FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

Ila kweli, unashangaa tunatinga Semi final.
Mweeeeeeh, yaan hatare.
 
Kuna VAR
 

Chama ni tofauti na Tiba. Lini uliona Tiba anafanyiwa Sub mashabiki wanamuakia kocha?
 
Hongera kwa ushindi, na hasa goli zuri ambalo mchoro wake hakuna angeweza kuuchora kabla.

Nafasi ya Simba kufuzu ipo ikiwa itakuwa bora kimbinu kuwazidi hao Wydad Casablanca.

Wydad walianza kuvutavuta na kukamata wachezaji wa Simba. Ile ni ishara gani, kuzidiwa au mbinu za mchezo?

Chama apunguze zaidi mbwembwe, Kuna goli ilikuwa afunge leo.

Makocha na wachezaji watenge muda kurejea hii mechi katika video.

Ule mchezo wa away, wajipange kumiliki zaidi pale kati.

Kasi ya Wydad kule Morocco itakuwa mara dufu, ni kazi ya makocha kubuni mbinu.

Simba irejee video zote za mavurugu ya Morocco, iwe mvua, kelele, tarumbeta nk waone kawaida.

Ule mkakati wa kuitoa Zamaleki 2013 uboreshwe zaidi. Simba ioneshe haijafika hapa kwa kubahatisha.

Hakuna lisilo wezekana na Wala haitakuwa miujiza Simba kuingia nusu fainali.

Kuna watauliza kwa wachezaji gani? Ni hawahawa, mbinu na bidii zaidi Simba wanavuka kibabe.

Mengi yalisha fanywa na Simba huko nyuma, kwanini isiwezekane sasa.
 
Tunashukuru kwa ushindi huu mwembamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…