Gari Brevis tamu sana kwa safari ndefu!

Gari Brevis tamu sana kwa safari ndefu!

Ok sawa Kijana nimekueleea ila Naendelea Kukukumbusha na kukushauri Kuwa Speed si zaidi ya 80 Kwenye Maeneo yasiyo na watu Na speed 50 kwa maeneo mengi na Speed 30-50 Kwa maeneo ya Watu..

Usitembelee Speed 150 Kwenye Gari ukajiona Mjanja..
Ni Ulimbukeni na Nilimbukeni peke Yake Atayekwenda Speed 150 Na akajisifu..

Vijana Okoeni maisha Yenu na Kuambizana Ukweli bila kupepesa macho Speed Kubwa Inaua na Inasababisha Ajali..

Haijalishi utanitukana Ama utaniona Mchawi ila kwa speed Hiyo naomba Nikuambie Kuwa Tumechoka Kuona ajali barabarani ambazo zinasababishwa na Uzembe wa Dereva,..

Kuhusu Magari nimeanza kuendesha Magari huenda hata Miaka hiyo hujazaliwa Nimeanza kuendesha One 10 na Chaser Enzi hizo miaka ya 1990 Nikiwa Chuoni mwaka wa nne sijui Ulikuwa na Miaka Mingapi?

Tumechoka Kupokea Kesi za Ajali barabarani Mahospitali zinazosababishwa na Uzembe wa Mtu kwa makusudi kwa kuendesha spidi zaidi ya Inayotakiwa na kushindwa kucontrol gari..

Mimi kama Mzazi wako Nakuonya Kwa hiyo speed Unayoendesha ukichukia Chukia na ukitukana Tukana
Nina uhakika hii comment hatajibu tena umeongea ukweli mchungu
 
Kwahiyo gari ikipitwa watu wasinunue kwenda huko au unataka niitupe ili ufurahie wivu mbaya sana

Gari ni matunzo dogo hata kama ni ya zamani ni matunzo tu ukiitunza vizuri gari na kukarabati kila siku utaiona mpya
Ubaya wa jf unaweza tukananana na baba yako au baba yako ukamwita dogo na usijue jaribu kutumia ustarabu kwenye upande w lugha hata kama hatujuani
 
Wewe ungekuwa na afya ya akili ungenionea wivu wakati hunijui! Lazima nikuchambe tu ili twende sawa na hukulazimishwa kuchangia chochote umejileta tu
Nikuonee wivu kwa brevis!Acha dogo kujiona umepata,sisi wa miaka 1970,Tuiendesha landlover 109,Tuliipa chupa tupu Brevis karatasi la mgororo,nione wivu mi mumeo!
 
Sasa land Rover na brevis ipi imepitwa na kwa nini Land Rover zipo mpaka leo ujinga wenu muwe mnapeleka kijijini kwenu
Bahati mbaya, kijijini Kwetu hatuna washamba kama wewe,sisi huku Mbeya gari kama hili unalojisifia nalo Tunaliacha katumba!Maana ni la kwendea sokoni tuu, wewe unataka Dar_Mwanza ndege huzioni!Unajichosha sana.
 
Speed sio udereva, speed ni ugonjwa, speed ni Kifo Cha kujitakia, speed majeraha ya kukosa akili, speed ni kukwepa majukumu, speed ni ushamba kama ushamba mwingine, speed sio kuonyesha wewe ndio unamiliki gari na barabara.nimelogoff.
 
Speed sio udereva, speed ni ugonjwa, speed ni Kifo Cha kujitakia, speed majeraha ya kukosa akili, speed ni kukwepa majukumu, speed ni ushamba kama ushamba mwingine, speed sio kuonyesha wewe ndio unamiliki gari na barabara.nimelogoff.
Utapata majeraha utakufa hata kama unatembelea baiskeli siku yako ikifika imefika
 
Mna hasira sana lazima mtakuwa wachawi sio kwa wivu huo
Hatuna hasira dogo,tunakuweka sawa na ushamba wako,uwe kwenye mistari ulioonyoka!.Umelata Uzi humu ukidhani utasifiwa na Upumbavu wako,umekutana na Chuma kikoli moto Hii ndio JF members!Sisi tutakupa kwa kadri ya akili zetu Bado wengine wapo kanisani wanakuja na Nondo zilizopakwa Mafuta!
 
Back
Top Bottom