[emoji881][emoji881]ππππππππ[emoji881][emoji881]
[emoji471] #CAFCL
[emoji460]οΈ Simba SC Vs Jwaneng Galaxy
[emoji414] 02.03.2024
[emoji909] Benjamin Mkapa
[emoji797] 7:00pm
Mungu Ibariki Tanzania!!
Mungu ibariki Simbaa
#WenyeNchi#
Hello [emoji112][emoji112] Tanzania.
Timu ya Wenye Nchi, Simba sports Tanzania hatimaye inaenda kukamilisha hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mchezo unaanza saa moja kamili usiku masaa ya Afrika mashabiki
Je Simba ataendeleza ubabe wa kandanda safi East Africa?
Je Jwaneng Galaxy atafanya aliyoyafanya 2021?
Nchi ni ile ile, Timu ni zile zile na Uwanja ni ule ule.
Welcome for the show
====== ==
Timu ya Simba inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Jwaneng Galaxy ya Botswana katika mchezo wa mwisho wa Kundi B ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jijini Dar es Salaam, leo Machi 2, 2024.
Ushindi utaifanya Simba ifuzu kuingia Robo Fainali kwa kufikisha pointi 9 hata kama Wydad itashinda dhidi ya ASEC Mimosas (imeshafuzu) na kufikisha pointi 9 pia, Simba ina faida ya kuwa na magoli mengi katika mechi baina ya timu hizo zilipokutana (head-to-head).
Aidha, Jwaneng nayo ina nafasi ya kufuzu, hilo litawezekana ikitokea imeshinda (itafikisha pointi 7) kisha Wydad ikapoteza.
Pamoja na yote ikumbukwe Jwaneng iliwahi kuiondoa Simba katika Raundi ya Pili ya michuano hiyo Msimu wa 2021/22, mchezo wa kwanza Simba ikishinda 2-0, marudio Galaxy ikashinda 3-1.
=========
Welcome for the show