Uchaguzi 2020 Furaha Dominic Jacob mshindi wa kura za maoni CCM jimbo la Kawe ni nani?

Na wewe chawa tu, watu wanahitaji CV yake, wewe unaropoka kiuswazi uswazi tu
 
Binafsi simjui kabisa, na huenda wengi wetu humu hatumjui kabisa.
 
yupo powa sana dogo.. tuna kutana nae sana mlimani city.. na hana shobo ana nidhamu.. mengine sijui.. 🙂

Bora wewe umesema yuko ni mtu poa sana lakini mengine sijui.

Kwa sababu wenye umri kama wangu watakumbuka campaign stump ya kwanza ya Ally Hassan Mwinyi watu waliuliza who the hell is is guy? Campaign Manager Julius Nyerere akawa anasema ni jamaa mmoja mpole, mkarimu, hana shobo, hana chuki, hana noma...

Tukampata Mzee Ruksa na baadae prototype yake kijana Jakaya na baadae ilikua aje Kijana Edward.

Ukarimu wao ulisaidia nini taifa hawa watu? Management ya nchi ilikuwaje chini ya hivu vijukuu vya Mtume?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…