FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

Basi sote tubaki na mitizamo yetu.

Simba huwa wana nyota sana na hii michuano haswa wakiwa na timu ya kawaida.

Umesahau kipindi mnapigwa HAMSA HAMSA lakini mliongoza kundi na kutinga robo fainali mbele ya Al Ahaly, AS Vita na Al Saura tena zikiwa za moto?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Ila kweli, unashangaa tunatinga Semi final.
Mweeeeeeh, yaan hatare.
 
Waarabu wahuni tu, picha linaanza pale kwao dakika ya pili wamepewa penalti, dakika ya tano mmekula red, dakika ya 8 pressure imeshapanda tunajifunga[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mpaka kipindi cha kwanza kiishe wote tumechoka mpaka mashabiki huku Vingunguti🫣🫣🫣 tunaangalia dakika tu mpira uishe...
Kuna VAR
 
Sasa huu nao ni ujinga,Leo Mpira umemkataa na Kila mtu kaona angemtoa..

Mbona anavumiliwa Kwa kumuacha Tiba licha ya kuboronga?

Mimi sio mwana Simba Wala Tanga ila napenda Mpira na kuona Timu zetu zinajenga heshima ya Tanzania..

Na mambo ya Yanga na Simba Huwa naangalia mechi za Kimataifa tuu.

Chama ni tofauti na Tiba. Lini uliona Tiba anafanyiwa Sub mashabiki wanamuakia kocha?
 
Hongera kwa ushindi, na hasa goli zuri ambalo mchoro wake hakuna angeweza kuuchora kabla.

Nafasi ya Simba kufuzu ipo ikiwa itakuwa bora kimbinu kuwazidi hao Wydad Casablanca.

Wydad walianza kuvutavuta na kukamata wachezaji wa Simba. Ile ni ishara gani, kuzidiwa au mbinu za mchezo?

Chama apunguze zaidi mbwembwe, Kuna goli ilikuwa afunge leo.

Makocha na wachezaji watenge muda kurejea hii mechi katika video.

Ule mchezo wa away, wajipange kumiliki zaidi pale kati.

Kasi ya Wydad kule Morocco itakuwa mara dufu, ni kazi ya makocha kubuni mbinu.

Simba irejee video zote za mavurugu ya Morocco, iwe mvua, kelele, tarumbeta nk waone kawaida.

Ule mkakati wa kuitoa Zamaleki 2013 uboreshwe zaidi. Simba ioneshe haijafika hapa kwa kubahatisha.

Hakuna lisilo wezekana na Wala haitakuwa miujiza Simba kuingia nusu fainali.

Kuna watauliza kwa wachezaji gani? Ni hawahawa, mbinu na bidii zaidi Simba wanavuka kibabe.

Mengi yalisha fanywa na Simba huko nyuma, kwanini isiwezekane sasa.
 
Mechi ya leo ilikua upande wa simba. Kama kawaida waidad wakiwa away wanacheza mpira wa kupooza, kupoteza muda, wanatengeneza nafasi chache, lakini mind set yao ni either droo au ufunge lakini kwa idadi ndogo ya magoli. Hakika simba ameprove kua moja ya timu bora Africa.

Imelinda heshima ya Uwanja wa mkapa. Kwa jicho langu la kiroho kipindi cha kwanza simba alikua shinde goli 2 ukiacha la baleke. Jamaa wajanja sana wakawasha ule moshi kupooza mpira. Nahisi jamaa walichungulia wakaona goli 2 kipindi cha kwanza. Tuone Cansanlanca itakuaje
Tunashukuru kwa ushindi huu mwembamba
 
Back
Top Bottom