Hujathibitisha Mungu yupo.
Kiukweli watu wanaisema Mungu yupo ndio wana kiburi.
Wamejiwekea kiburi cha kusema wanajua chanzo cha ulimwengu, na chanzo hicho ni huyo Mungu wao.
Sisi tunaobisha ni watu wanyenyekevu sana.
Tunajua ulimwengu ni mgumu sana kuuelewa, tumejishusha kwa unyenyekevu tukisema kwamba ulimwengu huu maswali yake ni makubwa sana, na hili jibu jepesi la Mungu ni kiburi, tena cha kijinga.
Unyenyekevu wetu unatutaka tukubali hatujui majibu, tufanye uchunguzi kujua majubu zaidi kuhusu chanzi cha ulimwengu, maisha na kika kitu.
Kwa hivyo, you have it backwards.
Watu wanaosema wao wanamjua Mungu ndiyo wenye kiburi.
Sisi tunaohoji hii imani na kutafuta majibu ya kina ni wanyenyekevu sana, tunajua ulimwengu una maswali magumu yasiyotaka kukurupuka kwa kutoa majibu ya kiimani ambayo hayapi kwenye research.