Gari Brevis tamu sana kwa safari ndefu!

Gari Brevis tamu sana kwa safari ndefu!

Udereva wa kujihami ndio udereva makini Duniani kote!Mbio barabarani sio udereva Bali ni kuwa na Afya ya Akili ndogo,na ni Hatari kwa anayeendesha mbio na kwa watumiaji Wengine wa barabara hasa watoto na akina mama wajawazito wanavuka barabarani.Namshukuru Mungu,nimeendasha magari kwa Sasa ni Miaka 20,Sijawahi pata ajali yoyote.Labds nyenyele na mchwa ndio nimewagonga,.Mtu kujisifia kukimbiza gari barabarani ni ugonjwa wa Akili sio bure.Sawa Kifo ni Kifo!
Wewe ungekuwa na afya ya akili ungenionea wivu wakati hunijui! Lazima nikuchambe tu ili twende sawa na hukulazimishwa kuchangia chochote umejileta tu
 
Ok sawa Kijana nimekueleea ila Naendelea Kukukumbusha na kukushauri Kuwa Speed si zaidi ya 80 Kwenye Maeneo yasiyo na watu Na speed 50 kwa maeneo mengi na Speed 30-50 Kwa maeneo ya Watu..

Usitembelee Speed 150 Kwenye Gari ukajiona Mjanja..
Ni Ulimbukeni na Nilimbukeni peke Yake Atayekwenda Speed 150 Na akajisifu..

Vijana Okoeni maisha Yenu na Kuambizana Ukweli bila kupepesa macho Speed Kubwa Inaua na Inasababisha Ajali..

Haijalishi utanitukana Ama utaniona Mchawi ila kwa speed Hiyo naomba Nikuambie Kuwa Tumechoka Kuona ajali barabarani ambazo zinasababishwa na Uzembe wa Dereva,..

Kuhusu Magari nimeanza kuendesha Magari huenda hata Miaka hiyo hujazaliwa Nimeanza kuendesha One 10 na Chaser Enzi hizo miaka ya 1990 Nikiwa Chuoni mwaka wa nne sijui Ulikuwa na Miaka Mingapi?

Tumechoka Kupokea Kesi za Ajali barabarani Mahospitali zinazosababishwa na Uzembe wa Mtu kwa makusudi kwa kuendesha spidi zaidi ya Inayotakiwa na kushindwa kucontrol gari..

Mimi kama Mzazi wako Nakuonya Kwa hiyo speed Unayoendesha ukichukia Chukia na ukitukana Tukana
Dr, mwaka 1990 ulikua Chuo tena mwaka wa 4? Shikamoo Dr 🙌.

Btw Ushauri mzuri kwa kijana mwendokasi unaua
 
Nina gari Brevis Cc 3000 hii chuma nikitangulia usinifuate aisee, gari inakimbia sana na imetulia kabisa safari ndefu huwa nakimbiza huku nacheka tu jana nimetoka Dar asubuhi mpaka Mwanza gari imetulia kabisa ukiwa speed 150 unaona kama iko speed 50.

Nina prado ila prado huwa naliacha nasafiri na brevis inakimbia sana na inachanganya haraka.
Unaacha Prado unachukua Brevis si ndio?
 
Siku Ukipata Ajali uje Pia Utuambie..
BTW Brevis ni gari Iliyopitwa na wakati na Wengi wanaziuza sana siku hizi..

Nowdays Kupata Brevis Namba DZ au DX au DY Kwa Shilingi Milioni 4 au Tano ni Kitu cha kawaida sana..

Ukitaka Sports Car Jaribu Crown
Kweli mkuu Mimi ni dalali gari aina ya Brevis haziuziki
 
Mkuu, ondoa hii mentality. Malengo ya madereva timamu si kushinda mbio unless upo kwenye michezo ya kulipwa.
Mimi sikuongelea mbio watu ndiyo wanakurupuka walio wajinga humu sijui wametoka fb nimesema nimetoka nayo dar mpaka mwanza na hii gari nilinunua mpya kabisa kwahiyo nimetumia muda mrefu lazima niwe nimewahi kukimbiza speed zote maana wakati mwingine unakuwa na haraka ila majinga mengi mengi humu yanapenda kudakia tu na kurefusha mambo
 
Nina gari Brevis Cc 3000 hii chuma nikitangulia usinifuate aisee, gari inakimbia sana na imetulia kabisa safari ndefu huwa nakimbiza huku nacheka tu jana nimetoka Dar asubuhi mpaka Mwanza gari imetulia kabisa ukiwa speed 150 unaona kama iko speed 50.

Nina prado ila prado huwa naliacha nasafiri na brevis inakimbia sana na inachanganya haraka.
Mkuu, jaribu na Toyota Mark X (DBA-Grx 120), ni chuma kwelikweli. Kina comfortability ya maana, acceleration ya kufa mtu na stability ya kutisha barabarani. Tofauti na Brevis, Mark X haili mafuta kijini jini na pia ina umbo au sura yenye mvuto.

NB: Maneno yote yenye utata ni kwa lengo la kusifia na sio vinginevyo.
 
Back
Top Bottom