This is a new dawn for Africa.Tawala zote kandamizi ambazo zimeibia watu wao rasilimali wakae chonjo,I mean zote,without exception,ikiwemo Tanzania.
Haiwezekani baada ya miaka sitini na tatu ya Uhuru tukiwa na rasilimali nyingi kiasi hiki,bado watu wetu wengi hawana maji,na hata hao wachache wanaopata maji si safi na salama;watu wanakufa kwa sababu hawana huduma za afya;watoto wengine hawasomi kwa kuwa wazazi wao hawawezi kuwapeleka shule kwa kuwa hawana michango,madaftari na kalamu au uniform; Elimu inayotolewa ni chini ya kiwango,shule hazina mazingira mazuri ya kusomea na vitendea kazi;watu wetu hawana nyumba bora za kuishi ;watu wetu wanapata mlo mmoja tu kwa siku na wengine hawapati kabisa nk.nk..
No, lazima kama Watanzania tufike mahali tuseme hapana hii haivumiliki tena inatosha,na tufanye kitu ambacho kitatutoa kwenye uonevu huu.