View attachment 3294480
Habari nilizopata kwa Chanzo changu cha kuaminika, kambi hii inatangaza kuanza mikutano nchi nzima kuongea na wana CHADEMA na wananchi juu ya msimamo wa Kutaka reforms na kushiriki uchaguzi.
Maandalizi yote yako tayari na watakuwa na magari kila mkoa na helkopita 2.
Hawa wakizunguka basi wananchi wawatambue na kufuatilia mali zao na biashara zao wajue zilipo Waanze kuzisusia .
Kama ana gari la abiria wasusie kupanda popote bora kuahirisha safari .
Kama Kama ni ana bar hakuna kunywa kwenye baa yake .
Kama ana hoteli au mgahawa hakuna kule kwenye mgahawa wake .
Kama anauza mayai hakuna kununua mayai yake na akionekana amemuuzia mtu basi hata yule aliyeuziwa hakuna kununua kwake .Kama ni Azam basi hata bidhaa zake tunaziacha ni bora tununue kwa Mo.
Kama ana Fuso ya mizigo hakuna kukodi gari lake .
Anauza genge sokoni hakuna kununua .
Akionekana kijana kwenye maeneo ya stendi amevaa nguo ya CCM au kofia ya CCM halafu anauza maji hakuna kununua maji yake .
Akionekana ni Chadema halafu anapinga reform huyo ni muuaji hafai kabisa kupewa ushirikiano wa kibiashara . Wanaoitwa wabangaizaji ndio wateja wao . Hakuna siku Mbowe au Mrema atauza maji barabarani sasa hawaoni uchungu wa wauza maji kuchagua kiongozi wao halafu Tume ya Samia inakataa kumtangaza .
MwanaCCM yeyote na hao G55 Kama ana duka la dawa hakuna kununua kwake .
Kama ana bodaboda hakuuna kupanda .
Kule Kenya Gen Z walienda mbali zaidi wakichoma mali zao . Huku tususie ili pesa wanazohongwa na CCM wasiweze kuzifanyia biashara maana tamaa ndiyo inayowafanya wachache vurugu ndani ya chama . Wangekua majasiri wangeifanyia vurugu CCM ili walete tume huru na katiba mpya . Yaani Samia anauza kila kitu lakini wanakaa kimya hata Mamwabukusi alipoitisha maandamano waliompinga na kuungana na Wauza nchi kwa sababu ya pesa za DP World basi hii nchi hawaitaki wanataka kutumia damu za watu kama kafara za biashara zao .
Mrema alikua anapiga kelele kila siku ili katiba mpya ipatikane na bila katiba mpya hakuna uchaguzi halafu leo anasema eti Chadema iingie kwanza uchaguzi . Yaani hata ukimuuliza mgambo yeyote au mwalimu yeyote hata polisi yeyote atakuambia Kura haziheshimiwi ,kura zinakuja na maelekezo yake na anayepinga anaonekana adui ndio maana Walimu wanakaa kimya na polisi wanatekeleza majukumu yao ya kuwakamata wale wanaopiga kelele kuzuia wizi wa kura kwa sababu hawana namna ya kuacha kutekeleza majukumu wanayopewa na msimamizi kuwa mtoe huyu nje anafanya anavuruga zozi la uchaguzi .
Sasa mfano kama alivyofanya yule dada mmoja tu kule Dodoma kuwakamata na kupiga kelele kuzuia wizi wa kura je wa alifanya hivyo watu mia tano kwenye kila kituo huo uchaguzi utafanyikaje ?
hata kama walinzi wana bunduki bado hazitoshi nchi hii na CCM labda watoe silaha zote kwenye maghala na kila mgambo ashike bunduki na wale migambo feki watoto wao wanaovalishwa uniform za mgambo ili wapate pesa za uchaguzi bado hawawezi kuzuia maandamano ya watu mil. 5 nchi nzima . Wanajeshi na polisi nchi nzima hawazidi laki moja na nusu pamoja na majeshi yote hawafiki laki Tatu . Sasa wetu Laki tatu wanawezaje kutumia bunduki kwa Raia wake zaidi ya mil.10 kwa faida ya wezi wa kura . Hapo ni lazima Jeshi likatae huo ujinga wa Wanasiasa wa CCM wasio toshekana na mali na madaraka kwa miaka 60 bado wanafanya uchaguzi wa kivita kwenye nchi ya kidemokrasia .