Freeman Mbowe: TRA walinidai Kodi Bilioni 2, Wakafunga akaunti zangu zote za biashara mpaka binafsi, Wakachukua hela

Freeman Mbowe: TRA walinidai Kodi Bilioni 2, Wakafunga akaunti zangu zote za biashara mpaka binafsi, Wakachukua hela

Mo siku akifunguka jinsi alivyolazimishwa kuhamisha hela siku alipotekwa ndipo mtajua kuwa hamjui. Nina ushahidi wa wazi wazi jinsi Jiwe alivyopora uwekezaji wa watu kwa kuwatisha. Yani ulikuwa unawekwa kwenye chumba usiku wa manane kazi ilikuwa moja kusaini nyaraka ama ukutane na chuma.

Kuna mmoja alisainishwa nyaraka usiku wa manane ili makampuni yake yataifishwe na hakuwa na jinsi maana TAKUKURU walikuwa wanamtisha kuwa akikaidi hatorudi tena kwao.

Yani kikosi kazi cha Jiwe kilikuwa kinaandaa nyaraka then unachukuliwa unapelekwa juu ghorofani na unakaa nao wewe peke yako! Hata mwanasheria wako haruhusiwi kuwepo.


Ebwanaeee Nenda zako mzee!
Eti una ushahidi!

Unashindwaje kuweka hapa? Mnafiki mkubwa wewe
 
Y
Ningeyajua mapema haya mambo. Wala nisingemlilia ile siku ya kuaga mwili wa katili. Natamani kudai fidia ya machozi yangu yaliyotoka isivyostahiki.
yalikua matumizi mabaya ya machozi, unatakiwa kushitakiwa na kupigwa faini kwa matumizi mabaya ya rasilimali!
 
Kwanini hakusema kipindi yupo uko nje anaposema alienda kuwekeza badala yake anasema sasa ivi...au kipindi kaandika tanzia uyo mbowe anajikomba kwa mama samia sawa tumeshakusikia.Waache wafu wazikane wenyewe...
 
Lakini mkuu nashangaa ilikuwaje akageuka kuwa mtu wa ajabu hvi baada ya kuupata urais?? Before kipindi akiwa waziri alionekana ni mtu safi, smart mzalendo kweli kweli.
Alikuwa mpuuzi na mpenda sifa tangu mwanzo. Lawama zote kwa Kikwete maana alimjua in and out na yeye ndo alikuwa rais na Mwenyekiti wa chama. Angeweza kumthibiti Mkapa.
 
Aagh kumbe alikua anadaiwa kodi??

Sasa keshalipa au kuongea huku anataka asamehewe au anavyotumbia sisi ndio hao TRA au??
 
Kuna wakati mwingine TRA wanakuwa kama vibaka,mnajua director yupo mahabusu, mnapeleka tax demand notice, ili ashindwe kujibu mmnyanganye mali zake.
 
Kama hakufata sheria..alitaka iweje!!! Kama alifata aende mahakamani..

Ila nawashangaa wengi.. maneno mengi kama vile uongozi wote umebadilika ukaja mpya kutoka sijui safari ipi.. na sheria za nchi zimekutwa..

Waendelee tu kuongea...........
Wakati wa jiwe majaji walikuwa wanasikiliza jiwe anataka nini achaga ujinga Basi kidogo
 
Magufuli alikuwa mtu mbaya sana.
Lile kaburi lake linapaswa kupigwa pingu, kutandikwa viboko au kuwa sehemu ya watu kujisaidia haja ndogo.
Hafai kabisa kukumbukwa kwa mema yoyote.
Hizi sasa ni dhihaka na fedheha kwa mtu aliye na Umri wa kukuzaa, hata kama ilivyofanya ndivyo sivyo mpaka mauti kumfika.
Ndio, lakini kwanini iwe sasa, Je ndio kuanza upya huko wanavyosema watu, au ni gear nyingine wanazitumia watu /kakikundi fulani kupitia madhaifu ya aliyekuwepo ili nao wawe sehemu ya wahanga!!?
Ziko wapi justification za Mh. Mbowe (ushaidi usio tia shaka) ili iwe ni mfano na wengine waliofanyiwa hivyo kujitokeza kulalamika?
Kejeli, matusi, dhihaka au kujifanya jeuri wa kutumia maneno yasiyofaa kitamaduni kunapindisha ukweli wa kujadili hoja kwa kina.
Tumieni vyombo vulivyopo kudai haki zetu kama zipo, kutukanana na kudhalilishana sio suluhisho la matatizo hasa kwenye kulaumu asiyekuwepo.
Tatizo letu ni kum-attack mtu mmoja asiye hai wakati waliofanya hayo wapo.
 
Sikuwahi kufikiria huyu Mbowe hii jeuri ya kukataa kuunga mkono juhudi anaitoa wapi??

Leo nimepata jibu, huyu mwamba ana hela nyingi ndio maana yupo stable sana.



Salamu kwa disii wa hai.
 
Mbowe mbona haya unayasema sasa?

Maana kama mti mbichi ulikuwa wafanyiwa hayo, je mti mkavu ambao no wafuasi wa chama chako je?
Uzuri tra Wapo, waje wakanushe! Tena ameyasema kwa uchache sana, ishu ya kubomolewa shamba lake hajalisema
 
View attachment 1749358

Nilifungiwa akaunti zote za bank za kampuni yangu. Nikafungiwa akaunti zote za biashara. Hata akaunti yangu binafsi ya mshahara wa ubunge ilifungwa toka mwaka 2018, nikazuiwa kupokea mshahara ambao ni haki yangu kisheria" Mhe.Freeman Mbowe akizungumza na wanahabari.

My Take
Natengua msamaha nilioutoa kwa Magufuli

====
MBOWE: NILITUMIWA MADAI YA KUDAIWA KODI NIKIWA JELA

Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema alitumiwa madai ya kudaiwa kodi ya Tsh. Bilioni 2, kwenye email binafsi akiwa jela ambapo alishindwa kuiona

Barua pepe ya kwanza ilimtaka kupeleka malalamiko ndani ya siku 30 kama hakubaliani nayo, kwa kuwa alikuwa jela hakuweza kuijibu, wakatuma nyingine kusema kuwa kwa kuwa amekaa kimya ameonekana kukubaliana nayo

Alivyotoka jela, akadaiwa kodi ambayo amedai kuwa haikuwa sawa kwa kuwa ili biashara ilipe kodi ya Tsh. Bilioni 2 lazima iwe imetengeneza faida ya Tsh. Bilioni 12 kwa mwaka, na biashara yake ni ndogo isingeweza kutengeneza faida hiyo

Ili Mamlaka ya mapato kuipata kodi hiyo walifungia akaunti zake zote ikiwemo aliyokuwa anapokelea mshahara wa ubunge. Kwa sababu hiyo aliondoka nchini ili kutafuta fursa za kuwekeza nchi nyingine
Huyu marehemu alikuwa kiumbe wa ajabu kiasi hiki!! Ni vigumu sana kuamini mtu mwenye Roho wa Mungu anaweza kufanya ushetani wa kiasi hiki. Basi hiki kifo kilikuwa ni ukombozi kwa wengi walioonewa.

Kumbe masikitiko yangu kwa msiba huu ilikuwa ni kufuru kwa sala za watu wengi ambao wamekuwa wakimlilia Mungu usiku na mchana.

Mungu wetu ambaye hekima yako inazidi mipaka ya fikra zetu, tunaomba uwatazame waja wako waliofanyiwa maonevu mengi na mtawala wao, uwafute machozi yao kwa namna ile ifaayo. Nao waliondolewa uhai wao kwa matakwa ya mtawala wao huyu dhalimu, tunaomba uwape cheo cha juu cha utakatifu ili waizunguke meza yako wakikusifu usiku na mchana.

Tunajua, hakuwa pekee yake, bado ina mikono yake aliyokuwa akiitumia kutekeleza ushetani kwa watu wako. Hawa wakatwe mikono yao, wakapate majuto yashindayo uvumilivu, wakugeukie wewe wakiujutia kwa machozi ya damu uovu wao.
 
Back
Top Bottom