Futa milele leseni zote za madereva waliogoma bila kufuata utaratibu.

Wee endelea kula kiyoyozi mkuu ,ni rahisi sana wewe kuongea hivyo ishu yakuiba mafuta ni tamaa ya mtu mmoja mmoja siokwamba madereva wa nchi nzima wanaiba kwa taarifa tuu hata hao vigogo huko wizarani wengi ndio wenye magari kwaiyo ni vizuri kutatua shida yao wasikilizwe kama walivoomba Rais au waziri mkuu atoe tamko na atatoa tuu maana naye ana mabus. Mnyonge mnyongeni haki zao wazipate
 
Lakini umesikia baadhi ya hoja...

Polisi (traffic) anakaa sehemu anasubiri basi kama 3 zipite... Sehemu ambazo wanasubiriwa ni zile zenye mstari mmoja ambapo huruhusiwi ku overtake

Sasa trafic anakuwa na private car... Anayapita mabus..makusudi Kisha anaendesha speed 30 mbele yao.. Sehemu ambayo Haina speed limit.. ambapo mabus yanaruhusiwa Kwenda speed 80...

Sasa yule Polisi anakuwa mbele ...mnaenda naye hata kilometer 10 kama haziruhusiwi...anafanya makusudi ili ufanye overtaking ...mbeleni mnakutana na kisanga Cha leta leseni... Katoe laki 5..

Nyingine ..Polisi wanawatega sehemu inaruhusiwa ku overtake..baada ya meter kama 3 ..Kuna mstari wa kuzuia kuovertake.. tuseme wakati unamalizia kulipita gari unakutana na mstari wa kuzuia overtake.. traffic anachukua leseni na bila hata 50k ...hakupi au anakuweka ndani
 
Sawa mkuu nimekuelewa
 
Hata hujui kitu namna serikali inavyofanyakazi zake. Huduma inarejea wakati akidakwa mmoja baada ya mwingine waliosababisha usumbufu kwa taifa.
 
Hela ya dawa ya viatu tu hiyo. Wewe kama dereva fanya udereva wako uliofundishwa, tegua mitego hiyo ya traffic kama wewe ni dereva kweli.
 
Hujui kama unapewa leseni ya kubeba abiria na route/njia kwa mashariti fulani? Walichokifanya ni kuhatarisha usalama wa taifa. Huo mgomo kama utakuwa haukufuata taratibu za kugoma watakuwa na hatia ya kuhujumu usalama wa taifa na uchumi. Walioanzisha mgomo wakae mkao wa kula.
 
Hela ya dawa ya viatu tu hiyo. Wewe kama dereva fanya udereva wako uliofundishwa, tegua mitego hiyo ya traffic kama wewe ni dereva kweli.
Mimi ni dereva.. private

Halafu acha kuwa na upande ..hasa Hawa Askari..mi huwa naendesha gari kwa mambo yangu binafsi..lakini ukikutana nao barabarani ni balaa...

Anakukagua utafikiri una ebola...akiona huna kosa anaanza... Nipe nyekundu..jua kali.. Sasa Hawa jamaa utafikiri hawalipwi mishahara.. au wanajua Kila mwenye gari ni ATM ya benki ?
 
Serikali haina hasara, inaweza kuleta wawekezaji kutoka Kenya, Uganda, Rwanda kwenye usafiri wa abiria ndani ya nchi. Kuna vitu vingine vinafanywa kwaajili tu ya kulinda ajira za ndani. Serikali inaweza kuleta wachina hapa wasafirishe watu kutoka Dar kwenda Mahuta.
 
Tena wakileta mzabuni Mchina tutasafiri kwa bei nafuu sana😄
 
Hata mimi huwa wananikamata sana, lakini kila wakinikamata ni kweli nimefanya kosa au gari ina kosa. Ninachofanya mimi ni kukubaliana na kosa langu na kuomba msamaha, kama wakikataa kunisamehe siwapi rushwa niko tayari waniandikie kosa na kulipa 30,000 nikifika au nikirudi kutoka safari yangu. Kwa hasira unaweza kukuandikia makosa mawili ulipe 60,000 lakini lakini sijali bora nilipe kuliko kuwapa 5000. Kwa tabia yangu hiyo huwa hawanikamati ovyo kwa kuona wanapoteza muda wao bure kwa mtu ambae hawatapata kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…