Nyakati zimeisha! Simba ile ya kutisha imeisha,Simba sasa hivi haiogopwi tena,ile timu iliyokuwa inatetemesha wapinzani imekufa!
Ile timu iliyokuwa ina viongozi wafia timu Mzee Dalali, Marehemu Hanspope,Kaduguda,Mzee Magoli,Khasim Dewji, timu ilikuwa ina wavuja jasho haswaa!
Leo tunafungwa na utopolo tano halafu wachezaji wanafurahi na kupiga picha na wapinzani kwa furaha na viongozi wanatabasamu tu!!
Leo tunamlilia mchezaji mmoja mzee bila yeye hatuna matokeo! Viongozi uzungu umekuwa mwingi na udalali tu,wachezaji wanacheza wanavyojisikia tu hakuna presha yeyote wanayopata kutoka kwa viongozi, wachezaji wazee wakina Ntibazonkinza ndio tegemeo la Simba!! Upuuzi mtupu,Simba haitakaa iamke tena.
Timu imejaa siasa na wanasiasa,CEO yeye kila siku anakuja na project uchwara hakuna jipya! Timu za vijana zimetelekezwa wachezaji wamekimbia! Tunaambiwa ni timu bora africa ila huo ubora wala mipango ya ubora haipo ni ujinga tu.