Full Time | Senegal 1-1 Tanzania | TotalEnergies AFCON U-17 | Senegal Mabigwa baada ya mikwaju ya penati 4-2

Full Time | Senegal 1-1 Tanzania | TotalEnergies AFCON U-17 | Senegal Mabigwa baada ya mikwaju ya penati 4-2

Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17), maarufu kama Serengeti Boys, leo inashuka dimbani kuivaa Senegal U-17 katika mchezo wa mwisho wa michuano ya TotalEnergies AFCON U-17.

Mchezo huo utaanza saa 4:00 usiku katika Uwanja wa Stade Moulay Hassan, Rabat, Morocco, ambapo Tanzania U-17 (Serengeti Boys) itakuwa ikimenyana na Senegal U-17 katika fainali ya michuano ya CAF U-17 Africa Cup of Nations Morocco 2026.

Senegal wanakuja wakiwa na uzoefu mkubwa, nguvu, na kasi, lakini soka la kisasa limeonyesha kuwa dakika 90 ndizo zinazoamua na hakuna timu ndogo tena Afrika.

Swali linarudi kwako shabiki wa soka:
  • Je, mbinu na uzalendo wa Taifa Stars utatosha kuwazuia Simba wa Teranga?
  • Au uzoefu na ukongwe wa Senegal utatawala mchezo wa leo?
Kete yako unaitupa wapi leo? Weka utabiri wako hapa chini!


Game ipo on fire dakika 5 ya mchezo

Dakika 7 Serengeti Boys wanafunga goliiiiii zuri sana

Dakika 11, Serengeti boys wanapeleka moto

Dakika 22, Bado vijana wa Tanzania wanaongoza

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimekamilika kibabe kabisa Serengeti Boys wakitoka na uongozi wa goli moja kwa sifuri

Good
 
Wameshatia siasa mie nipo upande wa senegal, kwa hali hii hata wacheze na jiwe, mie nitashabikia jiwe
Duh!...Siasa kwa timu yoyote huwezi kuikwepa zama hizi nchi hii.

Kwa hiyo watakie heri vijana mengine yanapita tu.
 
Naona Senegal wameanza kipindi cha pili kwa ukaidi sana; naamini watamwagiwa maji yu
 
Back
Top Bottom