Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Haya haya ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imewadia. Leo tarehe 20/10/2023 Tanzania itashuhudia mtanange wa kihistoria kati ya timu ya Simba ya Tanzania dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Mechi hii ni ya ufunguzi wa michuano ya African Football League ambayo inachezwa barani Afrika kwa mara ya kwanza.

Mechi itakuwa Mubashara Azam Sports 1HD kuanzia saa 12:00 Jioni kwa masaa ya Afrika Mashariki lakini mapema kutakuwa na sherehe za ufunguzi huku Ali Kiba akiongoza burudani.

Yanayojiri yote utayapata katika uzi huu…

Yapi maoni yako kuhusu mechi hii?

Baadhi ya Watu mashuhuri waliohudhuria tukio hili


Rais wa FIFA, Infantino (kulia) ametua Tanzania


Legendari Arsene Wenger na Moise Katumbi kwenye mkutano na Waandishi wa Habari


Arserne Wenger akiwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa

Your browser is not able to display this video.

Hali ya Uwanja mpaka sasa

UFUNGUZI WA TUKIO UMEANZA RASMI



Kikosi cha Simba kinachoanza
- Mpira umeanza huku timu zote zikisomana na kushambuliana kwa kushtukiza

- Dakika ya 23 bado ni 0 - 0

- 45' Goooooal Ahly wanatangulia hapa

HT: Simba 0 - 1 Al Ahly

Kipindi Cha pili kimeanza

- Mzamiru out - Kanoute in

- Miquisone out - Baleke in

- Kibuuuu anasawazisha hapa

- Kanouteeee anaipatia Simba goli la pili

- 60' Simba 2 - 1 Al Ahly

- 63' Karhaba anasawazishaaaa 2 - 2

80' Bado mabao ni 2-2

FT: Simba 2 - 2 Al Ahly
 

Haya haya ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imewadia. Leo tarehe 20/10/2023 Tanzania itashuhudia mtanange wa kihistoria kati ya timu ya Simba ya Tanzania dhidi ya Al Ahly ya Misri...
Asante Suley2019 nilisubiri uzi huu kwa hamu sana .

Mnyama Simba Nenda, Sisi zetu Dua na Daima Sisi tuko Nyuma yako [emoji123][emoji123][emoji123]

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Katika historia.View attachment 2786837

Somo : Mpira hauchezwi mdomoni.
Najaribu kufikiria tu

Ukai screenshot

Ukaifadhi kwenye device yako zaidi ya miezi 6

Ili uje uitumie leo baada ya kuona matokeo ya mechi na Wydad hayakuja kama ulivyo wish.

So unatafutiza timu ya kunifunga ili hii screenshot yako ionekane ya maana?

I promise you, we are Simba and we won't let you get that opportunity
 
Nina screenshots nyingi mno za hapa Jf na kwengineko kwa madhumuni mbalimbali kujifunza ,kusearch information nk yako nimeitunza kama kichekesho kwa ajili ya kufurahisha maana inanichekesha sana.

Humo zipo nyingi nyingine zina miaka lakini nimehifadhi kutokana na umuhimu wake.
 
Sema ndio hivyo ukiwa Yanga as long as sio Sunday Manara au Kikwete basi lolote linawezekana
 

Haya haya ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imewadia. Leo tarehe 20/10/2023 Tanzania itashuhudia mtanange wa kihistoria kati ya timu ya Simba ya Tanzania dhidi ya Al Ahly ya Misri...
Umepunguza utamu wa shughuli...kichwa cha Uzi kingekuwa sherehe za ufunguzi wa AFL
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…