Freeman Mbowe: TRA walinidai Kodi Bilioni 2, Wakafunga akaunti zangu zote za biashara mpaka binafsi, Wakachukua hela

Freeman Mbowe: TRA walinidai Kodi Bilioni 2, Wakafunga akaunti zangu zote za biashara mpaka binafsi, Wakachukua hela

Aisee, Na ile bustani ya Mbowe ilifyekwa mazao yote, Ukumbi wa burudani wa Bilcana nao ukavunjwa, ukaporwa na ubunge wako. Lakini ulikuwa mvumilivu sana wala hukulalamika mahali popote. Pole mkuu Mbowe, yote hayo walitaka ukaunge juhudi za mtu hatari.
Unahaki ya kususa hata kwenda msibani Chato
Nyie watu walikuwa na uchungu nyie,mi nshamsamehe kwakweli
 
Halafu Mbowe anataja kua Hayati Magufuli alikua na upendeleo wa kindugu, neportism, anaweza kutupatia ushahidi kua kulikua na upendeleo huu na huu wa kindugu wakati wa Magufuli?

Tupate ushahidi wa ndugu zake na Magufuli ambao aliwapendelea na hawakua na sufa kwenye nafasi za kiutumishi.

Hii kampeni ya ukabila inapigiwa chapuo sana na makabila ya kaskazini. Wanajitahidi kutaka kufukia tabia yao ya ukabila nchi hii. Mfano, Kimei amejaza wachaga CRDB.
Tukichimbua tu Mayanga Construction utarudi pale mlipozika ukalie upya.
 
Sikiliza maelezo yake mwenyewe anasema baada ya kufungiwa ndio akaamua kwenda Dubai kuanzisha biashara, hakusema kama alikua na biashara huko.
Amesema kuangalia fursa..kuwa makini kijana..tutakuchapa viboko na wewe kabla hatujalichapa la magu
 
Sasa naamini kuna kampeni chafu ya kumchafua JPM!
Kama ni toka 2018 alishindwa nini kuitumia ktk siasa za uchaguzi kama ilivyo kwa wanasiasa wetu kutafuta sympath!!
Kuna watu wanasema; oil chafu haichafuliwi na huwezi kusugua mkaa ukitegemea kuubadilisha rangi!!
 
Mo siku akifunguka jinsi alivyolazimishwa kuhamisha hela siku alipotekwa ndipo mtajua kuwa hamjui. Nina ushahidi wa wazi wazi jinsi Jiwe alivyopora uwekezaji wa watu kwa kuwatisha. Yani ulikuwa unawekwa kwenye chumba usiku wa manane kazi ilikuwa moja kusaini nyaraka ama ukutane na chuma.

Kuna mmoja alisainishwa nyaraka usiku wa manane ili makampuni yake yataifishwe na hakuwa na jinsi maana TAKUKURU walikuwa wanamtisha kuwa akikaidi hatorudi tena kwao.

Yani kikosi kazi cha Jiwe kilikuwa kinaandaa nyaraka then unachukuliwa unapelekwa juu ghorofani na unakaa nao wewe peke yako! Hata mwanasheria wako haruhusiwi kuwepo.


Ebwanaeee Nenda zako mzee!
 
Nashukuru Mungu sasa nipo free kutokana na Mambo ya Siasa walichonitenda kina Mdee,EL n.k inatosha...Am doing my own business nw!!
 
Hii ya kumshambulia Hayati iishe, naona watu wangekaa kimya tu Sababu Mungu anajua zaidi kashafanya yake Watu mpate amani, sasa yanini lawama tena?
Yaliyopita, yaliyopo na yajayo husemwa kwa pamoja Kama unataka mstakabali mwema
 
watanzania hatuna ukatili wa kiwango hiki. uraia wa huyu mtu uchunguzwe
Kati ya hazina Mungu alizotubariki nazo huwezi ukaacha kumtaja hyo mwamba na mzalendo wa kweli aliepo kwenye hyo avatar yako, badala ya kutumia vichwa kama hvi vitusaidie kumove on wapumbavu wanaweka wajinga kwenye madaraka.
 
Kumuamini Mbowe ni sambamba kumiliki cheti cha MIREMBE.

Sijahi kuona sehemu yoyote amekanusha tuhuma za kujikopesha pesa za chama.
 
Kama hakufata sheria..alitaka iweje!!! Kama alifata aende mahakamani..

Ila nawashangaa wengi.. maneno mengi kama vile uongozi wote umebadilika ukaja mpya kutoka sijui safari ipi.. na sheria za nchi zimekutwa..

Waendelee tu kuongea...........
Mbona wamemrudishia hela zake Kama hakufuata Sheria?
Pia mbona hamkupeleka mahakamani kwa kuwa na dirty money?
Ni sheria ipi ilitumika kupora hela za Mbowe?
 
Account zimefungwa, ulitegemea akae tu amsubiri JPM?
Kweli wewe ni mnyonge. Ukidondosha hela, unalala njaa, kuzisubiri mpaka uzipate hizo hela ndiyo ukale?
Wamefunga account na siyo hela. Unaweza kufungua account lenye jina la mwanao na ukafanya miamala km kawaida.
Mkuu kuna imani potofu kwamba wachaga ni wezi, eti mafisadi, Lakini ukweli ni kwenye mambo kama haya! Unajaribu kumzuia Mbowe kwenye mambo madogo hayo, kumbe anapeta tu! Kumbana Mtu mwenye akili zake, atatumia akili hizo kutoka kwa njia nyingine!
 
Mbowe amekosa Utu, hivi inawezekanaje leo hii anamkashifu na kumshambulia mtu aliye kufa?!!! ili iweje sasa?

watanzania walio wengi waneumia sana kwa kuondokewa na Huyo unaye mkashifu leo hii.
huu sio uungwana
Endelea kusikitika wewe ulieumia na kifo chake,acha watu watoe na moyoni,kama huko ni kumshambulia basi acha ashambuliwe maana ndio alitaka akumbukwe hivyo.
 
Mbowe ni muongo.

Mbowe anasema alifungiwa akaunti zote lakini akaamua kwenda kufanya Biashara Dubai, hizo hela za kwenda kuanzisha biashara Dubai zilikua akaunti gani kama akaunti zake zote TRA walifungia?
Ndugu nikusaidie kuelewa, wafanyabishara wote wakubwa duniani hutunza pesa zao kwenye nchi mbalimbali. Hawaweki kwenye nchi moja

Sent from my vivo 1611 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom