Fremu zinazojengwa hapa eneo la Jeshi Lugalo hadi njiapanda ya Kawe zitapangishwa raia au kwa askari tu?

Fremu zinazojengwa hapa eneo la Jeshi Lugalo hadi njiapanda ya Kawe zitapangishwa raia au kwa askari tu?

Kama tu Akili za Kujenga vyema hizo Fremu ( mpaka zingine zimepinda, zingine fupi na zingine zimeshaweka Ufa ) wamekosa je, unadhani Akili za Kupambana na Majeshi HATARI na Mahiri kwa sasa Afrika Mashariki kama ya Rwanda na Uganda watakuwa nayo na wataweza?
Muda wa kupambana na Rwanda sisi tunautoa wapi? Hiyo kazi tutawaachia ndugu zetu "Waha" wa Kigoma.

Watawanyoosha vizuri tu, wakati mikoa mingine inaendelea na shughuli za ujenzi wa taifa. Waha wakichelewa, tunapeleka wakurya kadhaa tu!

Waambie wasije wakajichanganya, maana zile pisi zao tunazitamani sana. Wasitupatie sababu!

Haya njoo umwage povu ndugu Popoma!
 
Kuna mtu aliwahi ni introduce kwenye huo mchongo! Ilikuwa ni lazma utafte mwanajeshi mmoja uingie nae mkataba wa ujenzi ujenge fremu zako ila zinakuwa chini yake kimkataba kisha utafanyia biashara kibingwa. Nilichomoaga hio nikaona ufala
Ulifanya uamuzi wa busara sana, kuna mdau alichukua mkopo akajenga kituo cha mafuta pale Gongo la Mboto jeshini, alikubali mchongo kama wako huo, wajeda wakamchenjia akapigwa pini na benki wanamdai wakati kituo kimefungwa, ni noma sana aisee!!

Jamaa alibugi stepu sana.
 
Niliposikia tu sababu ya kupelekea Ujenzi huo jinsi ilivyo ya Kipuuzi ( kutokana na Unyeti wa hiyo Kambi ) kwa Tanzania nzima ni kwamba nchi yetu sasa iko Uchi kabisa kwa Maadui na ipo Siku Tanzania itakuwa Mali ya Taifa lingine.
Tulia uliza upewe maelekezo Jeshi halijawahi kukosea
 
Kama tu Akili za Kujenga vyema hizo Fremu ( mpaka zingine zimepinda, zingine fupi na zingine zimeshaweka Ufa ) wamekosa je, unadhani Akili za Kupambana na Majeshi HATARI na Mahiri kwa sasa Afrika Mashariki kama ya Rwanda na Uganda watakuwa nayo na wataweza?
Hatuwezi kamwe kupigana na Dada zetu wa Rwanda na Uganda tunaheshiamna sana ndio maana wanakuja kwenyw mafunzo pale TMA .

Ni dada zetu wa Damu
 
Niliposikia tu sababu ya kupelekea Ujenzi huo jinsi ilivyo ya Kipuuzi ( kutokana na Unyeti wa hiyo Kambi ) kwa Tanzania nzima ni kwamba nchi yetu sasa iko Uchi kabisa kwa Maadui na ipo Siku Tanzania itakuwa Mali ya Taifa lingine.
Kifupi ni mradi ulioanzishwa kwa kukurupuka bila kufuata misingi ya 'Project Management' na hakukufanyika 'feasibility study', 'risk management' wala 'Social Impact Assessment'.
 
Niliposikia tu sababu ya kupelekea Ujenzi huo jinsi ilivyo ya Kipuuzi ( kutokana na Unyeti wa hiyo Kambi ) kwa Tanzania nzima ni kwamba nchi yetu sasa iko Uchi kabisa kwa Maadui na ipo Siku Tanzania itakuwa Mali ya Taifa lingine.
Mkuu hakuna neno unaloweza sema zaidi ya hapo. Majeshi yetu yameiingiliwa na kitu gani sijui.

Nani ana shauri huu upuuzi wa maeneo nyeti ya kijeshi kutoa uoto asili Ulikuwa unatumika kama 'camouflage'. Ni vikosi vingi Sasa vya jeshi vinageuza ardhi yao kutumika kama vitega uchumi. Kama kikosi cha 671 SAM HQ, kilichopo Mabibo - Makubuli, kama unatoka Mabibo external Kuelekea Tabata Kisukuru upande wa kulia kuanzia Simba Petrol station mpaka kwa Majinja Depot.

Kuna urefu wa kama 2.5 km kumejengwa mabaa na gereji. Waziri wa ulinzi na CDF angalieni upya uamuzi wenu ni hatari kwa usalama wa taifa letu.
 
Time change,majeshi duniani ni ya kisasa mno, kujenga frem outskirts hakuna tabu yoyote alikradi tu ni akina nani watapangishwa ( we have friendly army but dangerous to nation enemy)

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
Hayo uliyoweka kwenye mabano kwa kiingereza, kiuhalisia ni kinyume chake! Majeshi ya kuua na kutia vilema wananchi wake wenyewe, hasa ccm inapolazimisha kushinda uchaguzi!
 
Hauko 'Security Conscious' hivyo huna unachokijua na tafafhali acha Kunipotezea muda ila kuna Siku Tanzania ikivamiwa kirahisi na Watanzania kuwa Mali ya Nchi nyingine ndiyo mtatuelewa Wenye Akili Kubwa, Maono na Machale ya Kutukuka.
We mdada unajihisi unajua sana kuliko wengine humu
 
Ulifanya uamuzi wa busara sana, kuna mdau alichukua mkopo akajenga kituo cha mafuta pale Gongo la Mboto jeshini, alikubali mchongo kama wako huo, wajeda wakamchenjia akapigwa pini na benki wanamdai wakati kituo kimefungwa, ni noma sana aisee!!

Jamaa alibugi stepu sana.
Dah kweli mzee yani ilikuwa kipindi cha maana sema nilikaza tu for sure!
 
Back
Top Bottom