FT: Namungo FC 0-2 Young African SC | NBC Premier League | Majaliwa Stadium | 30.11.2024

FT: Namungo FC 0-2 Young African SC | NBC Premier League | Majaliwa Stadium | 30.11.2024

Hahaha kocha tumbo linaunguruma haamini anachokiona uwanjani Yanga kufunga zero hawafungi wamefungwa miguu, watu watalamba ndimu na leo
Sudi kabla ya kusinya mkataba alipaswa kumtafuta Gamondi amueleze yaliyomsibu hadi kuondoka.

Sudi kama anafikiria atakuwa mwana mageuzi wa kutengeneza historia mpya basi ajitafakari upya.

Mechi ikiisha Yanga hajashunda atakuta ameletewa mabegi yake hapa hapa Lindi.
 
Viporo kurudisha watu kwenye uskani
Screenshot_2024-11-30-19-20-06-65.png
 
Sudi kabla ya kusinya mkataba alipaswa kumtafuta Gamondi amueleze yaliyomsibu hadi kuondoka.

Sudi kama anafikiria atakuwa mwana mageuzi wa kutengeneza historia mpya basi ajitafakari upya.

Mechi ikiisha Yanga hajashunda atakuta ameletewa mabegi yake hapa hapa Lindi.
Atakodishiwa Bajaj sio bodaboda imuwahishe kwao
 
🔰𝐌𝐀𝐓𝐂𝐇𝐃𝐀𝐘🔰

🏆 #NBC Premier League
⚽️ Namungo FC 🆚 Young Africans SC
📆 30.11.2024
🏟 Majaliwa Stadium, Ruangwa Lindi
🕖 6:30PM(EAT)
View attachment 3165739

KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA.
View attachment 3165883
Tukutane hapa kwa Updates...

Updates...
18:31 Mpira umeanza kwa kasi ya Wastani hapa .
Umiliki ni 50x50

Dakika 2'
Yanga wanapata kona, anaipiga Aziz K inaokolewa na mabeki wa Namungo FC
0-0

Dakika 5
Yanga wanapata free kick inapigwa haileti shida.

Dakika 10
Kibabage anashindwa kumwaga maji hapa.
Anaingia hadi 18 lakini pasi yake inakuwa Mkaa
Game on.
0-0

Dakika 12
Yanga wanapata kona inapigwa haraka haraka inaishia kwenye mikono ya kipa wa Namungo.
Game On
0-0

Dakika 15
Namungo wanatengeneza shambulizi moja zuri.
Inapigwa inatoka nje, inakuwa off target.
Mchezo unaendelea
0-0

Dakika 17
Yanga wanapata tena kona hapa.
Anaanza Aziz kona fupi, bado haizai matunda.
Ball On
0-0

Dakika 20.
Yanga wanapata kona inapigwa inaokolewa vizuri kabisa na Namungo
0-0

Dakika 22,
Yanga wanafanya shambulizi kali hapa.
Kakolanya anaitoa
0-0

Dakika 28
Yanga wanapata faulo nje kidogo ya 18.
Anaipiga Aziz
Inakuwa kona, imeanza haraka haraka.
Haijazaa matunda
Mpira unaendelea, Yanga wanafanya shambulizi hafifu, Anaokoa kipa wa Namungo
0-0

Dakika 30
Mligo wa Namungo anapata kadi ya Njano baada ya kimchezea rafu Yao Kwasi
0-0

Dakika 33
Namungo wanafanya shambulizi hatari kwenye lango la Yanga, halifanikiwi waapoteza mpira.
Ni nafasi ya wazi kabisa kwa Namungo.
0-0

Dakika 42
Aziziiiiiiii, inagonga mwamba hapa inatoka nje.
Aziz K anakosa nafasi ya wazi hapa.
0-0

Dakika 45.
Nyongeza ni 3.
Game On
0-0
Yanga wanacheza kama bata mwenye mimba anayeharisha.
 
Back
Top Bottom