FT: Barcelona 4-3 Real Madrid | Laliga | Estadio Olimpic Luis Companys | 11.05.2025

FT: Barcelona 4-3 Real Madrid | Laliga | Estadio Olimpic Luis Companys | 11.05.2025

Basi wewe ni shabiki wa madrid maana nyingi ulizoorodhesha hapo ni zile ambazo madrid ndio alishinda, anyway leo barca akishinda basi msimu huu madrid anakuwa kapigwa mara nne mfululizo na barca, jumlisha na ya tano mwanzo wa msimu kwenye mechi yao ya kirafiki
Kama ni suala la mfululizo soma post #159
Kama ni suala la Head-to-Head leo mtafikisha 104 dhidi ya 105
Kama ni suala la biggest win, bado sana mlipigwa 11-1
 
Barca hana UCL toka 2015 Madrid toka 2015 mpaka sasa ana UCL 5 hii ni idadi ya makombe yote ya UCL ya Barca katika historia yake.

Umeanza kushabikia mpira mwaka gani ?
Miaka mingi naangalia soka. Kabla Eric Cantona hajaanza kucheza pale Man U, Ronaldo de Lima hajaanza kucheza Barca,n.k. Sidhani kama tuliangalia pamoja World Cup 1990.

Ukweli ni kwamba timu za serikali janja janga nyingi sana. Hawachelewi kubebwa waleeee.
 
Mbape akitaka arejee kwenye ubora wake na kugombea Ballon Dor itamlazimu ahamie ligi ya EPL, huku kwa wahispaniola kuna vitoto vanapiga mpira hatari mpk vinampoteza.
Amekutana na upepo mbaya kutokea La Masia
 
Muda mchache ujao, El Clasico inapigwa.

Ni Barcelona Vs Real Madrid katika mchezo muhimu wa La liga ambao utatoa picha ya mbio za ubingwa.

Ikumbukwe ni El Clasico ya mwisho kwa Carlo Ancelloti kabla ya ujio wa Xabi Alonso pale Real Madrid.

Ancelloti amefungwa mechi zote alizokutana na Barcelona huku pengo la point likiwa ni tofauti ya alama 4 huku ikibakia michezo minne tu kabla ya mechi ya leo.

Ungana nami kwa live updates…

==================
1’ Real Madrid wanaanza mpira kwa kasi

2’ Mbappe anafanyiwa faulo kwenye box, refa anasema penati

4’ Goaaaaaallllll Mbappe anafunga penati

5’ Barcelona 0-1 Real Madrid

7’ Real Madrid ni kama wanaitaka sana mechi ya leo

10’ Barcelona 0-1 Real Madrid

12’ Barca wameanza kuliandama lango la Real Madrid kama kawaida yao

14’ Mbappe anaweka goli la pili na kufanya ubao usome Barcelona 0-2 Real Madrid

15’ Lamine Yamal yuko chini

19’ Garcia anawapa goli 1 Barcelona

20’ Barcelona 1-2 Real Madrid

23’ Watoto wa Barcelona wamecharuka sasa

25’ Barcelona 1-2 Real Madrid

28’ Real Madrid wamepaki basi mapema sana, mchezo umetawaliwa na Barcelona

29’ Fade Valverde anapata kadi ya njano baada ya kumchezea madhambi Lamine Yamal

31’ Lamine anaisawazishia Barcelona na matokeo ni 2-3

34’ Raphinha anaitanguliza mbe Barcelona huku ubao ukisoma 3-2

36’ Tchouameni anapata kadi ya njano kwa kumchezea madhambi Ferran Torres

40’ Barcelona 3-2 Real Madrid

44’ Barcelona 4-2 Real Madrid
Mfungaji wa goli la nne ni Raphinha

45’ Zinaongezwa dakika 6

45+5’ Mbappe anafunga lakini goli linakataliwa kwakuwa alikuwa offside

HT’ Barcelona 4-2 Real Madrid

2nd half

50’ Asescio wa Real Madrid anapewa kadi ya njano kwa mchezo usiokuwa wa kiungwana kwa Ferran Torres

52’ Lamine Yamal anaaweka goli la 5 lakini inaonekana kwenye build up kulikuwa na offside ya Raphinha

53’ Inago Martinez wa Barcelona anapewa kadi ya njano kwa mchezo usiokuwa wa kiungwana kwa Jude Bellingham

57’ Christensen & Balde wanaingia kuchukua nafasi za Gerrard n& Cubarsi kwa upande wa Barcelona

63’ Barcelona 4-2 Real Madrid
Hapo dk ya 31 umeandikaje hayo matokeo?
 
Mbape akitaka arejee kwenye ubora wake na kugombea Ballon Dor itamlazimu ahamie ligi ya EPL, huku kwa wahispaniola kuna vitoto vanapiga mpira hatari mpk vinampoteza.
Toka 2008 Cristiano kuchukua Ballon d'or ndondokera nyingine imetokea 2025 kwa mtu wa EPl kuchukua hiyo tuzo tena hiyo tuzo imeacha maswali mengi.

Raphina hii ya sasa anachukua.
 
Back
Top Bottom