FT: Marumo Gallants 1 - 2 Young Africans | CAF Confederation Cup 17.05.2023

FT: Marumo Gallants 1 - 2 Young Africans | CAF Confederation Cup 17.05.2023

Marumo Gallants wapo nyumbani kuwaalika Young Africans katika mchezo wa marudiano ya nusu fainali ya CAF Confederation Cup kwanzia saa 1:00 usiku kwa hapa nyumbani Tanzania.

Mechi ya kwanza iliyopigwa juma moja lililopita Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Hivyo matokeo yoyote ya ushindi kwao, au droo yataivusha Yanga na kuipeleka Yanga katika fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

Kila la heri kwa Yanga, Taifa zima tupo nyuma yenu🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
Mbona hujatuambia galant hajapoteza mchezo wowote wa ligi ya CAF shirikisho msimu huu nyumbani? 🤣🤣🤣🤣
 
Tunaelekea uwanjani kumsapoti mtani
1684332554900.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni siku ambayo hakuna alieifahamu lkn ilisubiliwa miaka na miaka tangu kuumbwa kwa dunia.

Ni siku ambayo kila Mtanzania ngependa iwe upande wetu. Ni siku ya kipekee ambayo haitakiwi kupotezwa.

Eeh Mwenyezi Mungu ijaalie Young Africans SC iweze kupata ushindi siku hii ya leo nyoyo na nafsi zetu viweze kufurahi. Eeh Mungu ibariki Young Africans SC. Ikawe siku njema tupate ushindi inshallah. 💚 💚 💛 💛 @yangasc1935 #DaimaMbeleNyumaMwiko
 
Natamani wabondwe huko mpaka engineer na Gsm wapoteane huko south mana wanavihelehele Sana...Sasa kilichowapeleka huko wote hao nini? Pamoja na Simba kucheza club bingwa sikuona Mo anaenda Morocco ila hawa sasa du, kweli maskini akipata matako hayaachi kugongana!
 
Eenhee! Wanasemaga usiku wa deni haukawii kukucha na kwetu sisi Timu ya Wananchi ndo tulikuwa tunataka ifike tupate kumalizana na hizi dakika 90 zilizosalia.

Kila la kheri Timu ya Wananchi katika kuweka historia ingine.

#DaimaMbeleNyumaMwiko.
Ntakucheck baada ya mechi nikupe pole 🤣🐸🐸
 
Back
Top Bottom