Friji yangu inawaka na kuzima, tatizo litakuwa nini?

Compressor inaweza kuwa imefeli, sina nia ya kupigia debe kampuni ila fridge za lg na samsung zenye linear compressors hazina matatizo hayo. Nyingi pia huna haja ya kutumia fridge guard.
 
Compressor inaweza kuwa imefeli,sina nia ya kupigia debe kampuni ila fridge za lg na samsung zenye linear compressors hazina matatizo hayo. Nyingi pia huna haja ya kutumia fridge guard.
Kuna fundi aliniambia kuhusu Compressor ila gharama nikaona iko juu, so njia ya mwisho niliyobaki nayo nikubadili hizo compressor
 
Sasa kama ubaridi unapatikana shida ipo wapi
Time range ilinipa shaka, awali haikuwa hivyo. Nimeamua kulizima kabisa nitaliwasha baada ya ubaridi kuisha nione shida ni nini? Nimechukuwa maamuzi haya baada ya kusoma comments kadhaa
 
.. likizima, gusa compressor kwa mkono, kama ina joto kiasi cha kuondoa mkono ndani ya sekunde chini ya 5

1. gesi ndogo
2. capillary tube mbaya
3. compressor yenyewe mbaya
 
La kwangu upande wa Fridge halina ubarid kabisa,ila upande wa Frizer kule juu liko poa kabisa..ni takribani wiki sasa. Kama kuna fundi anisaidie changamoto ni nini.
Lina shida
Tafuta fundi
 
.. likizima, gusa compressor kwa mkono, kama ina joto kiasi cha kuondoa mkono ndani ya sekunde chini ya 5

1. gesi ndogo
2. capillary tube mbaya
3. compressor yenyewe mbaya
Rule out hiyo ya gesi kuwa ndogo, gesi ikiwa kidogo cimpressior halizimi kabisa maana thermostat inakuwa haibani
Capillary tube na compressor upo sahihi
 
Natumia lg iliyo na compressor mwaka wa 5 huu sasa,zipo imara sana
Nakaribia kumaliza 10 years warranty ya compressor.

Linear inverted compressor zinakuja na 10 year warranty
 
Langu ni Hisense
Sina guard
Huko dukani waliniambiaga hayo yana guard ndani kwa ndani.

Niko safe wakuu?
Naliwasha muda karibu wote.. nazima siku ya kulisafisha
Nawee ni mtumiaji wa Hisense?.

Unakuta ni kale kadogooooo hata Dumu la maji ya uhai la Lita sita, haliingiii🤣🤣🤣
 
Compressor inaweza kuwa imefeli,sina nia ya kupigia debe kampuni ila fridge za lg na samsung zenye linear compressors hazina matatizo hayo. Nyingi pia huna haja ya kutumia fridge guard.
Basi tu bei zao zimechangamka ila LG ni brand nyie, sio fridge tu hata tv.
 
Basi tu bei zao zimechangamka ila LG ni brand nyie, sio fridge tu hata tv.
Ukipiga hesabu vizuri ni bora kununua ghali.

Wakati nanunua 2013 nilinunua lg kwa 1.1 mil, brand nyingine zilikuwa kwenye 600000, huu unaenda mwaka wa 10 haijawahi sumbua chochote, na ninzile non frost, mwaka 2016 nikanunua deepfreezer ya kichina, halikuakaa miaka 4 , written off
 
Kweli kabisa.....Bi mkubwa ana friji la LG alinunua 2012, Hadi Leo Haina shida yoyote, naikubali sana hii brand, tatizo bei🤣
 
Kwa wastani wa dk mbili Hilo ni tatizo. Ingekuwa dk 15/30 ingekuwa sawa. Hapo km sio tatizo la friji basi ni low voltage ya umeme unaotumia. Jaribu kuliwasha usiku wa manane watu wakiwa wamelala maana muda huo matumizi ya umeme huwa madogo maana watu wanakuwa wamezima vitu vyao. ukikuta tatizo ni Hilo basi nunua stabilizer. Hapo kesi kwisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…