusema maendeleo hayana vyama lkn akipita majimbo ya kina bwege na wapinzani wengine, anatukana na kufokea wananchi kuwa hawezi kuwaletea maendeleo Sababu walikosea kuchagua.
 
Hajitambui bado anajikanyaga kanyaga.

Kwani asingeyasema hayo Mama yetu jamani angepungukiwa nini? Kauli zake kwa kweli zinakinzana na malengo / maono yake —hazijengi upya nchi iliyotoka kwenye dhoruba kali miaka mitano iliyopita (mfano kuvutia hao wawekezaji na kadhalika); sana sana ni kutia watu hofu tu kuwa nchi haina jipya lolote. Naona kama na yeye anapenda kupigiwa makofi makofi.!
 
Vipi kuhusu CUF, TLP, CHAUMA, NCCR, TADEA, UDP...hao hawajachanganyikiwa?
 
Nyerere ndio anatakiwa kutukanwa humu
Yeye ndio aliinda katiba mbovu akijua kuwa tutakuja kupata dikteta kama mwendazake
Yani watu wanamsahau huyu mzee nyerere
 
Mbowe analalamika kwamba Samia kwenye hotuba yake hajajitofautisha na Magufuli, mimi najiuliza Mbowe alitaka Samia afanye nini? Aseme mimi najitoa ccm nahamia chadema au?...
Naona umekimbia kulinda kaburi la dhalimu saa hii unatapika tu uzalendo uchwara hapa. Nilitarajia utaomba kuzikwa kaburi moja na yule ibilisi, kumbe umeacha aende mwenyewe.
 
Back
Top Bottom