Kwa mendez kulikuwa daraja la kijazi..kila mmoja alikuwa anapitia hapo
Hata angecheza mwingine ungeendelea kulaumu vile vile na yote hayo ni baada ya PSG kufungwa.
Mbona hujawahi kumkosoa Mendez ktk mechi yoyote kabla ya leo?
Iweje ktk FIFA WORLD CLUB CUP 2025 ndiyo Mendez aonekane uchochoro ila si kwa mechi zingine nyingi ambapo alikuwa akiwa tegemezi kiubora?
Je Vitinha, Dembele, Desire Doue na Hakimi pia hawakuwa na ubora ktk mechi zingine mbali na mechi ya leo FIFA WORLD CLUB CUP 2025?
Ukiendelea kumlaumu zaidi ni mawazo yako ila jifunze kukubali mpira ndiyo mchezo pekee ambao haujawahi kutabirika kimatokeo.
Pia jifunze kuheshimu wapinzani wako hata kama wana madhaifu maana hawakufika fainali kwa bahati mbaya.
Kocha Luis Enrique alidai FIFA WORLD CLUB CUP ataitandika Chelsea FC zaidi ya goli 5, vipi baada ya dakika 90 matokeo yamekuwaje?
Lamine Yamal aliongea shits kwenye press conference kabla ya mechi "Kaumbwa kubeba makombe na hakuna yeyote wa kumzuia asibebe kombe la UEFA Nations league final 2025" Hukumbuki kilichomkuta ktk fainali hiyo Mkuu?
"Usijisifu unajua kukimbia bali msifu pia anayekukimbiza"
Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.