Yanga hii sasa ni ya moto sana na ina mambo mengi mazuri, km kucheza kwa spidi , fitness imerudi, kutengeneza nafasi za kufunga, kukaba kwa nguvu kitimu kipindi cha kwanza na kila mechi kufanya sub 5 kuweka nguvu mpya na kwa muda sahihi. Maua mengi kwa Ramovic
Bado timu ina shida kupasua ngome za wapinzani kupitia katikati , Aziz Ki ni mzito kutoa pasi, timu kuridhika baada ya kufunga, kuacha kukaba kwa nguvu kipindi cha pili, wachezaji wengi kupenda mno kurudisha nyuma mpira, na baadhi ya nyakati baadhi ya wachezaji kulazimisha kufunga badala ya kutoa assist, leo Mudathir kazingua sana katuboa sana kama angempa pasi Dube lilikuwa goli la wazi la nne, kwani Muda ana shida gani aambiwe kutoa assist si lazima afunge ye si striker, Pacome anao anao sana badala ya kutoa assist watu wafunge sijui alikuwa anaenda wapi na mpira wenzake washafungua ye yumo tu. Akumbushwe.
Otherwise Yanga inarudisha makali yake kwa kasi.
Maandalizi ya kuifunga Simba yaanze sasa.